Wanachama wa CCM tawi la DMV tunaungana na watanzania wenzetu popote duniani kutoa salamu Za rambi rambi kwa wanachama wa chama cha chadema kwa kuondokewa na kiongozi wao mheshimiwa Bob Makani.
Mheshimiwa, Bob Makani atakumbukwa kwa hoja zake za kuchangia mambo mbali mbali yaliyoweza kulijenga taifa la Tanzania. Wanachama wa chadema wameondokewa na kiongozi imara katika safu za vyama vya upinzani.
Sisi wanancham wa CCM tawi la Washington, DC Maryland na Virginia tunatoa salamu za rambi rambi kwa ndugu wa marehemu na wanachama wa chadema popote duniani.
Poleni sana
Katibu wa ccm
Tawi la ccm-DMV
Yacob Kinyem
Marekani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...