abal Khayr Maalim Michuzi

Mimi nina langu jambo. Nahitaji nikopwe lakini huyo ninayetaka kumkopa anasema kuwa nikitaka niandike ubeti walau mmoja wa kuomba mkopo wa kiasi cha ngawazi 40 (shilingi elfu 40) kisha nikuletee ili dunia nzima ipate kuusoma ndio ataweza kunipa huo mkopo niutakao. 

Sasa Mindhal leo ni Jumatatu basi nimeona si haba nikaweka mambo bayana kama huyo mkopwaji alivyosema na akijibu nakupa riksa uweke vitu majibu yake wazi ili watu wote wapate kujua kajibuje ubeti wangu? . 

Sina hakika kama naye atanijibu kupitia hapa au la lakini baada ya kufikiria kwa kina nimeona itakuwa si vibaya nikampa hiki kipande toka kwa mshairi aliyeishi kule VOI, Kenya kwa jina la Muyaka al Ghassani kwenye karne ya 18.

sasa kwa huyo mheshimiwa napenda kumwambia hivi:

Hodi bwana nimekuja, nina shida na tatizi
Nijilie kutaka haja, arobaini ghawazi
Tazileta kwa pamoja, siku mbili hizi hizi
Tafadhali nikopeshe, haondoe haja yangu


-(ni mimi nduguyo Wimbi la Mbele).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2012

    Wimbi la Mbele:

    Mkopwaji amekupa jukumu hilo kwa kuwa kwa sasa pana uhalisia mkubwa kwa wengi wakopaji na mitazaqmo kama hii hapa chini:

    (1.)Kukopa Harusi kulipa Matanga,
    (2.)Kukopa asali kulipa shubiri,
    (3.)Kopa nikidai changu niwe mbaya,
    (4.)Kopa wakati wa kulipa ukimbie,

    Ndio maana Mkopwaji amekupa jukumu hilo ili ukilinganisha na dhana hizo nne (4) hapo juu ujielewe kuwa kwenye kulipa utaleta tabu tu!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2012

    Mkopaji umefanikiwa,
    kutunga beti muruwa,
    chochote kitachokuwa,
    elfu arubaini utachukuwa,
    lakini uzirudishe powa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2012

    Aaa wapi, Huja msifia kama yeye ni pedejee wa ukweli? Hupati kitu hapo!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2012

    Inamaana hali imekuwa mbaya mpaka watu kukopana wanaamua kuandika mashairi ndio hiyo arubaini ngawazi zitoke?

    Haya tutasubiri huyo mkopwaji atajibu nini kama atazitoa hizo pesa au la.

    Nimemgoogle huyo Muyaka lakini sijapata profile yake. anaposema aliishi kwenye karne ya 18 ana maana gani au aliishi 1980s na akina Shaaban Robert?

    ReplyDelete
  5. Shida haina adabu, khasa ikikuzidia,
    Waja watakuadhibu, hadi fika kukidhia,
    Shurutishwa ya ajabu, 'hewallah' haitikia,
    Katu hawana aibu, hadhiyo hukushushia.

    Pengine takuitika, na hajayo kukidhia,
    'Ghawazi' ulozitaka, hwenda akakupatia,
    Hajayo kimalizika, mbio kumrudishia,
    Ila "utu' kakiuka, umati kuunadia.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2012

    Umepewa Mashariti kwa ile hulka yako mbaya ewe Mkopaji:

    Tatizo wewe Mkopaji unapokuja kutaka kukopa unakuwa Mstaarabu ukiwa mnyonge na mikono nyuma!

    Ile kwaaa Mkopo umepatiwa mkononi unaondoka ukiwa umechangamka usoni na unapata matumanini!,

    Lakini siku ukitakiwa kulipa Loooo, tabu inaanza unakuwa Mkorofi, Mbabe, Ngumi mkononi,unakuwa unaijua sana sheria ya kuruka na kukana ya kuwa ulikopeshwa!, unakuwa Jasiri na Msumbufu!

    -Simu muda wote unazima!
    -Ukipigiwa simu muda wote haipatikani!
    -Simu ikiita unakata!

    Hii yote ndiyo tabu yako Mkopaji ukishapewa ndio maana unapewa shariti la kutunga Shairi kabla ya kupewa mkopo!,,,

    Mkopaji na Walimwengu mpo hapo?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 18, 2012

    AL HABIB MICHUZI
    Inaonekana kuwa huyo mlengwa wa hili shairi eidha hajaliona au anamvutia muda

    Nashauri liwekwe juu kwa saa 24 mpaka mkopwaji atakapo kuja rasmi na kumjibu vilivyo huyu mkopaji.

    Tafadhali iweje juu hii AL HABIB

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 18, 2012

    Ama kweli nimeamini:

    Kukopa Sherehe kulipa mapaka Polisi!

    Ndio maana Wakopwaji wanawapa Wakopaji mashariti magumu na ya 'kutweza' ya msaada kama Mwingereza!

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 18, 2012

    sasa NGAWAZI ndio nini?

    kweli michuzi iweke juu huyo mkopwaji anaweza kuiona hii

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2012

    Mkopaji kiama chake kikubwa ni kuijua sana Sheria ya kuruka na kukana!

    Anapokuja kukopa unamuamini kwa
    kumpatia mkopo bila Kuandikishiana Mkataba wala Mashariti !

    Wakati ukitaka ulipwe taona Mkopaji anasema 'Upo wapi mkataba wa makubalinao ya kuwa umenikopesha?'

    Unaona sasa tabu inaanza!

    Ahhh wewe Mkopaji si ulikuja kukopa ukiwa unatia huruma kabisa mnyonge na mpole ?

    Ni wewe kweli umekuwa jasiri wa kusema hivi?

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2012

    Ohhh wewe Mkopaji umekuja ukiwa Bwege kabisa lakini kipindi cha kutakiwa ulipe unakuwa Shujaa wa kukataa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...