Dhana ya kwamba shule zote za kata ziko katika mazingira magumu na hazifanyi vema katika maendeleo ya elimu hapa nchini si sahihi kwani kuna baadhi ya shule za sekondari za kata ambazo zina maendeleo mazuri sana kitaaluma kushinda hata zile shule kongwe za serikali na shule nyingi za binafsi. Mdau Abraham Lazaro wa Shirika la HakiElimu alifanya ziara hivi karibuni katika wilaya ya Arusha na kuitembelea shule ya Sekondari ya  Kaloleni.Pichani ni Shule ya Kaloleni Mjini Arusha iliyoanzishwa mwaka 1998, ilishika nafasi ya 12 kati ya shule zote 137 zilizofanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2011 katika mkoa wa Arusha.
Motto wa Shule “ Matunda ya elimu huwa ni matamu lakini.......” Nidhamu ni kitu ambacho kinazingatiwa na uongozi wa Mwalimu Munga ,usiombe ukutwe na makosa , hii ni siri kubwa ya mafanikio waliyonayo shule ya Kaloleni.
Jengo la utawala na ilipo maktaba ya shule ya kata ya Kaloleni lilojengwa kwa ufadhili wa JICA.
Mwalimu Mkuu Msaidizi Mrs Machange M.J akifanya mahojiano na mwandishi.
Sayansi bila vitendo haiwezekani, shule hii ina maabara za masomo yote matatu ya bailojia, fizikia na kemia.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2012

    napenda kusahihisha kuwa Kaloleni secondary Arusha sio shule ya kata.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2012

    Hongereni kwa mafanikio, ila picha zilizop zinanitia mashaka juu ya hayo mafanikio! Hata kupiga rangi na usafi wa mazingira mpaka wafadhili?

    ReplyDelete
  3. emmanuel enockJune 14, 2012

    mi mwenyewe nimesoma hapo,.1999 ndo nlianza form one,.tulikua ni waasisi wa shule hiyo..kwakweli mwalimu Mkuu Munga ambaye ni headmaster wa kwanza wa shule hii..alikua anajitahidi sana kudumisha nidhamu shuleni..pia alikua anamfahamu kila mwanafunzi na mzazi wake..hicho nikitu kingine kilicholeta mafanikio hapo...ila sidhani kama kaloleni sec ni shule ya kata....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2012

    Hii Shule siyo ya Kata hii shule ipo katikati ya jiji na ina walimu wa kumwaga na vifaa vyote vipo. Huwezi kuilinganisha na shule za kata zenye walimu wawili au watatu, hii ina walimu wa ziada na wengine hawana kazi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2012

    Mara nyingi mafanikio ya shule yanatokana na ari ya waalimu. Niko hapa Arusha na ninaamini kuwa waalimu wa shule hii wanataka wanafunzi wao wafanye vizuri na wanajituma kwa kujua kuwa ualimu ni "wito" kama vile ushekhe, upadri, uchungaji au udaktari. Hapa ninapoongelea masheikh, mapadri, wachungaji na madaktari ninaongelea kuhusu wale ambao shughuli hizo SI kazi tu ya kawaida bali ni imani na "mission" zao za dhati. Waingereza wanaziita fani za ualimu na udaktari "the noble professions".

    ReplyDelete
  6. Shule ya Sekondari ya Kaloleni kwa mujibu wa Serikali ni shule ya Kata,kwa usahihi zaidi tembelea tovuti ya wizara ya elimu http://bit.ly/Kpddg8 utafhamu zipi ni shule za kata, binafsi , serikali etc pia Manispaa ya Arusha ilithibitisha kuwa ni Shule ya Sekondari ya Kaloleni ni ya Kata.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 14, 2012

    Unayesema sio shule ya kata, elezea kwa nini siyo ya kata

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 14, 2012

    Waheshimiwa naomba mnijuze. Mimi nilikuwa najua shule za kata ni shule zilizokuja kuanzishwa na Kikwete alipoingia madarakani kama raisi akaweka mpango wa kuwa na shule ya secondari kila kata. Tukiangalia kikwete ameingia madarakani mwaka 2005. Shule hii imekuwepo toka miaka ya 90 hivyo mhishimiwa/ serikali/manispaa inaposema shule hii ni ya kata wananichanganya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...