Ofisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Bi. Jane Matinde (kulia) akitoa zawadi ya simu kwa mmoja wa wakazi wa mji wa Mtwara, Prisca Yonasi, aliyejitokeza katika hafla ya uzinduzi wa promosheni ya Jiunge na Supa
5 ya Airtel katika uwanja wa Mashujaa, Mkoani Mtwara
Wakazi wa Mtwara, Shabani Issa Zuberi (kushoto) ambaye ni bubu na asiyesikia akichuana na Kassim Rashidi kucheza muziki katika hafla ya uzinduzi wa promosheni ya Jiunge na Supa 5 ya Airtel katika uwanja wa Mashujaa, Mkoani Mtwara jana. Shabani alishinda.
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza katika uzinduzi wa promosheni ya Jiunge na Supa 5 ya Airtel katika uwanja wa Mashujaa, Mkoani Mtwara jana.
Baadhi ya wakazi wa Mtwara wakijiunga na Supa 5 wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo mjini Mtwara jana. Anayewaunganisha na Bi. Eva Mrutu wa timu ya mauzo ya Airtel.


Jamani hiki kizazi kipya mbona daily kula starehe a.k.a bata tu. Nadhani future ya nchi yangu Tanzania iko mashakani sana maana kwenye elimu ndio div failures zinaongezeka, kwenye ngono ndo zinazidi,kwenye kujirusha ndo hakukamatiki. Eeh Mungu wasaidie hawa taifa la kesho la nchi yangu Tanzania
ReplyDeleteMakampuni makubwa hususan ya simu yanaandaa matamasha haya, wananchi wanajirusha na kujiunga na mtandao wao.Mlala hoi anampa bepari ulaji, maskini hana mawazo ya kujikwamua kiuchumi, anakenua menu kwa tamasha litakalofuata (Hakosi).Ukimkosoa anakuja "mbogo", kazi hawataki kufanya wanataka kuwa ma "modo", wasanii nk, nakubaliana na mdau wa kwanza, Mungu ibariki Tanzania.
ReplyDeletewewe mdau , inaonekana huko uliko,basi ni box tu kila kukicha na huenda unabeba box sehemu 2 au 3 ili angalau uyamudu makali ya maisha ya huko,kwenye kisanduku chako cha barua hapo nje ,hakuna hata barua moja ya kutoka kwa ndugu au rafiki, ila ni barua tu za makampuni yakidai ulipe bili zako, sasa kweli mshikaji utaupata muda wa kwenda kujirusha ??? hapo ulipo una presha ya kufa mtu,kodi chumba kimoja ni $ 700 kwa mwezi,hapo bado nauli ya basi ya kila siku ambayo tuseme ni dola 2 kutoka Magomeni hadi posta,wakati sisi huku tunalipa sent 10 na kodi yetu kwa mwezi ni shilling elfu 30 kwa mwezi chumba kimoja , je ?? kwa nini tusijirushe ???? Unamuomba Mungu atusaidie mara ngapi ?? tuko peponi tayari and we are looking gooood !! Mshikaji wacha wivu, wewe saidia kujenga madaraja huko. ni mimi Zebedayo msema kweli.
ReplyDeletekama kujirusha au vumbi tupu, miye mambo yangu mswano huku ughaibuni, wewe baki kupiga domo hapo bongo, dua la kuku........
ReplyDelete