Kutoka kulia ni Shabani Simba - Afisa Habari na Uhusiano BAKWATA makao Makuu, Sheikh Musa Kundecha Amir wa Baraza kuu la Jumiya na Taasisi za Kiislam Tanzania (BARAZA KUU) pale alikuwa akitoa tamko kama kaimu Mwenyekiti wa jopo la Viongozi wa jumuiya na taasisi zilizo hudhuria mkutano wa sensa Mjini Dodoma, Kondo Bungo Amir wa Jumuiya ya Wahadhiri Tanzania, Ustaadhi Omar Msinziya- Katibu wa Jumuiya ya Vijana BAKWATA Makao Makuu, Sadiki Suleiman - Mkurugenzi Mtendaji Jumuiya Wataalam Waislam Tanzania (TAMPRO)
www.abs.org.au.census
Kwenye tovuti zote hizo unaweza kupata habari juu ya sensa za makazi na watu kwa nchi za wenzetu wanafanya sensa ikiwa na kipengele cha dini kikiwepo. Watu watakuwa na rejea ya uhakika. Hata kama watu wengine watatoa taarifa zao taarifa za kuaminika zitatoka ktk ofisi ya serikali , hakutakuwa na ubabaishaji kama ilivyo sasa ambapo unaweza kua malalamiko zaidi hatimaye kuvunjika kwa amani.
Mfano unaotolewa na Serikali kuhusu Nigeria haujazingatia nchi nyingine ambazo zinafanya sensa hizi kwa Mafanikio kama UK, Australia, Canada, Uganda, nk
Ni Marekani tu ndio iliyoa kipengele hiki kwa sababu zake binafsi. Wanaotawala wachache hawataki wajulikane kuwa ni wachache.
Msimamo wa Waislam juu ya Sensa ya August 2012
1.Kipengele cha dini kiwepo ili kuondoa utata uliopo sasa kwa kupata taarifa rasmi za kiserikali kuliko kuacha kila mtu atoe za kwake, hali hii inaweza kuchochea kuvunjika kwa amani
2. Iundwe tume huru kusimamia zoezi la kuhesabu watu ili kila kundi liridhike
3. Serikali itunge sheria na kuisimamia kupiga marufuku utoji takwimu holela hasa katika shughulirasmi na za serikali jambo ambalo linaweza kuleta uvunjifu wa amani na utulivu kama walivyofanya TBC1 kwa kurusha taarifa zisizorasmi za sensa.
Kuendelea kupuuza malalamiko haya ni kukaribisha hisia za dharau, na kutosikilizwa kwa waislam ambako knaweza kuleta shida siku za usoni.
Tamko hili limesomwa na Sheikh Musa Kundecha kwa niaba ya Sheikh Mohamed Mtuliya (BAKWATA) ambaye ni Mwenyekiti wa Viongozi waliotoa Tamko.Viongozi hao ni wawakilishi wa Taasisi kubwa za kiislam zifuatazo;
1. BAKWATA
2. BARAZA KUU
3. SHIA ITHNAASHERI
4. JOPO LA MAULAMAA TANZANIA
5. HAIYATUL ULAMAA
6. JUMUIYA YA BOHORA
7. UMOJA WA WAHADHIRI TANZANIA
8. JUMUIYA YA WATAALAM WAISLAM TANZANIA
9. SUNNI JAMAAT
10.JUMUIYA YA ISMAILIYA TANZANIA




Kwanini wakiristo wanaogopa kuwekwa kipengele cha dini katika sensa?
ReplyDeleteMimi naomba kuelekezwa umuhimu wa kuweka kipengele cha dini katika sensa, je hii itasaidia nini katika kuleta maendeleo ya nchi yetu?
ReplyDeleteWasiwasi wangu mkubwa hii yaweza kuwa ni moja ya sababu zitakazoleta mpasuko na mtafaruku katika nchi yetu. Kuna haja gani ya kutaka kujua wakristo ni wangapi, waislam ni wangapi, hindu ni wangapi nk, kama siyo kutafuta namna ya kubaguana zaidi?
H.Kissiwa
Watanzania tuamue kuacha mijadala isiyotusaidia, wenzetu wanatuacha kimaendeleo sisi kazi yetu kubishana tu, leo linaanzishwa hili kesho hili na keshokutwa hili, badala ya kushughulika na umasikini wetu. Vipi Jamani? mliopo nchizilizoendelea tuone mwongozo, leteni uzoefu, andikeni ushauri, maana tuliopo hapa Tanzania tunaweza kuona kama tumefika kweli kumbe tunacheleweshana bila sababu. Mimi inanisikitisha sana, sasa hivi tumefika mahali kila mtanzania anapiga maneno, anapiga siasa, mwanaharakati, mpambanaji, mlalamikaji nk Nchi tutaijenga saa ngapi? Aaaah Jamani hebu tubadilike, tunajenga taifa la namna gani? Napendekeza tuachane na haya mambo yasiyo na tija, kila mtu afanye kazi, wanasiasa waliopo wanatosha, wengine tukalime, tuliopo ofisini tuhudumie watanzania na viongozi tuongozeni vizuri. TAIFA HILI LIJENGWE NA WENYE MOYO SIO WENYE HASIRA, Please muda unakwenda Huuu, Ohooooo!!!!!
ReplyDeleteWanao lalamika kubaguana kwa kuwepo na kipengele cha dini katika sensa mimi sielewi wana towa wapi hoja hii. Ubaguzi upo tayari Bongo bila hata ya hicho kipengele kuwepo. Weka kipengele cha dini katika Sensa kila mtu ajue kwa nini mnaogopa?
ReplyDeleteBongo kuna itikati za kutishana kila linapokuja jambo jipya. Nakumbuka mfumo wa vyama vingi ulipoanza wananchi tulitishiwa oh! vyama vya upinzani vitahatarisha amani, leo ni miaka imepita na watu wanaendelea kupiga kura bila matatizo.
Tufuate mdeli ya sensa ya Marekani ambapo dini haina nafasi ktk sensa.
ReplyDeleteKama viongozi wadini mbalimbali wanataka kujua idadi wa waumini wa dini zao, basi kazi hizo zifanywe na jumuia zao za kidini.
Mdau
umoja kwanza
Matatizo hayawezi kuja kwa kujua idadi ya watu wa dini fulani.Tatizo tulilonalo sasa ni kubwa, kuna taasisi nyingi zinajitolea idadi ya watu kulingana na dini ilhali wanajua serikali ya Tanzania haijahisabu kwa namba hivyo kwa miaka ya karibuni achilia mbali chini ya miaka ya 1974.Kwa mfano TBC1(chombo cha serikali hiki) kilitoa takwimu ya idadi ya watu kulingana na dini yao.Waislamu wakaja juu, walimwandikia barua Mkurugenzi wa TBC1 aeleze amepata wapi hizo data wakati serikali haijawahi kufanya sensa ya namna hiyo kwa siku za karibuni?Wakampa muda awajibu?Mkurugenzi wa TBC1 akajibu ni kweli serikali haijafanya sensa ya namna hiyo na TBC1 ilifanya makosa,akaomba msamaha. Kwa hiyo basi,mtazamo wangu sensa ifanyike kulingana na DINI.Na hata vitambulisho vya Taifa vitakuwa na taarifa ya dini ya mtu kwa sababu italeta shida kama hakuna kipengele cha dini kwenye taarifa ya mtu.Hatutakiwi kukimbia tatizo tunatakiwa kutatua tatizo.Sayansi na teknonolojia haijawa hivi ilivyo kwa siku moja,kwa kutatua matitizo mengi kila siku na wanasayansi.Kwa hiyo hata nchi yetu tukitaka tuendelee tunatakiwa kutatua tatizo moja hadi nyingine.Sioni sababu ya WAKRISTO kuogopa kuhisabu watu kulingana na dini, kuna tatizo gani.Mbona viongozi wao wadini wakati mwingine wanataja waislamu wapo kiasi gani,wakristo wapo kiasi gani,n.k.,wakati wanafahamu serikali haijahisabu kwa mtindo huo.Tusidanganyane,hizi ni ENZI ZA UWAZI NA UKWELI.Haina haja ya kuficha ficha.Nilivyoenda kusoma kozi ya uzamivu nchi fulani kwenye fomu ya kutaka bweni walitaka nijaze kipengele cha dini.Hii inawasaidia kuweka mazingira ambayo hayatamuuzi yule mtu.Mfano kama ni muislamu watahakikisha nguruwe,nk.k haviwi na huyo mtu.AMANI ITAPATIKANA KWA KUVUMILIANA NA KUJUA VIZURI DINI YA MTU MWINGINE.KILA DINI IHUBIRI KULINGANA NA VITABU VYAO VYA DINI VINAWAAMBIAJE.NA WATU WALIOKATIKA DINI NYINGINE WAFAHAMU KWAMBA KINACHOHUBIRIWA NI KILE KILICHOANDIKWA KATIKA VITABU VYAO.NA KAMA WANAUHAKIKA KWAMBA KINACHOHUBIRIWA KINATOKA KATIKA VITABU VYA DINI YA HAO WATU HAWANA HAJA YA KUWASHITAKI, HAPO PATAINGIA ZANA YA KUVUMILIANA KATI YA DINI NA DINI. MFANO WAISLAMU KWENYE KITABU CHAO KINASEMA WAZI KABISAA YESU (ISSA) NI MTUME NA SI MUNGU NA UKIJA KWA WAKRISTO WAO WANASEMA KWAMBA YESU NI MUNGU. KWA HIYO BASI HAPA ITAHITAJIKA KUVUMILIANA KWA KUWA VITABU VYAO VINASEMA HIVYO,HAINA HAJA YA KUNDI MOJA KUMSHITAKI MWINGINE MAHAKAMANI.KUTAFUTA UKWELI WA JAMBO NI KITU KINGINE. KWA HIYO BASI NIMALIZIE KWA KUSEMA KUWA TUNAHITAJI SENSA YENYE KIPENGELE CHA DINI.TUSIPOTEZE MUDA,TUACHE WOGA USIO NA MAANA.NCHI NYINGI WANA HICHO KIPENGELE HATA UTURUKI.FAIDA ZAKE NI NYINGI KULIKO HASARA.ANAYESEMA KWAMBA AMANI ITAVUNJIKA KWA KUJUA IDADI YA WATU INABIDI ATETEE HOJA YAKE,AWEKE BAYANA KABISAA ANAMAANISHA NINI NA ITAVUNJIKAGE AMANI????
ReplyDeleteH. Kissiwa
ReplyDeleteGooogle nchi yeyote uitakayo
- Go DEMOGRAPHICS
-Click RELIGION
-Utakuta percentage za dini zote
-Umuhimu wa kuweka kipengele cha dini kwenye sensa ni kupata accurate figure kwenye hiyo sehemu.
Kwa sasa taasisi mbali mbali zinajitolea takwimu kama wajuavyo wao, ziwe za serikali na watu binafsi. Nimenukuu baadhi ya vipengele kutoka gazeti la habari leo la mtandanoni la leo la tarehe 14/6/2012.
ReplyDeletehttp://www.habarileo.co.tz/index.php/wazo-langu/711-sakata-la-sensa-lishughulikiwe-kwa-busara
Ni hivi:
"... vyombo vilivyotoa takwimu hizo ni tovuti ya Wakatoliki inayoonesha kuwa mwaka 2008 Waislamu walikuwa asilimia 34, Wakristo asilimia 44 na Wapagani asilimia 22.
Aidha, akaitaja Televisheni ya Taifa (TBC) ambayo hivi karibuni iliripoti kuwa Waislamu ni asilimia 32, Wakristo asilimia 52 na Wapagani asilimia 16
wakati Idara ya Uhamiaji ikionesha kuwa mwaka 2010 Waislamu walikuwa asilimia 35, Wakristo asilimia 32 na Wapagani asilimia 33
Pamoja na hayo, alisema pia chapisho la Serikali la
Ramani ya Taifa linaonesha kuwa mwaka 2011 Waislamu walikuwa asilimia 35, Wakristo asilimia 45 na Wapagani asilimia 20."
Wanasemaga wenye macho hawaambiwi tazama. Sasa kama hali iko hivi KWANINI PASIWEPO SENSA ITAKAYOTOA UHALISIA WA IDADI YA WATU NA DINI ZAO.Maimamu wako sahihi kabisaaa, miye Mtanzania nawaunga mkono kwa asilimia mia moja(100%). Na hakuna kuhudhuria sensa kama serikali haitaki kuweka kipengele cha dini,manake naona kuna ubabaishaji.Hizi ni enzi za ukweli na uwazi.
"NAOMBA MICHUZI ADMINISTRATOR UNIWEKEE HII MANAKE NAONA WAKATI UNAFICHAGA COMMENTS ZINAZOTOAGA UKWELI WA MAMBO"
Kwa wale wanaotaka tufuate Marekani na kutokuwa na kipengele cha dini,
ReplyDeleteKwanza: Kwanini tufuate marekani? Kama tunapenda kufuatafuata tuu, jee kwanini tusifuate Uingereza ambapo wanacho kipengele cha dini kwenye sensa yao?
Pili: Kwanini wamarekani kwenye sensa yao wanataka kujua watu weusi ni wangapi, wazungu ni wangapi na latino ni wangapi?
Tatu: Jee changamoto zinazowakabili wamarekani ndizo hizo hizo zinazotukabili sisi? Kuna kosa gani kwa serikali kuwa na takwimu rasmi za watu wake na imani zao?
Nne: Kwa wale mnaosema kwamba kujua idadi ya waumini wa dini mbalimbali kutaleta mpasuko, jee hii itasababishaje mpasuko? Au mnaogopa kwamba walio wengi watakataa kuendelea kudhulumiwa na wachache?
Tano: Hivi unawezaje kuitumia nchi kama Nigeria kuwa ni mfano wa yatakayoweza kutokea Tanzania? Ni elimu gani hiyo kwa nyie "mliosoma" inayowawezesha kufananisha Tanzania na nchi ambayo watu wake wa makabila tofauti hawawezi kuwasiliana pasipo kutumia lugha ya kizungu?
Sita: Katika kukaa kwangu madarasani, nimejifunza kwamba binadamu wanaweza kubishana kwa kuwa na maoni tofauti, lakini huwezi kubishana na kweli iliyo thabiti, au "facts". Jee kwanini mnaogopa kujulikana kwa takwimu sahihi au "facts"? Au mnaogopa kwamba huu unaweza ukawa ndiyo mwanzo wa kukomesha dhuluma?
Kila taasisi ya dini inapaswa kujua ina waumini wangapi nchini, si madhumuni ya sensa ya makazi na watu kujua Waislam ni wangapi na Wakristo ni wangapi, maana ugawaji wa rasilimali na maendeleo ya makazi hayaangalii dini na itikadi za watu. Tuache kulalama kwa sababu viongozi wa dini mbalimbali walihusishwa katika mchakato wa sensa hii tangu awali, kuleta vipingamizi wakati wa mwisho unapandikiza hofu na pia kutaka kulifanya zoezi hili muhimu kuwa si la maana tena....
ReplyDeleteTunaogopa nini kuweka kipengele cha dini kwenye sensa! Mnaopinga hili jambo mnaona ni afadhali kila mtu/jumuia ijitolee takwimu zake kama inavyoona yenyewe? Kwanini tusiwe na takwimu za uhakika ili zitumike popote zitakapohitajika. Angalia sasa matokeo yake TBC wanatoa takwimu za uongo halafu wanaomba radhi, kwanini tusiepukane na hili!!!
ReplyDeletehuwa tukitoa malalamishi kwamba mnatubagua, tuko wengi lakini underepresented.
ReplyDeletehutujibu, lete ushahidi, data, siyo lawama.
sasa wewe mkusanya data, hutuomba data kila siku, twakwambia kusanya hutaki.
tupe ruhusa tukusanye wenyewe nchi nzima, hutaki.
Ukweli ni kuwa Mtikila ndiye aliyeanzisha upuuzi huu, pale alipodai mnamo 1993 kuwa eti Waislamu ni 35% tu ya Watanzania na jamaa mwingine anaitwa Kimilikwo akadai kuwa eti Waislamu ni 30% ya Watanzania. Percentage hizo zimekuwa zikinukiuliwa katika mtandao kama kwamba zina msingi wowote wa kisayansi. Wiki jana tu katika blogspot ya mwenyekiti Mjengwa kuna jamaa anaitwa Matinyi ametoa website 2 zinazodai eti Waislamu ni around 30% ya Watanzania bila kusema sensa uchwara hiyo ilifanywa lini na nani aliifanya. Suluhisho ni moja tu: Katika sensa inayokuja swali la dini liulizwe ili tumalize ubishi huu once and for all!
ReplyDeleteSi TBC tu. Nilipokuwa Norway niliona kabrasha ilyotayarishwa na Norwegian Council of Churches ikisema kuwa 29-33% ya Watanzania ni Waislamu. Mimi nilmwambia mwenyeji wangu kuwa that's utter rubbish kwa kuwa tangu baada ya uhuru hakujawahi kuwa na sensa iliyojumuisha dini Tanzania. Sensa ya kwanza baada ya uhuru ilifanyika 1967. Ukweli ukidhihiri.................
ReplyDeletemimi katika hili ni juha wa kutupwa ebu mtusaidie:-
ReplyDeletekwa wanaoafiki
1. faida 5 za kuweka kipengele cha dini kwenye sensa
2. hasara 5 za kutoweka kipengele cha dini kwenye sensa
kwa wasio afiki
1. faida 5 za kutoweka kipengele cha dini kwenye sensa
2. hatari 5 za kuweka kipengele cha dini kwenye sensa
Hivi bila data utasemaje kama upo au haupo ubaguzi? Hivi kama kuna ubaguzi hamuoni utalelewa na ombwe la data? hivi mnaogopa nini kuwepo data?
ReplyDeletedata ikusanywe ili wataalamu watatue matatizo yetu yatokanayo na dini ni historia mbaya za kidini nchini.
ACHENI KUHESABIWA TUU.
ReplyDeleteKwani baada ya kuhesabu wakristo na wapagani na kupata idadi ya, say, mil 25, tutasema hivi:
1. sera zetu za kupunguza idaidi zmefanikiwa, toka mil 35 mpaka 25. Tunatajia kupungua kwa milioni 10 kila miaka 10.
2. Sera za uzazi wa mpango zimefanikiwa,
3. ukimwi na malaria vimetuangamiza,
4. taifa masikini linakufa kwa njaa, tupeni misaada.
5. watu wengi wamehama nchi kutafuta masiha bora.
6. watu wengi wametwanyika kwenye soko la EA ili kupata ajira
7. yapo majibu mengi msijali.....
NO, wakigoma tutapata data mbaya kwa gharama kubwa, na mipango yoote ya mbele itakuwa bomu.
ReplyDeleteViongozi msikalie misimamo isiyowasaidia, data mbaya itaharibu kila kitu.
Mtambuwe "ukifungua dirisha kwa ajili ya hewa pia ukubali vumbi, mbu, nzi, harufu, nk. viingie" la sivyo hata hewa hutapata.
Mtambuwe Viongozi
ReplyDelete"ukifungua dirisha kwa ajili ya hewa pia ukubali vumbi, mbu, nzi, harufu, mwanga, baridi, joto,nk. viingie" la sivyo hata hewa hutapata.
Je ukose hewa na mwanga kwa ajili ya kukwepa vumbi, joto, baridi, n.k.?
anoy wa Thu Jun 14, 08:16:00 AM 2012
ReplyDeletekila taasisi inatakiwa kujua idadi ya waumini wake sawa!lakini unaonaje taasisi nyengine inapowasemea watu wa dini nyingine wako idadi kadhaa dhidi yao huoni huko ni kupotosha ummah,kama jambo hilo halina manufaa ktk jamii kwa nini wakristo wanaibuka na takwimu za uongo kila mara na huku wakizinasibisha na serikali kuupotosha umma wa watanzania?? huo ni unafiki wa hali ya juu. Zamani mliwadanganya watanzania kwa kua hawakua wamekwenda shule na nyie wachache mlioendelezwa na kanisa na kupitia taasisi zilizo nyingi zilizoasisiwa na mkoloni kupitia kodi za wananchi...Sio sasa watu wanaelewa haki zao na kama kuna upotoshaji wa makusudi ni lazima usahihishwe ndipo maisha yataendelea kama kawaida,,,kinyume chake hatuwezi kushirikiana wala kushiriki katika sensa na jambo lolote la kitaifa ikiwa mnalipotosha kwa makusudi na huko ndiko kutapelekea jamii fulani kujitenga hence nchi kugawanyika.
Bishaneni mpaka mtoane macho lakini mwisho wa yote mfike mahala mkubaliane lipi ni lipi.
ReplyDeleteKama wanaotaka watakuwa wengi wapewe haki yao na kama wasiotaka watakuwa wengi nao wapewe haki vile.
Lakini lililo la msingi tukumbuke tuna safari ndefu sana kuendelea sasa labda haya tunayojadili sasa yatatusaidia hapo baadae ili tutakapokubaliana na safari yetu kuanza twende kwa kasi zaidi.
Wote tukumbuke kwamba safari yetu ni moja na lazima twende wote! na kusafiri lazima tusafiri.
Basi serikali yetu inayodai ni sikivu kwa maoni ya watu wake itusaidie wote kusudi kila mmoja aridhike kwamba katendewa haki kusudi safari yetu twende salama badala ya kuendelea kubishana.
Tutachelewa jamani........
siku hizi statistics ni kila kitu. Dini ni moja kati ya vitu muhimu kujulikana, na in most cases itasaidia kuleta maendeleo. Kwa mfano; siku hizi elimu ni dili kubwa tu, kupitia sensa, naweza kujenga shule na kuiita ya ki krist au ya kiislam ili kuvutia wakazi wa eneo bila hata ya kubagua dini nyengine. Pia naweza kujua kiti moto ita lipa au nita anzisha valangati na wakazi. Huu ni mfano mdogo tu kujumlisha dini kwenye sensa. Naamini serikali haitoi ruzuku kwa dini yenye watu wengi kama ilivyo kwa vyama vya siasa vyenye wabunge wengi.
ReplyDeleteHEBU TUWEKENI MIFANO RAHISI YAKIMAENDELEO.
Haina haja ya kulazimisha sensa. kama hawataki sensa na kitambulisho cha Taifa wasusie pia. Serikali itapata tuu hesabu ya watu kutoka kwenye vitambulisho vya Taifa.Hakuna haja ya kufanya kitu kilekile mara mbili. Ni bora kutumia pesa za sensa kwa mambo mengine ya kimaendeleo. Dini dini.. watu wenyewe hata kuishi kulingana na dini zinavyotaka imekuwa ngumu mnabishania visivyo na Tija. Eti fulani katoa idadi isiyo rasmi, hayo ni maoni yake... Muulize katoa wapi? Ina maana leo akisimama mjinga mmoja akasema kitu cha uwongo na ukajua ni uwongo bado tuu utaendelea kubishana naye? Inasikitisha sana!!
ReplyDeleteTatizo lingine ni jazba , naona watu wana jazba sana wakihisi kuwa wanaonewa kutokana na idadi ndio maana wanashikilia kutaka hicho kipengele
Mimi. Hivi miaka yote hii mbona hakuna aliyedai jambo hilo? Kwani nani anaweza kuniambia raslimari za Taifa hivi sasa zinagawanywaje? Au kuna mgao wa siri ambao wengine hatuujui? huo mgao Kwa ratio ipi? Nani anagawa? Kila mtu anachuma kwa jasho lake, sio dini wala nini. Mimi naona ni ndoto za alinacha tuu zinawasumbua .. inferiority complex.
Mimi.