Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia) akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing wakati wa hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya  China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya kilimo nchini.
Viongozi mbalimbali kutoka ubalozi wa China na seraikali ya Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya kuanza  hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya  China  na Tanzania kwenye miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania.Kutoka kushoto nyuma ni balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule.
Baadhi ya mashuhuda wa miradi mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ukiwemo ujenzi wa  reli ya Uhuru (TAZARA) walioalikwa kwenye hafla hiyo  Bw. Abdul Haji (kulia) na mama Roza Kangoma (kulia) ambaye ni mama wa balozi wa Zambia nchini Tanzania pia aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha mafunzo cha TAZARA.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia) akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa na ubalozi wa China nchini Tanzania kuhusu  mikakati ya serikali ya kuboresha  kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao wakati wa hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania katika miradi mbalimbali ya Kilimo inayofanyika Tanzania.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo katika ubalozi wa China nchini Tanzania wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
Raia kutoka mataifa mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya kusherehekea  mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kutoka nchini China katika miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania wakijipatia nakala mbalimbali za machapisho kuhusu shughuli za kilimo, siasa, Utamaduni, Teknolojia na masuala ya kijamii.Picha na Aron Msigwa-MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...