Home
Unlabelled
Ujenzi barabara ya mabasi yaendayo kasi waendelea jijini Dar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hivi hayo mabasi yatakuwa yanakimbia spidi ngapi?au ndo jina tu?
ReplyDeletedalili zinaonekana ujenzi utakuwa wa kusababisha kuzidisha uchafu na uchafuaji mazingira
ReplyDeletehiyo barabara ya speed bus ipo katikati hapo labda wataweka ukuta kutenganisha hizo barabara mbili huo ukuta unaweza kusababisha ajali mbaya sana
ujenzi wa kimasikini wenye plani ya kimasikini utatuharibia mazingira na muonekano mbaya wa maeneo ya nchi.
Is this true story? Mabasi yaendayo kasi Tz wakati yanayoenda taratibu yanauwa watanzania kila kukicha na kufanya wajane na yatima kuongezeka kila iitwapo leo? Watazuieje yasiue?
ReplyDeletehaya haya !! kumbe ya Mungu mengi, na sisi iko siku tutafika !! mliokimbia nchi ,sasa udenda unawatoka, bongo bar hazifungwi, nyama choma kila kona, ukiwa na dola moja ,unakula mpaka unashiba, pressure ya maisha hakuna !!! na maendeleo kila siku ndo kama hivi. Jamani bongo ni peponi. Zebedayo,bongo forever.
ReplyDeletendugu yangu Zebedayo umeshawahi kwenda nje ya nchi?i mean Ulaya au america?.kama bado basi bora ukae kimya kaka yangu. Me nilikuwa kama wewe nikijua bongo ni peponi lakini nilipopata ka-trip ka office kwenda nje nilikuja kugundua sisi kweli ni dunia ya tatu na tu maskni sana. I wish wa-tz wenzangu angalau hata nusu wakapata nafasi ya kwenda angalau siku mbili nje&kujionea then tutafunguka akili na kuamua kuijenga nchi yetu ili baadae iwe kama huko duniani.
ReplyDeletedola moja unakula mpakaunashiba? Uko Bongo pande zipi nihamie mdau au unaongea na masaburi?
ReplyDeleteWatanzania tumezidi kulalamika. Mwalalamikia foleni,mnawekewa mabasi kasi mnalalamika oh uchafu,oh ajali sasa mwataka nini? Wewe wa uchafu sijui umeitoa wapi dhana hiyo,kwani umeiona plan yake ikikamilika inakuwaje? Kwa nini tusisubiri ikamilike ndo tuanze kukosoa? ovyo!
ReplyDeleteNafikiri sio speed bus this is free flow bus au mabasi yasiyo na foleni ndo manake no trafic jam
ReplyDeleteDu, kweli elimu bado inatakiwa, na wahusika wa huu mradi wana kazi ya kuelimisha umma kuhusu hili neno, 'MABASI YAENDAYO KASI" naona bora waanza kusema mabasi ya haraka, Wadau wote wa globu ya jamii, wanavyosema mabasi yaendayo kasi(BUS RAPID TRANSIT) kifupi BRT, ya jiji letu tukufu yataitwa DART=DAR ES SALAAM RAPID TRANSIT. hilo neneo kasi wadau wengi hudhani ni speed ya basi inakua kasi, la hasha, ina maanisha mabasi yatakua ya harka kwa kuwa yana njia zao yenyewe ambazo hazitaingiliwa na magari mengine, hivyo hakuna foleni na yatasimama tu kwenye kituo na mahali penye taa, kuhusu speed ya kasi na kuogopa yatasababisha ajali haina uhusiano kabisa, ni mabasi ya kaiwada ya abiria mijini na sidhani hata speed zao zitakua zaidi ya 60km/h, jitahidi kutumia mtando vizuri , nendeni youtube seach BRT, na utajifunza vizuri nini maana ya mabasi yaendayo kasi, na mdau hapo aliyesema ujenzi wa kimasikini unakosea kabisa, mradii huu sio wa kimasikini, ni world class na pene linatoka world bank, usisahau kampuni inayojenga mradi huu pia ni kampuni matata ya kimataifa ya ujerumani, hivyo msipende kujump kweny conlusion mapema hivi, mradi wa mabasi yaendayo HARAKA jijini dar es salaam unafuat ule wa TRANSMILENIO wa bogot Colombia na youtube kuna video kibao zikielezea jinsi maradi unavyofanya kasi na jisi mabasi yalivyo, kwa kua mradi wa dar unatkua copy ya ule kila kitu, mkuu iss mithupu kwa nini usiapload zile video hapa kwenye globu ya jamii ili wadau zaidi wawenze kuosha macho? lasivyo watu watapotoshana kuhusu speed ya mabasi haya na wanaweza kuanza kuandamana na kusababisaha ucheleweshaji wa mradi huu maalumu tunaousubiri kwa hamu, imagini unatoka kimara hadi ferry dakina 3 tu, kuliko sasa hivi masaa kadhaa utafikiri unatoka mkoani, wadau tujitahidi kuchunguza kitu kama na kama huna uhakika nacho uliza au google, kama kawa mithupu fanya mambo , asante sana na libeneke oyeee
ReplyDeleteSiyo yaendayo kasi ni yaendayoyo HARAKA. Kwanini hamsikilizagi vipindi vinavyoelimisha??
ReplyDeleteInaonekana hizo basi zitakuwa zinapita katikati tu. Unafikiri watu wa kawaida watakubali kusimama kwenye foleni wakati kati peupe? Ni project ya pesa nyingi sana na inaonekana kama haitolipa kabisa. Wangeweka tram ingekuwa safi maana inachukua watu wengi zaidi ya basi na hai-ermitt CO2 nyingi maana ni za umeme. Tunachafua mazingira na mandhari ya mji na hizo CO2 emissions kama kila mtu anataka aende mjini na usafiri wake. Serikali ingepiga marufuku magari kuingia mjini, au kuweka vibali maalumu kama kuna dharura, ingepunguza sana msongamano na kulinda mazingira.
ReplyDeleteACHA USHAMBA WEWE.....TATIZO HUJATEMBEA, WE UNASHANGAA UKUTA KUJENGWA KATI KATI YA BARA BARA.....MBONA FREEWAY ZA NCHI KIBAO HUWA ZINAKUWA NA UKUTA
ReplyDeletehayo mabasi sidhani kama ni kweli yatakuwa yanaenda kasi.Ila tu ni jina hilo!
ReplyDeleteMimi naona barabara itazidi kuwa pana sana na ni hatari kwa mvukaji kwa miguu,badala ya kuzuia ajali sasa mnatengeneza ajali..Kwa ushauri bora mimi naona mjenge daraja juu au underground kwa watu kuvuka kwa urahisi,ma sivyo itakuwa ni hajali za kila wakati
Na ushauri mwingine hayo mambasi yanatakiwa yawe ya serikali,,maana watu binafsi itakuwa ni kukimbiza kwa kutaka faida
Ahlam,,London
wabongo kulalamika hakuishi hata ufanye nini mara barabara itaua mara ukuta mdogo barabara yenyewe kwanza ndo inachimbuliwa
ReplyDeleteWewe Zebedayo acha ujinga. Bongo kuna nini kilichoongezeka? Kwa vile hujaenda nchi yoyote ya nje ndo maana unaita uharibifu wa mazingira kuwa ni maendeleo. Mlio nje bakini hukohuko bongo hakukaliki. Na sasa hivi watu walivyo na roho mbya na wivu ndo mtachoka mkileta vijigari vyenu hapa. Mtu huna uhuru wa kutoa maona hasa kama unakosoa serikali. Maofisini customer care ni very poor na hakuna anayewajibishwa. Watu wa dini nao wanaanza kutishia amani za dini zingine. Kwa kweli bongo nilipapenda lakini kwa haya yanayojitokeza nimeanza kupachukia. Hapafai kabisa.
ReplyDeleteMabasi yaendayo kasi!
ReplyDeleteHivi kwa miundo mbinu yetu ya njia za kukata kata itawezekana vipi mfano basi litoke hukoo Manzese halafu lisikate barabara ingine hadi Posta?
Je kwa mpangilio huo wa kukata barabara itakuwa mwendo kasi au mwendo pole ili kukata barabara zingine, kupisha mabaiskeli ya matairi matatu (Guta) na kupisha waendao kwa miguu?
Mbona naona miujiza?
Mabasi yaendayo kasi Tanzania itakuwa ni maajabu ya Mussa!
ReplyDeleteTuwaite Guinnes waje waandike rekodi kama itafanikiwa mpango huu!
Je itawezekana chini ya jua ndani ya Bongo?
Bus Rapid Transit itasaidia kupunguza msongamanao wa magari barabarani. Kama nchi kama Columbia imeweza sioni kama itakuwa tatizo kwa Tanzania. Uzuri wa Bus Rapid Transit ni kwamba njia yake inaweza kuibadilishwa kuwa ya light rail kama msongamano wa magari ukiongezeka.
ReplyDeleteMichu, shikamoo,najua utakuwa unanizidi kidogo umri, lakini aisee ,aliyekupa ujanja huu wa kutuanzishia blogi hii takatifu, nakuombea kila aina ya dua. Hii mada ya barabara imenifurahisha sana, na kweli kuna wabongo sasa hivi kila sehemu ya dunia tunakutana humu na inapendeza sana tena sana kusoma maoni mbali mbali. Wabongo tunazidi kukomaa, hata wale ambao bado hawajakomaa kikutoa maoni,tusiwanyime nafasi za kuchangia, unajua tena kwenye msafara wa mamba, kenge,vyura,konokono hawakosi. Aliyekataa kwamba bongo ukiwa na dola moja unakula wali maharage na unashiba !!! basi huyu ndo wale wale wala chips,au aliyekataa kwamba bongo siku hizi ni peponi, basi ndiyo wale wale wanaokimbilia nje bila hata kujiandaa au kuulizia kwanza.kuna msemo usemao, its always green on the other side, na aliyesema kwamba alienda nje na kaona huko eti kumejengeka ile mbaya na eti sisi tuko nyuma na masikini wa kutupwa !!! pole sana kaka, wewe nawe ndo wale wale wenye kutamani vya mwenzio, na cha ajabu,huenda ulisumbuliwa na macho ya ugenini, laiti kama ungelijua kwamba kuna wazawa wa hiyo nchi uliyokwenda , wanatamani waje kuishi Tanzania au tayari wako hapa, aliyekupa hiyo nauli kwenda huko !!! , siku nyingine ,naomba aipeleke kwenye kambi ya watoto yatima . Zebedayo msema kweli.
ReplyDeleteWabongo hatuna jema wala baya! Yaan daily ni kuishi tu negative side...while maendeleo huja hatua kw hatua so maandaliz ya kujenga barabara ya mabus hyo ni hatu ya kimaendeleo.mtaka kilaskiu tupande mingalangala? Hachaane hzo ,lazma tuishi kwny positive side
ReplyDelete