Mkurugenzi Mtendaji wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Bw. Walter Bugoya akitoa neno wakati wa uzinduzi wa kitabu cha 'FURAHA HUJA ASUBUHI' (JOY COMES IN THE MORNING) kilichoandikwa na Hopolang Phororo kinachozungumzia Mateso na manyanyaso ya wasichana wadogo wakati wa malezi yao na haki ya msingi ya jinsia ya kike katika jamii.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Fatma Mrisho akitoa nasaha zake wakati uzinduzi rasmi wa kitabu hicho jijini Dar es Salaam. Alisema 66% ya wanawake na 20% ya wanaume nchini wameshawahi kukutwa na majanga ya unyanyasaji wa Kijinsia katika maelzi yao ambapo kwa sasa Dar es Salaam na Mbeya zinaongoza.
Mtunzi wa Kitabu cha 'JOY COMES IN THE MORNING' Bi. Hopolang Phororo akielezea simulizi ya kweli iliyomkuta kama mwathirika wa unyanyasaji wa Kijinsia wakati wa usichana wake na moyo, uvumilivu aliokuwa nao wa kuweka uzoefu huo katika maadishi ili jamii ijifunze na madhara ya unyanyasaji wa Kijinsia unaokua kwa kasi nchini Tanzania.
Mmoja wa washiriki wa uzinduzi huo akitoa neno la shukrani wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Hopolang Phororo na haki za msingi za wanawake wanaokutwa na matatizo ya unyanyasaji wa Kijinsia Tanzania.
Ningependa kununua hiki kitabu je ni duka gani la vitabu hapa mjini Dar naweza kukipata.
ReplyDeletemisupu mbona hujatuambiye ni bei gani hichi kitabu kinaonekana ni kizuri sana na wapi kinapatikana
ReplyDeletemdau u.s.a