Baadhi ya wanachama wa klabu ya wafanyabiashara wateja wa NMB wakifuatilia kwa makini mafunzo ya utafutaji masokob yaliyokuwa yakitolewa jana.
Meneja wa NMB kanda ya kaskazini,Vicky Bishubo akifuatiwa na Mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB,Adam Shayo( kulia) j ,wakijumuika kumsikiliza kwa makini mtoa (hayupo pichani)katika semina ya siku moja kwa klabu ya wafanyabiashara wa NMB wa mkoa wa Arusha.
 Meneja wa NMB kanda ya kaskazini ,Vicky Bishubo wa pili kutoka kushoto akifuatilia kwa makini mafunzo ya ujasiriamali yaliyokuwa yakitolewa kwa klabu ya wafanyabaishara wa NMB ,katika hotel ya Golden Rose jijini Arusha ( picha na Woinde shizza,arusha).
 =======  ======  ========  ==========

Na Woinde shizza,arusha

BENKI ya NMB kanda ya kaskazini imeanza  kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa wateja wake waliopo kwenye klabu ya wafanyanyabiashara  wa  NMB katika mikoa ya kanda ya kaskazini yanayolenga kuwajengea uwezo namna ya kutafuta masoko ili kuboresha biashara zao.

Meneja wa NMB kanda ya kaskazini , Vicky Bishubo aliyasema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa klabu ya wafanyabiashara wa NMB ,150 kutoka mkoa wa Arusha.

Alisema kuwa, mafunzo hayo yamekuwa yakiwasaidia kupata mbinu za kibiashara na fedha na kupanua uwezo katika utafutaji wa masoko na hivyo kuwawezesha kumudu urejeshaji  wa mikopo kwa wakati  pindi wanapokopa .

Bishubo alifafanua kuwa mafunzo hayo ,yamekuwa yakitolewa kila mwaka , yamesaidia kuwaunganisha wafanyabiashara na benki katika kupata mikopo na kuirejesha kwa wakati.

Aidha alisema mafunzo hayo yatatolewa pia kwa vilabu vya wateja wa NMB waliopo kwenye mikoa ya Kilimanjaro na Tanga wiki hii,ambapo vilabu vya benki hiyo kanda ya kaskazini vinawanachama zaidia 450 ambao wamekuwa wakinufaika na mafunzo hayo kila mwaka.

Naye mwenyekiti wa klabu ya wafanyabiashara wa NMB ,Adamu Shayo alisema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia sana kuwajengea uwezo wa kibiashara kupanua wigo wa biashara zao ukizingatia nchi ya Tanzania sio kisiwa.

Alisema biashara zao zimekuwa zikiingiliana  na wenzao kote ulimwenguni katika kutafuta masoko ya ndani na nje,hivyo mafunzo kama hayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa kuwajengea uwezo wa kutafuta masoko.

Alisema kuwa mafunzo haya yamekuja wakati mwafaka kwa sababu mipaka ya Nchi za Afrika mashariki inafunguliwa na utandawazi unaenea kwa kasi na itasaidia kufaidika na soko la pamoja la jumuiya ya Afrika masharika.

Shayo ambaye ni mmiliki wa chuo cha ualimu Sila(Sila Teachers College) chenye namba ya usajili CU 115  kinachotoa cheti cha grade A ya ualimu na ajira moja kwa moja ndani ya serikali ,alisema ameweza kunufanika na mikopo ya benki ya NMB kupitia klabu ya wafanyabiashara na kuweza  kujenga chuo hicho chenye kiwango cha kimataifa.

Mafunzo hayo yateendelea kwenye mikoa ya Kilimanjaro ,Manyara na Tanga a,mbapo kwa kupitia vilabu vya wafanyabaishara,wateja wa NMB watapata fursa ya kupata mafunzo hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...