Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Kinondoni, Bw. Idd Azzan atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wanafunzi waliomaliza shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim (Reunion) zitakazofanyika Jumamosi Juni 30.
Mwenyekiti wa Reunion Bi. Mambo Tambaza alisema katika sherehe hizo ambazo zitahudhuriwa na wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kutoka ianzishwe mwaka 1966, walimu waliowahi kufundisha shule hiyo na wanafunzi wanasoma watahudhuria.
Makamu Mwenyekiti wa Reunion, Bw. Aboubakar Liongo alisema maandalizi ya sherehe hiyo yamekamilika na sherehe hiyo itaanza saa 5 asubuhi kwenye hoteli ya Cine Club iliyopo Kawe, Dar es Salaam.
Alitoa wito kwa wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kujitokeza ili kufahamiana na kuangalia uwezekano wa kuisaidia shule hiyo.
"Tumetoa taarifa kwa wanafunzi wote kwa njia ya mtandao na ujumbe mfupi wa simu za mkononi, ni matumaini yetu kuwa wengi watahudhuria" alisema Bw. Liongo.
Katika sherehe hizo mkuu wa shule hiyo na wanafunzi wanaosoma wataeleza hali ya kitaaluma katika shule hiyo na msaada wanaohitaji.


Shule imehitimu mamia kwa maelfu tokea mwaka 1966 hadi mwaka jana!.
ReplyDeleteTUPIGE HESABU:
IDADI YA MIAKA TOKEA HAPO NI 46
KILA MWAKA IDADI YA WASTANI WANAONALIZA 560 HIVI KUTEGEMEA NA MWAKA KWA KUWA KUTOKEA MWAKA 1985 SHULE ILIANZA UTARATIBU WA MADARASA YA SHULE YA MCHANA AFTERNOON.
1.KUTOKEA 1966-1984 (MKONDO MMOJA)
WA ASUBUHI:
MKONDO WA ASUBUHI NI WANAFUNZI 280
IDADI YA MIAKA 18
HESABU 18X 280= 5,040
2.KUTOKEA 1985-2011 (MIKONDO MIWILI) ASUBUHI NA MCHANA
ASUBUHI NA MCHANA 280 X2 =560
IDADI YA MIAKA 26
HESABU 26 X 560=14,560
SASA KUTOKEA 1966 HADI 1984 NA KUJUMLISHA 1985 HADI 2011 INA MAANA WAMEHITIMU 14,560+5,040=19,600
TUKISEMA KUACHA WALIOTANGULIA MBELE ZA HAKI IDADI YA JUMLA YA WAHITIMU NI 19,600 SASA JE IKITOKEA MFANO WAJE NUSU YA IDADI NI 9,800 JE WATATOSHA CINE CLUB?
HIO SI NIKUWA ILIBIDI SHUGHULI HII IFANYIKIE UWANJA WA TAIFA?
TETE TE TE! KINONDONI MUSLIM!! NI TANZANIA NZIMA,,
ReplyDeleteWALIOTANGULIA MBELE YA HAKI MOLA AWAREHEMU
NI KWELI INAHITAJIKA UWANJA WA TAIFA.NA WENGI WAKO NJE YA NCHI,,,
MIMI MOJA WAPO
AHLAM,,UK
kabla ya kwenda Azania kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na sita nilisoma kinondoni muslim kwa kweli naipenda sana shule ile na kila nikitembelea inanipatia memory moja ambayo sitoisahau labda kwa kuwa ndio niliyoijunzia mambo mengi yanaponisaidia maishani.pamoja na kusoma ughaibuni lakini still kinondoni ado ina nafasi kubwa sana ndani ya ubongo wangu i wish ningepata nafas ya kuonana na wanafunzi wenzangu wa enzi hizo za mwanzoni wamiaka ya 1990's. kwa wale mtakaobahatika kuhudhuria please enjoy it to the fullest on our behalf.
ReplyDeleteMngetupa muda na cc tuliokuwa mbali kwani tulishawahi kuulizana kufanya jambo kama hilo in the future lakini wenzetu mmewahi, anyway kama ikiwezakana mfanye nyingine sometimes December ili na waliombali nao waweze kufika kwani kama ujuavyo dreams za waliowengi ilikuwa kwenda majuu kama sikosei. Mdau Adam Uk
ReplyDeleteBandugu zangu wana alumni wa kimbwelu kila la kheri kwenye sherehe hizi...tafadhali mtuhabarishe nasi tulio mbali mambo ya kuchangia..salaam kwa mr.sharif, oya, mruma na wengineo...niliipenda geography kutokana na mafundisho ya mr.peter
ReplyDeleteWasalaam, kachala 93-96 o-level
One luv
Ni shughli pevu kabisa nipo Jijini Dar lakini mambo yamenikamata sana leo.
ReplyDeleteNapendekeza tuandae Permanent Portal kama ALUMNI ASSOCIATION tunaweza kuomba msaada wa mwanzo wa kuwasilina na kuandikishana kupitia kwa Ankal Michuzi hapa mwana Mtandao mweneztu wa Kinondoni!!!
USAJILI UWE NA VIGEZO HIVI:
1.JINA KAMILI LA MTU
2.MIAKA ALIYOSOMA KINONDONI
3.KUFIKIKA KWAKE KIMAWASILIANO YEYE MUHUSIKA ATACHAGUA KAMA ATATUMIA E-MAIL, FACEBOOK AU NYIA YEYOTE ANAYORIDHIA YEYE.
4.ITASAIDIA KWA RIDHAA YAKE AKITUHABARISHA NI WAPI ALIKO NCHI, INATOSHA.
5.ANAWEZA KUTUGUSIA KAMA MAEONANA NA WANA KINONDONI WENGINE ENEO ALILOPO.
MIMI, mwenzenu Mwana Kinondoni.
Class of 1987-1990
Form Four-D
Afternoon
Mohamed M.
E-mail:hahemed@AOL.COM
La ziada naongezea,
ReplyDeleteZipatikane pia na namba za kusajiliwa
Mohamed M.
Class of 1987-1990
Form Four-D
Afternoon
E-mail:raishop@AOL.COM
Duhhh Ankal !
ReplyDeleteKwa idadi aliyotoa Mdau wa kwanza ya wahitimu 19,600 Kinondoni Secondary hivi haitoshi tukaomba Uwakilishi Bungeni na sisi?
Hebu muulize hilo Kiongozi Mkuu!