KAMATI ya Redd's Miss Tanzania imetembelea kambi ya Miss Dar Intercollege iliyopo kwenye hoteli ya The Grand Villa, Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwafunda.

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika ijumaa ya kesho katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na chuo cha Usmiamizi wa Fedha (IFM).

Akizungumza na warembo hao, mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye aliwataka warembo hao kufuata miongozi na kanuni za shindano hilo ikiwemo kuwa na nidhamu.

Alisema urembo si sura na umbo zuri bali unahusisha pia nidhamu katika jamii hivyo amewataka warembo hao kuzingatia hayo.

"Nafahamu ninyi ni wasomi wazuri hivyo mmeyapokea vema mafunzo tuliyowapa...hatutarajii kusikia mmoja wenu anachafua hali ya hewa katika siku za usoni na mambo ya skendo skendo,"Alisema Makoye.

Dina alisema shindano hilo litapambwa na msanii wa uziki wa kizazi kipya nchini Nasib Addul ‘Diamond’ sambamba na bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.


“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.

Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.

Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.

Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, dina ismail (zamani Mamapipiro), Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2012

    Mh! yaani hao wanaume wanawafunda nn hao wasichana jamani, au ndo kufundwa kule?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2012

    Pole sana Bw. Moh'd au Mohamed!
    Lakini jamani haya matatizo mengine tunajitakia wenyewe! Jina lako ni Mohamed, mtaani kwenu enzi hizo ukajulikana kama Moh'd basi na wewe ukakubali na kujiandikisha hadi Ulaya kama Moh'd hivyo hivyo! Sijui uliogopa kujumuishwa kwenye kundi la Magaidi? Sasa leo unashangaa kuona Nyumbani wanakuita na kukuandika kwenye Pass-port yako kwa jina la ukweli (Mohamed)! Aaah,ndugu yangu, hapo sas usimlaumu mtu ye yote!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 22, 2012

    mara nyingi naona hao wadada wanafundwa na wanaume au wakiwa mazoezini nahao jamaa unawakuta nadhani kuna jambo la kutazama kwani haya mashindano ni ya wanawake sasa nadhani hata kuwafunda ingekuwa vizuri kina dada wakafanya hiyo shughuli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...