Mkurugenzi wa kampuni ya LINO Agency ambao ni waandaaji wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Hashim Lundenga (katikati) akizungumza na warembo watakaoshiriki kinyang'anyiro cha kumsaka Redd's Miss Chang'ombe 2012 (hawapo pichani) wakati kamati ya Miss Tanzania ilipotembelea kambi hiyo kwa lengo la kuwafunda warembo hao.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamti ya Miss Tanzania,Bosco Majaliwa "Mshua" na Kulia ni Mratibu wa Redd's Miss Temeke,Ben Kisaka.
Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye akisisitiza jambo kwa warembo hao wakati walipoitembelea Kambi hiyo ya Redd's Miss Chang'ombe 2012 kwa lengo la kuwafunda warembo hao.
Mratibu wa Mashindano ya Redd's Miss Chang'ombe 2012,Tom Chilala akiutambulisha uongozi wa Miss Tanzania kwa warembo wa kitongoji hicho wanaotaraji kuingia dimbani juni 9,2012 katika ukumbi wa kisasa uliopo Quality Centre,pugu road jijini Dar es Salaam.
Warembo wakifanya mazoezi ya kucheza ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya shoo yao watakayoitoa siku hiyo ya shindano.
Picha ya pamoja ya warembo hao.
why they don't wear shoes on the top photo? have them in sneakers or sock during practice, its decent and not fancy, please and thank you!
ReplyDeleteWarembo WAFUNDWA! Wanfundaji wenyewe ndo hao kina baba?! Si mpaka wafundike basi. Kila la kheri any way. Next time wekeni maKUNGWI.
ReplyDeleteMnawafunda kama nani?imekuwa Kitchen party!Kutembea uchi sio mafundisho kwa dini zote mbili.Mabint waache wakafundwe na wazazi wao.Acheni kuendelea kuchuma Dhambi nyie watu.
ReplyDeletemdau Canada
Kwanini mashindo ya urembo yanaendeshwa na wanaume? Kwani hakuna wanawake wanaoweza kufanya hivyo? Kuanzia ngazi ya taifa mpaka ngazi ya vitongoji ni wanaume. Wanawake mko wapi jamani? Nawashauri wasichana wanao ingia kwenye mashindano wadai haki ya mashindano yao kuratibiwa kusimamiwa na kuendeshwa na akina mama vinginevyo mmmmm
ReplyDeleteTangu lini kina baba wanawafunda mabinti zao??
ReplyDeleteYaani hao kina baba ndo wachezewa hivyo, lol. kwanini wasikae madarakani huko Miss Redds. Na hao wazazi wanaoacha wtoto wao wawe chini ya hawa kinababa ktk onyesho hili la kike sielewi, mbona hamna wanawake jamani au wanaume ndo wajua urembo zaidi siku hz.
ReplyDeleteVery shame, hivi hakuna tena maadili Tz? Maana mi nimetoka huko muda mrefu, hawa wazee ndo wanawaangalia wajukuu zao uchi? hamuoni haya? mmmh kwani kuwa mrembo hadi ujionyeshe mapaja, hii style mmeikopi kwa wale walikuja kuwaambia msaada hakuna hadi mmekubali ndoa za mashoga. Kwani wazazi hamuoni/ wenye dini je? Na serikali vipi.
ReplyDelete