Baadhi ya Warembo watakaoshiriki shindano la kumpata Redd's Miss World Tanzania 2012 wakiwa kwenye picha ya pamoja katika kambi yao iliyopo kwenye Hotel ya Kitalii ya Giraffe jijini Dar Es Salaam tayari kwa maandalizi ya shindano lao litakalofanyika siku ya jumamosi hii,lengo likiwa ni kumpata mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Dunia yatakayofanyika nchini China.warembo hao ni 1.Gloryblaca Mayowa (Lindi)2. Hamisa Hassan (Kinondoni)3. Queen Saleh (Ilala)4. Christine Willium (Iringa)5. Pendo Laizer (Arusha) 6.Lisa Jensen (Mara)7. Mwajuma JUma (Tmk)8. Neema Saleh (Ilala) 9.Jeneffer Kalolaki (Ilala) 10.Stella Mbuge (Kinondoni).
Redd's Miss Tanzania,Salha Israel (kushoto) na Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania,Albert Makoye (kulia) wakiwakaribisha Warembo hao kwenye kambi maalum iliyopo kwenye Hoteli ya Kitalii ya Giraffe Jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 14, 2012

    Jinsi Biashara ya Ushindani wa Urembo, Muziki, Sinema na habri/Media inavyofanywa kwa moyo Tanzania, ingekuwa moyo huu unapelekwa kuanzisha Teknologia, viwanda, kilimo cha kisasa, naapa tungefika mbali sana. Labda tungekuwa tunakimbizana na Marekani, Japan, China na South Korea. Ulaya hawana mpango.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 14, 2012

    Mtanzania amewekeza zaidi katika Muonekano, Ngono,kutokuwa na malengo ya baadae au kuwa na muono wa mbali, pia Mtanzania anazingatia zaidi Sifa.

    Ndio unakuta Umaarufu wa mtu ktk Tanzania haulingani na Uwezo wake kihali, unakuta mtu ana jina kubwa lakini hana kitu (kiuwezo)!.

    Mtanzania mara zote hafanyi mambo kwa tija, yeye anajali muonekano, starehe ya muda mfupi na umaarufu tu ndio maana hatufiki popote!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 14, 2012

    Hivi kweli huu ushindani wa urembo unatusaidia nini Tanzania kama nchi maskini kwani hayo mapesa yasiwekezwe katika mashindo ya masomo na uvumbuzi. Hawa mamiss wanailetea sifa gani ya maana nchi yetu isipokuwa kuandikwa hovyohovyo magazetini.Tubadirike sasa tungependa kuona mashindano hayo yanafanyika kutafuta vipaji vya watu katika ELIMU na UVUMBUZI kwa faida ya nchi yetu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 14, 2012

    Wowowo no longer stylish, what a shame!

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 14, 2012

    Binti wa mbele picha ya mwisho mzuri ila katumbo kidogo ahkaendani na mwili wako, fanya sit ups sana na utatoka...all the best

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...