Waziri wa Habari, vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali leo jijini Mwanza.Pamoja na mambo mengine amewataka maafisa hao kuielimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo yanayofanywa na serikali kupitia vyombo vya habari.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Seith Kamuhanda (mstari wa kwanza) akifuatilia mada kuhusu changamoto zinazoikabili Tanzania katika kuhama kutoka mfumo wa Analojia kwenda Digitali kufikia mwaka 2012 katika Kikao kazi cha Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali leo jijini Mwanza. Wengine wanaoonekana nyuma ni maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali.
Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Mwanza.
Waziri wa Habari, Vijana na Utamaduni Dkt. Fenella Mukangara (mstari wa kwanza katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara hiyo na maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali mara baada ya kufungua kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano leo jijini Mwanza.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 12, 2012

    Mdogo wangu anazeeka haraka na majukumu ya Serikali na siasa. Yasikutia pressure mambo ya huko uliyakuta na utayaacha. Mafile watu wanayachakachua huko.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 13, 2012

    Mdau wa kwanza naona ni kweli hasa, mama Daudi amebadilika kabisa, beefing up na uso umechoka. A shock to me the sudden change. Hao mafisadi amewakuta na atawaacha hapo, they are a powerful force in Bongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...