Shule ya Msingi Mlimani ni moja kati ya shule kongwe hapa Tanzania. Shule hii ilianzishwa miaka ya sitini na hadi sasa imetoa vijana wengi wanaolitumikia Taifa la Tanzania kwenye Nyanja mbalimbali. Shule hii iliyopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Vijana wengi wa Chuo Kikuu, Savei, Makongo, Sinza, Kimara na maeneo ya karibu wamepita hapo.
Kutokana na kula chumvi nyingi, majengo na miundo mbinu ya shule hii yamechoka. Ili kuboresha majengo vijana waliosoma hapo wakajikusanya na kuanzisha ‘’ Giving Back to Mlimani Day’’. Mwaka huu siku hii iliangukia jumamosi ya Tarehe 30 June 2010. Mlumni wa Mlimani wanawashukuru MNO wadau waliotoa; Jasho, Fedha , Muda na kusaidia kufanikisha shughuli hii.


Alumni wa Mlimani Primary wakileta vitendea kazi.


Dr. Tage akipaka rangi huku Salma Magimbi akimpa muongozo


Mdau wa Mlimani primary Imani Kajula akipiga ‘’chepe’’


Moja ya madarasa yaliyofaidika na ‘’Giving back to Mlimani’’


Wadau wa Mlimani Primary; Majuto, Tage, Tahir, Sawiche, JP na Huila baada ya kupiga mzigo


Alumni wa Mlimani wakiwa kwenye picha na Mwalimu Msuya kwenye ‘’Giving back to Mlimani’’


Kazi na dawa, misosi pia ilikuwepo; Huila, Victor matondane na wadau wengine wakipata menu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2012

    Hongera sana Mlimani Alumni!

    Mabosi mliopo katika Idara mbalimbali na Mashirika, shime tujitokeze tukumbuke shule tulizotoka kipindi hicho.

    Tufanye jitihada kuzitupia macho angalau zing'are baada ya miaka kadhaa kupita nazo angalau zipate muonekano.

    Hali ni ngumu, inatia huzuni sana kuona darasa ulilosoma miaka ile hali yake ipo palepale.

    Hadi chata za Masela kama 'Mchizi kapita saa nane usiku' ,chata zingine ukutani kama 'mkumbuke Cozza Lee', pia chata kama 'Jitu Kumbuka' zikiwa bado zingali zinasomeka katika kuta!

    Je ni nani afanye kama sio sisi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2012

    Ankal Mlimami Alumni shughuli hiyo hewani,,,vipi mbona hujaturushia picha za yaliyojiri ktk shughuli ya Kinondoni Secondary kule CINE CLUB last week?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 03, 2012

    Huu ni mfano wa kuigwa, hivi kila waliosoma shule wakisaidia mambo si yatakuwa mswano? tukisubiri tufanyiwe Yesu atarudi sisi tunasubiri!. Huu ni mfano, na sisi tuliomaliza Oysterbay primary tutafanya kweli.

    Badala ya kukumbukana kwa party tufanye mambo yenye kujenga na kuongeza chachu ya mafanikio.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2012

    nimeipenda sana hii kwa kweli,i could go aswell,mimi pia nilisoma hapo mlimani primary some 14yrs back ndio nilimaliza,nipo nje ya nchi now,i wish ningekuwepo that day nijiunge na wadau,viva Mlimani,,WE CARE FOR OUR ENVIROMENTS,,n congrats WADAU kwa jambo hili la kimaendeleo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 03, 2012

    Mimi nilimaliza hapo miaka kumi na tisa iliyopita lakini hali yangu bado tete, ndiyo maana sikuweza kujitokeza maana ukifuatilia watu wote waliojitokeza wametoka kimaisha, wabongo huwa tunachorana sana,
    utasikia mara ooooh huyu jamaa alikuwa mtundu sana tulijua tuu ataishia hapa alipo

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 03, 2012

    Kweli badala ya kuilaumu serikali kila mara kwa kutozitunza shule zetu(ukizingatia serikali yenyewe imebeba majukumu makubwa sana)wazo la hawa ndugu zetu ni mfano wa kuigwa sana; na ingekuwa vizuri hii ingetumika kama njia muafaka na taasisi husika, kuboresha shule zetu; i.e. kuomba watu kujitolea waliosoma shule mbalimbali, wanakutana na kuamua wao wanawezaje kuisaidia zile shule husika, labda wengine wanaweza kujitolea madawati,viti, vitabu au ujenzi wa choo, n.k nk. sehemu inayobaki ndiyo inafidiwa na mfuko wa serikali. Ingeleta maendeleo kwa kasi sana; badala ya kuchangia harusi tu. Jamani big up sana, kwa wazo hili, na Mungu awabariki na kuwarudishia pale palipopungua

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2012

    Big Up kwa Mlimani Alumni... Naomba na Sisi Bunge Primary Alumni tuikumbuke shule yetu. Imechoka sana siku hizi yaani hadi aibu. Tujitokeze kusaidia shule yetu BUNGE!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...