Na Mashaka Mhando,Muheza


BENKI ya NMB Tawi la Muheza imezindua kampeni ya kuwapa elimu wanafunzi wa shule za msingi wilayani Muheza juu ya uelewa wa matumizi ya fedha na utunzaji.

Uzinduzi huo umeanzia katika shule ya msingi ya Mbaramo wilayani Muheza ambapo zaidi ya wanafunzi 50 wa darasa la saba walipatiwa elimu hiyo ambayo wameifurahia na kuahidi kupeleka kwa wazazi wao na jamii kwa ujumla.

Meneja wa huduma kwa wateja wa benki ya NMB Tawi la Muheza Shamimu Ally alisema kuwa benki hiyo inaakaunti maalum kwa watoto waliyochini ya miaka 18 iitwayo NMB Junior Account ambayo imewekwa mahususi kufundisha jinsi ya kuweka fedha kwa ajili ya matumizi ya baadae.

Alisema kuwa NMB kupitia sera yake ya msaada kwa jamii ambayo ipo katika mambo makubwa matatu yaani elimu, Afya na Michezo kupitia sera hiyo inampango uitwao NMB Financial Fitness ambapo mkakati huo ni kufanya kila mmoja awe na uelewa wa matumizi ya fedha ikiwemo kujenga afya yake.

Meneja huyo alisema kuwa uzinduzi huo uitwao NMB Financial Fitness unaimanisha kuwa na uelewa wa maswala ya kifedha kwa mfano inakataza mtu kukopa kama hajui jinsi ya kuweka fedha na kwamba mtu akijua jinsi ya kuweka fedha atajua jinsi ya kutumia fedha kwa ungalifu.

Kwaa upande wake Afisa mikopo wa Benki ya NMB Tawi la Muheza Bi Zamda Rashidi katika uzinduzi wa mpango huo aliwakabidhi wanafunzi hao wa shule ya msingi Mbaramo vitabu vya kwenda kusoma ili kujua elimu hiyo.

Rashidi aliwataka wanafunzi hao kwenda kutoa elimu hiyo kwa wazazi wao na walezi ili kuhakikisha wanafahamu mpango huo ambao utawawezesha kujua maadili ya kukopa kwa uadilifu kuliko sasa, baadhi yao wanakopa na kwenda kununua vidani vya dhahabu.

Aliwataka wanafunzi hao kufungua akaunti ya watoto katika benki ya NMB ili kujiwekea fedha zao kwa maisha ya baadae hatua ambayo ijawajengea uwezo wa kiuchumi na kuingia katika mfumo wa kisasa wa kuweka fedha benki.

Rashidi alisema kuwa mpango huo utaendelea katika shule mbalimbali za msingi wilayani Muheza kwa ajili ya kutoa uelewa huo utakaowasaidia watoto wa shule kujua umuhimu wa kuweka fedha benki.

Viongozi hao waliwauliza wanafunzi hao maswali ya kibenki ambapo aliyejibu vizuri alipewa zawadi ya rula.

Kwa upande wao wanafunzi hao na walimu wao walishukuru kwa kupewa elimu hiyo nzuri na watu wa benki na kuahidi watapeleka ujumbe huo kwa watu wengine ili wafahamu huduma za kibenki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...