TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE,INAELEZA KUWA MELI YA ABIRIA ILIYOTAMBULIKA KWA JINA LA MV. SKAGET ILIYOKUWA IKIELEKEA ZANZIBAR KUTOKEA JIJINI DAR ES SALAAM NA ILIYOKUWA NA ABIRIA ZAIDI YA 200,IMEPINDIKA NA KUANZA KUZAMA BAADA YA KUZIDIWA NA MAWIMBI MAKUBWA YALIYOKUWA YAKIPITA BAHARINI.

AJALI HIYO IMETOKEA MUDA MFUPI ULIOPITA KATIKA KISIWA CHA CHUMBI AMBAPO NI MPAKANI KWA DAR ES SALAAM NA ZANZIBAR.

VYOMBO VYA UOKOAJI VIKO NJIANI KUELEKEA ENEO LA TUKIO HIVI SASA NA LIBENEKE LA GLOBU YA JAMII LINAENDELEA KUFUATILIA KWA UKARIBU TUKIO HILO NA TUTAENDELEA KUPEANZA TAARIFA KADRI ZINAVYOPATIKANA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2012

    Ooh!yale yale tena ya kuzidisha abiria? Mungu awanusuru wote waokolewe wakiwa salama.
    TUWAOMBEE HERI NDUGU ZETU.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2012

    Ohoo, yale yale!!! http://wolfganghthome.wordpress.com/2012/02/20/zanzibar-news-updae-mv-skagit-stopped-from-sailing-to-pemba-by-zam-over-safety-concerns/

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 18, 2012

    Eee mwenyezi mungu mwingio wa rehema tuepushe na maafa na wasafiri wote waokolewe watanzania tuungane kwa sala.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 18, 2012

    YA'ARABI TUNUSURU WAJA ZAKO,YA'AALLAH!
    HIVI NINI!MUNGU WANGU TUOKOE TUMEZIDIWA SASA!!!!
    NIMESTUKA MNO JAMANI MIMI!
    KUFUNGUA TUU,HII HABARI IKO JUU!!
    TUSAIDIANE KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU SANA!
    ATUKINGE NA HAYA MAJANGA!
    AHLAM,,LONDON

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 18, 2012

    huu ni msiba mkubwa kwa mara nyengine tena! hivi vyombo vya usafiri vya majini huwa havizingatii habari za hali ya hewa??? my thoughts and prayers to the families of the deceased, and wishing quick recovery kwa wale walioumia. what a tragedy!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 18, 2012

    Hivi Dunia nzima vyombo vya usafiri tunamiliki sisi pekee?

    Hivi ni kwa nini Kanuni,vigezo na mashariti,Taratibu na Sheria ktk uendeshaji wa vyombo na biashara za usafiri havizingatiwi?

    Tutakwisha hadi lini?

    Wazanzibari tufuate taratibu na kanuni na tusipende vitu kwa njia za mkato na magendo!

    Inawezekana Meli haikuwa na vigezo vinavyostahili lakini ikalazimishwa kwa njia za mkato mkato kuendesha biashara.

    Je, kwa madhila haya tutapata kulaumiana ya kuwa hizi ndio kero za Muungano?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 18, 2012

    Tuwaombee wasafiri

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 18, 2012

    vp ankali mbona kimya hizo taarifa nusu nusu tupashe basi tuhabarike vyema kinaga ubaga.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 18, 2012

    inna lillahi waina illahim rajiun rahman atuwafikishiye salaama ndugu zetu wazazi wetu, jamaa zetu, marafiki zetu na majirani zetu . amin.

    mdau New York

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 18, 2012

    Imepindikaje?Unamaanisha ilikatikakatikati au namna gani,sijaelewakichwa cha habari.

    ReplyDelete
  11. a.k.a mimiJuly 19, 2012

    ...innaa lillahi wa innailahi rajiun!jamaan eeh,enyi wadau wa vyombo vya usafiri vya majini 2seme ume2pangia ki2 gan haswa?kutumaliza au?timizen wajibu wenu kwanza maslah baadae!msiufanye usafir wa majin kuwa usafiri hatarishi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...