Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kalley Pandukizi (kulia) akimkabidhi Kitabu cha Katiba na Sera za Chama Mwenyekiti mpya Ndugu Cosmas Wambura.
 
Tawi la Chadema Washington DC limepata Viongozi wapya walioshika nafasi za waliokuwa Viongozi wa muda. Katika Uchaguzi huo Cosmas Wambura amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda Kalley Pandukizi. Nafasi ya Katibu imechukuliwa na Isidori Lyamuya aliyechukua nafasi ya Liberatus Mwang’ombe aliyekuwa Katibu. Nafasi ya Mweka hazina imechukuliwa na Ludigo Mhagama na nafasi ya katibu mwenezi imechukuliwa na Hussein Kauzella. Nafasi nyingine zilizogombewa ni Wenyeviti na Makatibu wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee. Pia kulikuwa na nafasi ya Afisa Habari wa Chama. Akiongea baada ya Uchaguzi Mwenyekiti aliyechaguliwa ndugu Cosmas Wambura amesema atatoa ushirikiano mkubwa katika kuendeleza shughuli mbalimbaliza kukijenga Chama. Pia Katibu mpya amesema watashirikiana na Mwenyekiti na wanachama wengine wote kuhakikisha Chama kinzidi kuwa Imara na kupata wanachama zaidi.
Mwenyekiti mpya wa Chadema Washington Cosmas Wambura akipeana mikono ya pongezi na Katibu mpya Ndugu Isidori Lyamuya.
Kutoka kushoto Katibu mpya Isidory Lyamuya, Mwenyekiti mpya Cosmas Wambura, Katibu aliyemaliza muda wake Liberatus Mwang'ombe na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kalley Pandukizi.
Baadhi ya wanachama wa Chadema walioshiriki zoezi la Uchaguzi la kupata Viongozi wapya wa Chadema Washington DC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2012

    Nina omba kuliza kuna Tawi la chama Democratic or Republican party Tanzania?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 16, 2012

    Ha ha! More leaders than the audience and followers... wondering..

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 16, 2012

    POA SANA WANAUME WA US HAMNA MAVITAMBI, V GOOD

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 16, 2012

    Huyo nae anachekesha mavitambi na box wapi na wapi

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 16, 2012

    nyumbani kunikushindeni sasa huku mnataka kutuleta balaa

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 16, 2012

    umeambiwa baadhi ya wanachama we hapo juu tukuelewe vipi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 17, 2012

    Haya sasa Chadema chaguaneni huko Marekani halafu mje kwenye Uchaguzi Bongo sisi CCM tuwamwage vibaya !

    Mtapata Kura kama namba za viatu, mfano Vituo vingine Kura zinahesabiwa mnajikuta mnapata Kura 5, 6,9,8 na 7 !

    Ebo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...