Mkazi wa eneo la Mbagala Rangi tatu jijini Dar es salaam akivuka katika dajara lililopo katika mtaro uliopo katika barabara ya Kilwa road

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2012

    Diamond alikosea?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2012

    Kaka Michu, nakuomba sana picha za namna hii usionyeshe,maana duh !!watu wa UK wataponda ile mbaya, siunaona hapo juu ?? tayari wameshaanza- wewe waonyeshe magorofa au kwa msemo wako ,vikwangua anga basi,mambo ya madaraja kama haya tuachie sisi wa hapa hapa.Zebedayo.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2012

    Hivi barabara zetu zikishajengwa hakuna utaratibu unaowekwa wa kuzisimamia kama vile usafi wa mitaro, kufagia n.k? Kazi ya manispaa ni ipi katika kuboresha na kulinda miundombinu iliyojengwa kwa gharama kubwa kutoka ktk kodi za walalahoi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2012

    Kweli Ankal, mdau hapo juu yuko sahihi kabisa. Hii blogu yako inasomwa duniani kote ndugu yetu, sasa mambo kama haya yabakie na sisi jamani tusijiumbue wenyewe. Labda atakapotokea mtu akaanzisha blogu kwa ajili ya viongozi wetu tu au labda kwa ajili ya wakuu wa mikoa tu au mawaziri tu, then tutakuja na picha za kila aina humu, tukionesha maeneo yanayohitaji usimamizi wa karibu ili yawe inavyotakiwa. Lakini haya ya kutuumbua tuwaachie akina CNN, ALJAZEERA, SKY NEWS, n.k. Mfano, ni nadra sana kusikia habari njema za TZ zikitangazwa na media kubwa duniani lakini ikitokea balaa kama hii ya juzi ya meli, wote wanaitangaza bila kuchelewa!!!! Ankal, please lizingatie hilo tafwadhali.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2012

    Ankal, nadhani umeupata ujumbe kutoka kwa wadau hapo juu, maeneo kama haya ni sawa na mabanda ya uhani, sasa siri ya huko mabanda ya uhani, hmmm ankal iache hivyo hivyo, wachie hao wana world news watumbue kama alivyosema madau hapo, Manake nilikua nimefingua blog hii nisome na niko na marafiki zangu ambo awajafika bongo, tunavyopenda isifia bongo yetu, mara nikakutana na picha hii, weeeee Hapo chacha niliakikisha na napeleka picha haraka isionekane na haya mabanda ya uhani, ukiletaga za vile vikwangua anga aaaaa, hapo mulua, shuti unaichia ionekane na kuisoma habari pole pole, na wakiuliza hapo wapi haraka haraka hapa bongo

    ReplyDelete
  6. Nadhani hakuna ubaya wowote kuziona picha kama hizi, kwani ndio mazingira halisi ya baadhi ya maeneo/mitaa ya sehemu mbali mbali za nchi yetu. Mazuri yapo na mabaya kadhalika. Picha hiyo tayari ujumbe wake umefika na pengine kuwafikia wahusika sahihi na kuanza kulitafakari au kulitafutia ufumbuzi suala hil na kulifanyia kazi ASAP.

    Hata hivyo, kidaraja cha kuvukia kipo maalum, sema tu uvivu umetuzidi, tunapenda kutumia 'shortcu't ila huo mtaro ndio kichefuchefu pia ni mazalio mazuri ya mbu, hivyo manispaa au wizara husika ujumbe ndio huo katika picha, tunataka uwajibikaji.

    ReplyDelete
  7. acheni upuuzi wadau, michuzi endelea kuleta picha zote hasa za uasilia wa maisha yetu, ndivyo tulivyo jamani. Safi sana kaka michu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 22, 2012

    Unaona??? yale yale Kaka Michu, sasa tunaambiwa wapuuzi eti kwa kuficha siri zetu. angalieni jamani,daraja la kuvukia lile paleee tena linaonekana vizuri sana , sasa huyu mbongo kwa haraka zake kaweka gogo la mnazi ili awe karibu na kibanda chake cha kuuzia simu, sasa huyu ndo anatufanya tuchekwe na watu wa UK,walivyo wepesi kwa kukosoa,kumbe huko waliko ndiyo hovyooo kabisa,mavyakula frozen ya majuzi yale,wakati sisi huku tunakula fresh kila siku,nyama mpya kila siku, samaki wanatoka ferry kila siku saa 12 za asubuhi wengine bado wazima. Nikisema bongo ni peponi !!! watu wa UK wanakinga ngumu. Najua ukweli unauma daima. Na huo uchafu kwenye mtaro, ngoja VODA watakapofanya promotion zao maeneo hayo ,huo mtaro utasafishwa saaafi. Nyie mmekimbia wenzenu wamekuja kuwekesha huku na wanazichota kweli kweli. Zebedayo, nitafia bongo na nitazikwa bongo.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2012

    Huu mtaro unatakiwa kusafishwa na mitaro yote kuwekewa mifuniko ya juu kwa jinsi ilivyo sio salama kwa watoto na wazee wasiojiweza.Pia sio salama kiafya pamoja na mazalio ya malaria.
    Mdau UK

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 22, 2012

    kazi kweli kweli ndugu zanguni. kwani michuzi asipotoa hizi picha kwenye blog mambo yatabadilika? nini maana ya kufahamisha jamii ? Anyway mficha uchi..... Na hili swala la watu kutaka kufananisha kila kitu na US au UK, huo ni ujuha wa hali ya juu eti frozen foods ivi we umeshatoka nnje ya TZ au unahadithiwa tu maisha ya ughaibuni? kwa kifupi DIASPORA sio adui yako kama unavyotaka iwe. adui yako ni mmbu, rushwa, ujinga, njaa, ubinafsi na uelewa mdogo.Kua kijana acha inferiority minds. Dunia ya kwanza ni ya kwanza na sisi tukijitahidi tutafika ila watu wenye mawazo finyu lazima wabadilike au watoke. Long live MICHUZI BLOG!!!!!!!!!!!

    Mdau, Dirty South

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 23, 2012

    Inaelekea watu wengine wanajisifia mpaka wanapitiliza! Sitashangaa kukuta ni wale wanaoona ni heri angezaliwa mbwa nanihi!


    sesophy

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 23, 2012

    Kusafisha mitalo si kawaida yetu, bali mvua inaponysha ndiyo inayosafisha na vilevile unakuwa ndiwo wakati wa kutapisha vyoo. Hii ndiyo kawaida ya Uswahilini Bongo, ndiyo maisha ya nenda rudi!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...