Mmoja wa Waasisi wa TANU NA CCM,BI KANDURU AKIMPA MKONO MKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA BI Regina Chonjo baada ya Mkuu huyo kutembelea makazi ya Bibi huyo ambapo alipata ufadhili wa kujengewa Nyumba hiyo na kusikitishwa na Alivyotapeliwa katika ujenzi wake.
WAZEE WA NACHINGWEA WAKIMSIKILIZA MKUU WA WILAYA YAO NA BILA KUSITA WALIDAI KUSHANGAZWA KUPATA WITO WA MKUU WA WILAYA KUKUTANA NA WAZEE KWA KUWA KATIKA HISTORIA YAO HAWAJAWAHI KUKUTANA AU KUSIKIA JAMBO HILO KWAO.

NA ABDULAZIZ VIDEO.

MKUU wa wilaya ya Nachingwea,Regina Chonjo amekerwa na hali ya uchafu uliozagaa kwenye maeneo mbalimbali ya mji wa Nachingwea na kuitaka jamii kushirikiana naHalmashauri kujenga tabia ya usafi.

Chonjo alisema kuwa licha ya kuwa na virimba katika maeneo mengi ya mji bado wananchi wanaendelea kutupa taka ovyo na kufanya kila eneo kuwa ni dampo.

“Kwa kweli hali ya mji wetu ni mbaya kwani hata siku ambayo nilifika nilionahali hiyo na nilishamweza mwenyekiti wa halmashauri kuwa hali si ya kupendeza na kumpataka kuweka mkakati wa kuwashirikisha wananchi”alisema Chonjo

Alisema kuwa kama watu wakishirikishwa kikamilifu wanaweza kubadilika kitabia na kujali usafi na mji wetu ukawa wa mfano kwa usafi kama ilivyo mji mingine ambayo tabia ya usafi ni ya kawaida.

Kauli ya mkuu huyo wilaya aliitoa jana wakati akizungumza na wazee wa maeneo ya mji wa Nachingwea aliokutanao kwenye ukumbi wa chuo cha ualimu kwa lengo la kujitambulisha na kubadilishana mawazo.

Awali swala la hali ya uchafu uliokithiri kwenye maeneo mbali mbali ya mji wa Nachingwea lilisemwa na mmoja wa wazee hao,Albert Mnali ambaye alisema kuwa maeneo ya yaliyo wazi yamegeuka kuwa madampo kwani kila eneo linatumiwa kutupia taka.

Mnali aliisema kuwa halmashauri imezidiwa na taka kwani taka zinazozalishwa ni nyingi ikilinganishwa na uwezo wa kuzisomba kwani halmashauri halina gari la kuzolea taka.

Mnali aaliishauri hamashauri kumtafuta mzabuni atakayekuwa na jukumu la kuzoa taka badala ya kufanywa na halmashauri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2012

    Sasa baada ya kusikitishwa na utapeli huo DC kachukua hatua gani? Maana kwa nafasi yake akiishia tu kusikitika utakuwa ni unafiki tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...