Bw. Donatius Kamamba (pichani), Mkurugenzi wa Mambo ya Kale katika Wizara ya Maliasili na Utalii , ameteuliwa kuwa mjumbe wa  Kamati ya Utendaji  ya Shirika la Kimaifa lisilo la Kiserikali liitwalo  The International Council on Monuments and Sites  - ICOMOS” kwa kipindi cha miaka mitatu (3) hadi Novemba,  2014. Uteuzi huo ulifanywa na Gustavo Araoz, Rais wa ICOMOS tarehe 3 Julai, 2012.
ICOMOS ni Shirika  la Kimataifa lisilo la kiserikali lenye jumla la nchi wanachama 98. Majukumu yake ni pamoja na kutoa ushauri kwa UNESCO kuhusu Uhifadhi wa Urithi wa Utamaduni na hufanya tathmini ya maeneo yanayopendekezwa kuingizwa kwenye Orodha ya Urithi wa Utamaduni  - World Heritage Sites. Aidha, ICOMOS inalo jukumu la kutathmini shughuli za uhifadhi zinavyotekelezwa katika maeneo ambayo tayari yapo  katika Orodha ya Urithi wa Utamaduni.
Kuteuliwa  Bw. Donatius Kamamba kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya ICOMOS ni ishara kuwaTanzania inayo taaluma katika fani ya Uhifadhi wa Urithi wa Utamaduni na inayatunza vizuri maeneo husika yaliyoko nchini. Maeneo hayo ambayo ni vivutio vya utalii ni kama vile: Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songomnara, Michoro ya miambani ya Kondoa, Eneo la Bonde la Oldupai, Nyayo za Zamadamu zilizoko Letoli, Miji ya Kihistoria ya Pangani, Kilwa Kivinje na Mikindani, Majengo ya kihistoria ya Ikulu , Maboma ya Kijerumani ya Biharamlo na Mahenge na Njia ya Kati ya biashara ya Utumwa.
Aidha Bwana Kamamba anazo nyadhifa nyingine za kimataifa. Mwaka 2007 alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la  Uongozi wa Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Urithi wa Rasimali za Utamaduni (International Centre for the Study  of Preservation and Restoration of Cultural Property - ICCROM), kilichopo Roma, Italia. Pia mwaka jana Novemba, 2011, aliteuliwa kuwa Rais wa nchi wanachama wa ICCROM kwa kipindi cha miaka miwili Novemba ,2001 mpaka Novemba, 2013.

[MWISHO]
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA  MALIASILI NA UTALII
17 Mei 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...