Wakati tunapoelekea katika shamra shamra ya sikuu ya Saba Saba,
watanzania tunafurahia sikuu hii kwa kupata burudani ya raha ya nyimbo
mpya zilizopo katika CD "Bongo Tambarare" kutoka kwa bendi maarufu ya
muziki wa dansi  Ngoma Africa Band aka FFU yenye maskani nchini Ujerumani, CD hiyo yenye nyimbo tatu  "Bongo Tambarare" , "Supu ya Mawe" na "Uhuru wa Habari" imeshaanza kupiga hodi katika milango ya vituo mbali mbali vya redio duniani na hapa nyumbani itasikika wakati wowote kuanzia sasa ili watanzania wenye Bongo Tambarare yawe wapate raha ya muziki. 
CD hiyo yenye nyimbo tatu zilizojaa ujumbe wenye furaha na mafunzo kwa jamii, kama vile "Supu ya Mawe" ni utunzi na  wake kiongozi wa bendi hiyo kamanda Ras Makunja wa FFU akiimba kwa kushirikiana na mpiga solo afande Chris-B. Watanzania tuipokee CD "Bongo Tambarare" na tufurahie Saba Saba kwa kupata raha ya "Supu ya Mawe" kutoka kwa Kikosi kazi Ngoma Africa aka FFU.
unaweza kusikiliza pia at www.ngoma-africa.com 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2012

    Enhhhh bngpo Tambarale na Supu ya Mawe.

    Supu hii ya mawe ndio ya kuzimulia baada ya kunywa gongo la mabibo!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2012

    kichwa cha habari kina makosa. Kiswahili sahili wanasema kupeleka, na siyo kupereka

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 03, 2012

    FFU wana visa vya kila aina sasa hii supu ya mawe jamani tutakunywa vipi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2012

    sasa kwani akina ffu hawalali usingizi ? vichaa wetu ffu kila kukicha lazima wataibuka na mpya na kutingisha umma,au kuna nguvu za kiza nyuma yao?zinawaongoza.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 03, 2012

    Ebwana eeeh,

    Wana wa Ras Makunjas inabidi mfanye mpango wa makaratasi kabisa huko Majuu kwa njia yeyote ile iwe hata ya Vibali vya Uganga wa Kienyeji maana Wazungu Taaluma hiyo hawana, ikishindikana Ndoa na Vikongwe!

    Kwa vile mkijipindua tu kurudi Bongo kwa jinsi mlivyolizima na kukaa sana huko ni wasi Mjerumani hatawapeni tena visa!

    Msirudi Bongo kihasara hasara msije mkabaki na ziara za Msumbiji na Malawi!

    Jeremani ndio Mshirika mwenye roho ya ngumu kabisa, mashariti na sheria kali katika nchi zote za Umoja wa Ulaya.

    Jeremani mchezo?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 03, 2012

    Sasa Ankal Michuzi hii supu ya mawe si hatari tupu maana inawekukwama kooni,hivi kichwani mwa huyu mtunzi mna kitu gani?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 03, 2012

    Sasa Ankal Michuzi hii supu ya mawe si hatari tupu maana inawekukwama kooni,hivi kichwani mwa huyu mtunzi mna kitu gani?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 03, 2012

    Kiswahili sanifu ni "Tambarale".

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 04, 2012

    wewe anony wa 01:04 2012,
    Sasa unawashauri akina ras makunja watafute makaratasi,una mawazo gani? unadhani kuwa miaka yote hiyo ndio wasiwe na makaratasi au vibali vya kuishi ujerumani. usiwe na mawazo kila mtu anayeishi ulaya ni mdandia meli au anaishi kiujanja ujanja

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 04, 2012

    kamanda ras makunja wakati mwingine unaanzisha baraha na nyimbo zako,sasa supu ya mawe kamanda wetu tutainywa vipi? kama si kuwatafuta watu ubaya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...