Msanii Mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya Fid Q akiwapagawisha wakazi wa Mkoa wa Mtwara hapo jana wakati wa tamasha la"WAJANJA" linaendeshwa na Vodacom Tanzania,Jumapili ijayo litafanyika katika mkoa wa Tanga minne likiwa na lengo la kuwaelimisha wananchi kutumia mtandao wa kampuni hiyo kwa kuongea kwa robo shilingi na kutuma ujumbe kwa shilingi ishirini na tano kwenda mtandao wowote na kutumia facebook na twitter.

Katika hali isiyotarajiwa na wengi Msanii na Mkali wa Bongo Fleva Farid Kubanda maarufu kama Fid Q juzi alifunika katika shoo wa Wajanja tour ya Vodacom iliyofanyika Mtwara jumapili hii na kusababisha mashabiki waliojitokeza katika tamasha hilo kukataa asishuke jukwaani.

Fid Q aliepanda jukwaani majira ya saa kumi na moja na nusu baada ya Diamond kumaliza Shoo yake, na alipopanda jukwaani umati wa wana Mtwara ulilipuka kwa shangwe na kuwapa wakati mgumu mabaunsa waliokuwa wakisimamia shoo hiyo. Hata alipomaliza nyimbo zake mashabiki walipiga kelele kutaka aendelee kuimba na kumwita Ngosha! Ngosha!Ngosha!nakuanza kulisukuma basi alilopanda msanii huyo mpaka nje ya uwanja.

Wasanii wengine waliofunika katika Show hiyo ni Pamoja na Diamond, Shetaa, Ney wa mitego na Mabeste.

Akizungumza na waandishi wa Habari Meneja Mahusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu amesema kuwa Tour ya Wajanja wa Vodacom itafanyika siku ya jumapili ya wiki hii Mkoani Tanga katika uwanja wa Mkwakwani.

"Wajanja tour sasa inaelekea kwa "waja leo waondoka leo" mkoani Tanga baada ya kufunika vilivyo Mkoani Mtwara hivyo wakazi wa Tanga wajiandae kupata burudani kutoka kwa wasanii kibao watakao kuwa katika Tamasha hilo." Alisema Nkurlu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...