Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (kulia), akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 10, Mkurugenzi wa Uhamasishaji wa Mamlaka ya Elimu nchini (TEA), Seif Mohammed.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) akifungua hafla hiyo. Wengine pichani ni Eric Shigongo (kulia) na Seif Mohammed (katikati).
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo (katikati) akisisitiza jambo katika hafla hiyo.
Seif Mohammed (kushoto), akiishukuru Global Publishers na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kuchangia mfuko huo.
Sehemu ya wanahabari waliokuwa kwenye hafla hiyo.
Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakijisevia msosi.
Baadhi ya wanahabari wakipata lunch.

Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd leo imetoa hundi ya shilingi milioni 10 ikiwa ni sehemu ya mapato yaliyopatikana kwenye Tamasha la Matumaini lililoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa hosteli za wasichana nchini. Kampuni hiyo imetoa hundi hiyo kwenye hafla fupi iliyofanyika katika Hoteli ya Atriums iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS / GPL)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...