Wizara ya Maliasili na Utalii inatoa taarifa kuwa hakuna ripoti ya wanyama iliyokaliwa na Maliasili kama ilivyodaiwa na gazeti moja la kila Wiki toleo la tarehe 23 Julai 2012.
Gazeti hilo lilidai kuwa taarifa ya Kamati iliyoundwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuchunguza tuhumu ya watumishi wa Wizara kuhusika na utoroshwaji wa wanyama KIA haikukabidhiwa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Habari hiyo siyo kweli kwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii alishakabidhiwa taarifa hiyo na anaifanyia kazi.
Wizara inasisitiza kuwa suala la utoroshwaji wa wanyamapori KIA linashughulikiwa na mamlaka nyingine za Serikali, na kwa sasa liko mahakamani. Hivyo, siyo wajibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii kulitolea taarifa.
Aidha taarifa ya Kamati iliyoundwa na Katibu Mkuu ni kwa matumizi ya ndani ya Wizara na siyo ya kusambazwa kwa sasa.
                                                                  George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 25, 2012

    Maelezo hewa sana, siamini yametolewa na msomi wizarani.

    Wizara inatakiwa kufahamu kama ni polisi ndio wamapeleleza na wamefikia wapi ili itoe report kamili, sasa kama wizara haitaki kujihusisha, ipo hapo kwa ajili gani?

    Kama kuna mdau anayeweza kujibu nitashukuru

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2012

    Namsifia Kagasheki, Waziri wetu wa mali asili kwa Kuitangaza tanzania kwenye mambo ya utalii, lakini kwa Ubadhilifu wa wakuu wa idara mbali mbali unakatisha tamaa kabisa. Wape vijana vitengo mkuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...