Muokoaji akiwa na mmoja wa maiti wa ajali hiyo. Hii ni baada ya Meli ya Mv Stargate (Skagit) iliyokuwa safarini kutoka Dar kuelekea Zanzibar kuzama majira ya saa nane mchana katika maeneo Pungume na Chumbe baada ya kukumbwa na upepo mkali.
Meli hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana ilipindukia upande mmoja na abiria wengi waliweza kuokolewa kwa jitihada mbali mbali ikiwa ni pamoja na msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, Tug ya Bandari na vyombo vyengine. Maiti kadhaa zilikwishapatikana na kiasi cha abiria 150 wameokolewa na waliojeruhiwa wanatibiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Taarifa zinaeleza kwamba kulikuwa na watoto takriban 30 na Watalii kutoka nchi mbali mbali wafikao kumi.
Wazamiaji kutoka Kikosi cha KMKM pamoja na Jeshi bado wapo eneo la ajali kusaidia kuokoa maisha ya wananchi waliokumbwa na maafa haya.
Taarifa zaidi na picha tutawaletea tutakapozipata
Waokoaji wakiopoa moja ya maiti. wakiwa katika boti ya Kilimanjaro.
Boti ya KMKM ikiwa katika zoezi la kuokowa majeruhi.
Helikopta ya Jeshi la Polisi ikizunguka eneo la tukio.
Boti iliozama ni kama hii ambayo ni pacha wake.
Boti ya Fly Horse ikiondoka katika bandari ya Zanzibar kueleke kutoa msada wa uokoaji.
Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu Mhe Hamad Masoud akiwa katika boti ya Kilimanjaro akiwa sehemu ya Tukio ilipozama boti hiyo maeneo ya Chumbe.
Tagi la Shirika la Bandari likiwa katika sehemu ya tukio.
Hali ilivyokuwa baada ya meli kupinduka. Baadhi ya abiria walionusurika wakisubiri kuokolewa wakiwa juu ya mgongo wa meli
Waokoaji wakiwa kazini. Kazi ilikuwa ngumu kutokana na mawimbi makubwa
Majeruhi wakiokolewa.
TUMECHOKA... KILICHOBAKIA KUANZIA WAZIRI, NAHODHA HADI MKAGUA TIKETI WAFUKUZWE KAZI NA KUSHTAKIWA MAHAKANI.
ReplyDeleteHATUTAKI TUME NYINGINE NI UNAFIKI WA KISIASA.
Nafikir haujui n nan muhusika kama n kuwajibishwa anatakiwa kuwajibishwa wazir wa maliasili na utalii mhe harrison mwakyembe
DeletePoleni kwa waliopeteza ndungu jamaa na marafiki,inasikitisha sana.
ReplyDeleteKama hali ya hewa ilikuwa mbaya sana na upepo wa kusi wa nguvu, kwanini boti ziliendelea kusafiri.
Sijui ni wangapi kati ya hao walioopolewa toka majini na kama bado walikuwa nusu-hai walifanyiwa "CPR", maana inavyoelekea waokoaji hawakuchelewa kufika kwenye tukio la ajali.
Waliotutangulia wapumzike kwa amani, Amen
mi hata sina la kusema,si kwa Hamadi-TRA,Wamiliki wa meli,Wasajili wala Polisi,maofisa bandari na wauza ticket,tumuachie Mungu tu.Maana haiwi nchi ina Mawaziri wawili wa mambo ya usafiri na kila siku vifo.
ReplyDeleteINNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAJIUN.
ReplyDeleteNa tuwe pole sote tulioguswa, kufikwa ama kuondokewa na ndugu, jamaa na marafiki zetu katika ajali hii, pia wawe pole wote walionusurika katika zahma hii. Ingawa hata bado hatujapowa uzuri kufuatia ile ya M.V.SPICE na nyingine hii tana imetokea. Eee! YARABI, tunusuru na utuepushie mitihani yako mithili ya hii na mingineyo. Uzilinde safari zetu ziwe za salama na amani, twendako na turudipo - AMEN.
Wahusika tafadhalini endeleeni kutukhabarisha zaidi chanzo chake ni nini au kimesababishwa na kitu gani. Poleni sana tena sana ndugu zangu wote wa Visiwani na nyote mliofikwa na janga hili, Zanzibar na Tanzania nzima kwa jumla.
Many thanks Michuzi kwa kutupa updates kwa picha. Inauzunisha na kutia uchungu sana.
ReplyDeletePoleni sana wahathirika, ndugu jamaa na marafiki wa waliopata ajali. Kwa kweli inasikitisha na inatia uchungu sana.
ReplyDeleteBora zijengwe barabara tu kutoka Zanzibar to Dar na Unguja to pemba la si hivyo basi hili tatizo halitokwisha maisha!! tutabaki tukiteketea kila kukicha!! mdau Leicester. uk.
ReplyDeleteInnallilahi Wainaillaihi Rajiuna, poleni sana wote waliokumbwa na huu mkasa na tukumbuke kuwa lahaula walla quwatta illa bi idhnillahi. Kwa sababu sidhani kama kwa siku ya leo tangia asubuhi ni meli hii peke yake iliyosabiri lakini hii ndio iliyoandikiwa ikumbwe na hiyo dhahma. Upepo wa kusi haukuanza kuvuma leo na pia hautabiriki, unaweza ukawa asubuhi haupo mchana ukachagiza yote ni ya Allah Subhana na mitihani yake kwa walimwengu. Cha msingi ni kumuomba Mungu tunaposafiri tufike salama, na tukiwa safarini tuchukue tahadhari za kiusalama zinazotakiwa, labda iwe lazima kuvaa life jaketi kutokea mwanzo wa safari, na pamoja na tahadhari hizo siku ikifika haina dawa tutamlaumu Hamadi sijui nani lakini mengine yako nje ya uwezo wa mwanadamu,
ReplyDeleteWatanzania tumrudie Mungu dhambi zimezidi Tanzania.
ReplyDeleteHii tena imekua mchezo kila mara watu kufa kama kuku, Serikali lazima ichukue hatua kali sana kwa wenye hizi meli si kuacha wanaua watu hovyo, Wanafikiria pesa kuliko roho za watu huu ni uaji umekua si ubinadamu na seriakali inachangia kwa haya yote yanayotokea inakula rushwa kuuwa wanachi wake huu ni upumbavu mkubwa sana.
ReplyDeleteKWANI,KAZI YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA NINI?NADHANI WALIPASWA KUTOA ALERT JUZI, ILI SHUGHULI ZOTE ZA MAJINI ZISITISHWE,NADHANI WANAPASWA KUWAJIBIKA KWANZA KABLA YA MTU MWINGINE YEYOTE.
ReplyDeleteTatizo wahusika wakifuata sheria za usafiri baharini,wanatishiwa kuuawa..wanaogopa.Tumesikia mawaziri wetu waliohusika na bomoabomoa ufukwni Mbezi wameshatishiwa kuuawa!!Kazi tunayo Tanzania
ReplyDeleteInasemekana kutokana na Usajili Holela wa vyombo na Mamlaka za Unguja hiyo Meli ya SKAGET haina hata Ofisi Maalum hapa Dar Es Salaam.
ReplyDeleteTiketi zinakatiwa 'chini ya mti wa mwarobaini' nje Opposite na Shule ya Sekondari ya Forodhani!
Je, ktk mazingira kama haya tutafika kweli?
mamlaka ya hali ya hewa ni kwa ajili ya kusoma mawio na machweo sio kutoa habari ya hali ya hewa inavyoendelea kwa siku nzima nchi kavu na hata kwenye maji.Hivi hii mamlaka ya hali ya hewa kazi yake kubwa nini hasa kwa upande wa usafirishaji wa anga na kwenye maji?
ReplyDeleteJAMANI JAMANI HIVI HILIJESHI LA WANA MAJI WTZ KAZIYAKE NININI NCHINI SPIDI BOT ZA UOKOAJI HATAHIZO HATUNA TUKIO LINATOKEA KUOKOLEWA BAADA YA MASAA 5 KWELI JAMANI INATAKIWA BANDARINI KUWE NA SPIDI BOTI ZA UOKOAJI ZISIZO PUNGUA KUMI SIZANI KAMA WATANZANIA TUKRKUA TUNAKUFA KIASARA NAMUNA HII .
ReplyDeletePoleni sana watanzania kwa ujumla na Mungu baba awatie nguvu wote waliopoteza ndugu zao.
ReplyDeleteSasa mimi nauliza huko nyumbani mamlaka ya hali ya hewa ina fanya kazi gani au haina vifaa, Maana walitakiwa kutoa taarifa mapema ili watu wasitumie bahari,si meli peke yake hata wavuvi, na wanaotumia boti za michezo. Sasa nashangaa huwa wananafanya kazi gani hao wahusika wa hali ya hewa au ni kutoa taarifa za mvua tu.Huku jamani kila baada ya saa moja tunaambiwa hali ha hewa inaendaje na inakuwa kama wanavyosema mfano kama kutakuwa na snow nyingi ili watu wachukue taazali.Mimi kwa maoni yangu naona hao mabwana wa hali ya hewa wachunguzwe upya their education may be hawako educated enough kwa ajili ya kazi hii au hawako serious na kazi yao. Serikali yetu pia iwe serious kuhakikisha inaangalia sehemu muhimu kama hizi maana inasikitisha wahu wanavyoteketea jamani si kwa watumiaji wa majini hata nchi kavu hususani barabara.Jamani jamani maendeleo ya huko yako wwapi inauma sana. Mdau kutoka
Cardiff - UK.
Mimi pia naungana na wengine wote kuwapa pole wote walioguswa na hata kuguswa na ajali hii ya boti/meli! Wengi wanalaumu wahusika (wenye boti, viongozi, nahodha n.k.), pamoja na hayo tusisahau jana hali ya hewa ilikuwa mbaya sana. Kama huku nchi kavu tulikuwa tunapeperushwa na upepo, je hayo mawimbi baharini si ilikuwa mbaya zaidi! Naungana na wale wanaowalaumu Mamlaka ya hali ya hewa: Nadhani wana jukumu la kutahadharisha juu ya matukio yanayohusiana na hali ya hewa! Tatizo lao wanasubiri hadi hali itokee ndo wanatabiri! Hata ile jana nilitania mapema tu asubuhi, baada ya kuona hali ya upepo mkali ukivuma kwa kasi sana: niliwaambia jamaa zangu hawa Mamlaka ya Hali ya Hewa watakurupuka sasa hivi.... na ndivyo ilivyokuwa!
ReplyDeleteTuelezwe kazi yao hasa ni ipi? Je ni kutuambia kuhusu Mawi na Machweo tu? Sikubaliani na wanaosema kuwa ni kazi ya Mungu! HAPANA!! Tujue Mungu ametuumba ili tuutawale ulimwengu na wala hafurahii vifo vya viumbe wake! Tusisahau yule mshitaki wetu Ibilisi shetani, halali, yuko kazini wakati wote ili awaangamize waja wa Mungu! Maana kazi yake ni kuua, kuharibu na kuangamiza!
Tumuombe Mungu atuepushie haya mabaya yanayoikumba nchi yetu! Tutende haki na kumcha yeye peke yake! Siko lake si zito lisiweze kusikia wala Mkono wake si mfupi usiweze KUOKOA!
Naomba Mungu awape Imani wenzetu waliopoteza ndugu zao kwakuwa sisi sote ni ndugu pia Mungu atupe Moyo wa uvumilivu maana huu ni msiba wetu, nawaomba watu walioanza kulaumu waache huu sio muda wake.
ReplyDeleteda jamani ivi lini tutajifunza izo meli zilikua mbovu ndo maaana hata zipowekwa kwenye ebay hazikupata wateja kwa bei ya $300000 sasa sisi tumekuja kuuziwa mkenge tena kwa bei ya $400000 yaaani inatia hasira sana wenzetu wametufanya dampo la kutupa takataka tuwe wadadisi kabda ya kununua vitu na kama ajali ilitokea kwa upepo mkali kwa nini meli iliruhusiwa kusafiri mamlaka ya hali ya hewa ina fanya kazi gani? wenzetu kama hali ya hewa sio nzuri meli hata ndege haziruhusiwi kusafiri tutakua wazembe mpaka lini jamani ni miezi kumi tu tokea ajali mbaya ya meli itokee sasa hata mwaka haujaisha nyingine tutajifunza lini?????? mungu weka roho za wote waliokufa mahali pema.... amen
ReplyDeletemdau london uk
Tunashukuru sana ndugu michuzi kwa updates za hali halisi ilivyokuwa. Cha muhimu marehemu watarajiwa tujiandae kwa kumpa Yesu maisha ili hata ikikutokea kwa sababu yoyote ile ukapumzike milele mbinguni. Amen
ReplyDeletepoleni sana ndugu wote mliopoteza ndugu na jamaa ktk hilo boti,sasa kama kawaida yetu tunaunda tume
ReplyDeletepoleni sana ndugu na jamaa, roho hina niuma sana, kwa makusudi ya binadamu wameweka pesa mbele kulikoni utu mmejaza watu kama wanyama,kila mwaka basi,upepo gani? viongozi awajali kweli ulizia boti/meli niya nn?utambiwa niyakiongozi.poleni sana mliopotelewa
ReplyDelete