Baadhi ya wadau wa masuala ya blog nchini wakiwa katika picha ya pamoja jioni hii katika hafla fupi iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania kuwatunukia tuzo maalum, zoezi ambalo limeahirishwa kutokana na ajali ya meli iliyotokea mapema leo visiwani Zanzibar. Msemaji wa Vodacom amesema imebidi waahirishe zoezi hili ili kuungana na Watanzania wote katika kuomboleza msiba huu mkubwa kwa taifa na kwamba kampuni hiyo ya simu itajiunga katika juhudi zozote za kujitolea kwa hali na mali katika maombolezo na kuwafariji waliopatwa na maafa pamoja na wafiwa. Taswira za chini ni za wadau hao baada ya kupata habari za ajali hiyo. |
![]() |
Haki Ngowi na Matina Nkurlu na wadau |
well done VODACOM, mumejifunza sana. Ilipozama Spice Islanders muliendelea na sherehe bila ya kujali janga lililotokea. Huu ndio Uungwana, sote ni ndugu na ni wateja wenu.
ReplyDeleteMdau, Zenj
mithupu hiyo fish eye yako tutakoma mwaka huuu
ReplyDeleteHawa mabloga walichaguliwa lini na kwa kigezo kipi?
ReplyDelete