Bank Muamalat Bhd ya Malaysia na Bank of Shi Zui Shan ya China zimesaini memorandum of understanding (MoU) ya ushirikiano kwa ajili ya kuanzisha bank zinazofanya kazi kwa kufuata mfumo wa sheria za kiIslam nchini China.

Mkurugenzi mkuu wa Bank Muamalat Datuk Mohd Redza Shah Abdul Wahid akifafanua uhusiano huo alisema, bank mbili hizo zina matumaini ya kuanzisha benki zinazofuata sheria ya kiIslam ktk kipindi cha miaka miwili inayokuja. Ktk hatua za mwanzo, makundi hayo mawili yatabadilishana utaalam na kutakua na mafunzo maalum yanayohusu bank za kiIslam.

Vitengo karibu 23 vya benki zinazofuata sheria ya kiIslam vitaanzishwa ktk mikoa mbalimbali  nchini Humo ktk kipindi cha mwaka mmoja. Kufuatia kuanzishwa kwa vitengo hivyo, itapatikana nafasi ya kuzijaribu banki hizo na baadae kufungua benki ambayo itakua ni benki kamili ya kiIslam. Ushirikiano huo ni moja kati ya juhudi za makusudi za serikali ya China kuhamasisha bank zinazofuata sheria ya kiislam.

Bank Muaamalat itawafanyia mafunzo ya banki zinazofuata sheria za Kiislam wataalam watano wa Benki ya Shi Zui Shan na gharama zote za mafunzo hayo zitatolewa na Benki Muamalat.  Pamoja na mambo mengine wataalam wa Benki Muamalat watatoa huduma ya ushauri kwa Benki ya Shi Zui Shan ktk kipindi chote cha kukua kwa benki hiyo.

China ina idadi ya waIslam wasiopongua milioni 30 na wengi wao wanaishi Ningxia mji ambao upo Yinchuan a kuna soko kubwa ambalo pande zote mbili zinamategemeo ya kufaidika nalo. 
Kwa maelezo zaidi kwa habari na 
ushahidi wa yaliyoandikwa ingia 
ktk sehemu ya matukio.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2012

    It is very interesting kuona kwamba benki zinazofuata sheria ya kiislam zinakua kwa asilimia karibu 20 kwa mwaka, nadhani huu ni wakati muwafaka wa kujua nini hasa sifa ya benki hizo na ni tofauti gani iliyopo kati yao na benki nyingine.

    ReplyDelete
  2. Che GuevaraJuly 24, 2012

    Ni faida kweli au ? huna interest rate faida unapataje? changa la macho kwani kuna kitu kinafichwa!!

    ReplyDelete
  3. Ktk benki zinazofuata sheria za kiIslam hakuna interest rate badala yake kuna kitu kinaitwa profit rate. Hiyo ni moja kati ya tofauti kubwa zilizopo kati ya benki zinazofuata sheria za kiIslam na zile za riba. Moja kati ya masharti yake ni kwamba riba haitakubalika kwa hali yoyote, mteja atagawana na benki ktk hali mbili hasara na faida na biashara zote zinazofanyika ni lazima ziwe ni halali kwa kwa sheria ya kiislam, kwa mfano huruhusiwi kufanya biashara ktk mambo ya ngono na mengineyo. Kuna tofauti kubwa kati interest rate na profit rate na hili linapatikana kwa kuzifahamu vizuri Islamic modes of finance. Kwa maelezo zaidi tembelea www.ijuebankiyakiislam.blogspot.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...