Kaka issa na wana blog ya jamii wenzangu,
Mie niko na maswali mengi sana sipati jibu kwenye hii nchi yetu na raia wake!Nikwamba kila kona nchi yetu ama serikali zote zinazokuja sijaona hata siku moja inawatetea watanzania hata hawa wabunge tunaosema sasa hivi watakuwa wasemaji wetu lakini ninaona kazi bure kila siku mtanzania anarudishwa chini wageni wananyanyuliwa!Jibu inakuwa nini?nikwamba tuzidi kupata wageni wengi ama vipi?
Wanablog mimi leo jicho langu liko kwenye Mtanzania anavyokandamizwa na ushuru akiwa na kibiashara chake ambacho kitamletea rizki yakula na familia yake na pia jamii inayomzunguka!ama kama atanunua kitu chake nje ili kije kumsaidia na familia yake na pia anaweza kuisadia jamii inayomzunguka vilevile mfano hata kama nikigari anaweza kumchukuwa hata jirani wake akienda kazini!
Swali nikwanini mtanzania akinunua kitu kutoka nje atakilipia tena ushuru kile kitu mara nne na nitofauti na ile tax ambayo huwa tunaisikia ikipangwa bungeni ama ipo kwenye vitabu vyao tax! kitabu kipo na computer ipo lakini huwa havifanyi kazi sbb juma wa TRA ndio ameamua utafanya hivyo.
Tukienda kwa wageni kila siku wao hawalipi kodi hususan wenye mahotel ambayo kila siku unasikia yamebadilishwa majina na mengi ya wageni huwa hayaangaliwi kwenye taxi kwakweli mtanzania akikimbia nakuesema vibaya nchi yake sijui utamlaumu vipi sbb nikweli nyumbani hapati kazi unamwambia hana kisomo lakini atasoma vipi wakati akitafuta pesa yakujisomesha unamkandamiza na ajira hapati lazima atakimbia kila mtanzani na wageni wanachukuwa nchi sbb mrundi akiingia ama mkenya hatoki tena sbb yeye anapata wepesi kwa njia nyingi!
Sasa hivi watu wengi wanakimbia mali zao bandarini sbb kitu alinunua tsh 100 anaambiwa alipe 10,000 vipi huyu mtu atakuja kupata rizki yake na yeye ili aendeshe familia yake?Halafu akishindwa kulipa kiwango ameambiwa mnauza mali yake inakuwa ni nini ni kumdhulumu mali yake ina maana majambazi si raiya tu hata serikali iwekewe hukumu pia ihukumiwe!
Ukiangalia maswala ya muungano na ushuru hapa naona pia bara wanawapa nguvu wapinga muungano sbb wanaona vipi leo zanzibar inabanwa kiuchumi sbb kama mtu anashushia gari yake anaambiwa mil 3 akiivusha anaambiwa alipe tena mil 10 sasa ndio anaambiwa kama usishushie zanzibar bora ushushie hapa dar ili wanzanzibar wasiweze kujiendesha kwakweli tuko na viongozi wanajiita wasomi lakini kifikra hawana usomi sbb kitu kidogo kinaweza kuharibu vitu vingi sana!
Tunaomba viongozi mliopewa nyadhfa muwe na iman na watanzania wenzenu pia!!
Mungu ibariki tanzania!
Mdau salum Abdullah Ahmeid
ahmeidsalum44@hotmail.com
mtoa hoja ndugu yangu nakuunga mkono yote uliyoyasema ni kweli tupu watu wnaakandamizwa kiyama na mafisadi kila mtu anawajua wa nchi hii lakini wanatembea vifuwa wazi kama nchi hii wameresi kutoka kwa wazazi wao.
ReplyDeletena eti hatukusoma walio soma kwa kisomo chao naona wamesomea wizi mtupu mtu akiingia kwenye madaraka ana kamua kiyama mpaka nchi iangamiye.
lakini mungu yupo kila kilicho na mwanzo mwisho wake hakusi, siku mmoja mungu atatuokoa wanyonge because wakuu wetu hawawezi hata siku mmoja.
bora mtu uende majuu ukabebe boksi na baadaye mambo yanajiseti na unasoma na mengi mengi tuuu ukikaa katika nchi yako zuluma daima
wakumbuke tu kwamba siku mmoja watakwenda kumuuna muumba wao ndo watajua siku hiyo, HAKI YA MTU HAELIKI NA IKILIZA KWA DHULMA UTAILIPA UTAKE USITAKE KAMA HAPA HAPA DUNIANI AU KESHO AKHERA.
hapo bandarini dar wakuu wanakula rushwa kiyama, wee acha tu ni kiasi cha kumjua mkuu anakuunganishia line mzigo unatoka na unalipa kidogo watu wanafaidika kwa kuwajua waku wa bandarini tena wamekuwa mabilioneya kwa kunganishiwa line wee achaa tuu , ndo tanzania yetu hii
ReplyDeletekisomo na usomi mwingi uliotapaka na ujanja wingi na wizi wingi umejaa katika kizazi cha kisasa cha TANZANIA YETU
ndo maana hatutaki muungano unatukandamiza sana na ufe ufee, mwanzilishi wao kasema kama hatutaki tusipigwe mabomu lakini tizama leo tunavyotendewa ndani ya mwezi wa ramadhani,kweli hii ni haki?
ReplyDeletewamechoma moto makanisa wenyewe na kutusingizia sisi ili watupige mabomu kwa sababu hatutaki muungano na inshallah bi izni lillahi na mwezi mtukufu huu inshallah muungano utakufa mkitaka msitake kwa kudra ya rahman inshallah
TUACHENI TUPUMUWE NA HATUTA SITA KUITETEA ZANZIBAR YETU ILI IWE HURU KATIKA KOLONI LENU LA BARA, tuweni kuchinjeni kuzulumuni haki zetu tubaneni lakini inshallah kwa nguvu za rahman tutaipata ZANZIBAR YETU.
Si mkoa au kajisehemu hichi hata kama nikadogo tuacheni wenyewe tumeshakocha na nyinyi na zulma zenu.tumeshaamaka hatu rudi nyuma tena mpaka KIELEWEKE INSHALLAH
Waislamu kote nchini tuombeni tutoke katika mazila haya tuwe kitu kimoja inshallah amin.
ramadhan mubarak kwa umma wote wa kiislam popote pale walipo amin.
Mimi ninakuunga mkono kwa yote uliyoyasema ndugu yangu japokuwa kuna watu wasiofikiria wataanza kutwanga bila ya kufikiri.Siyo hayo tu angalia jinsi wageni wanavyonunua ardhi yetu kupitia serikalini bila ya hata wenye ardhi kujua wanakuja kufukuzwa kwenye ardhi yao waliokuwa wanamiliki taribani toka kwa wazee wao, kisa mkubwa kapewa mahel hajali utu wala sheria.Pia angalia makontena yakiwa ni ya wanafunzi waliotoka nje kurudi nyumbani yatafunguliwa na kutereshwa kila kitu na mkwara mwingi kuhusu vitu vya zamani amani yako ni kutoa rushwa ni hii inajulikana na kila mtu hata wabunge wanajua lakini sio kipaumbele chao.Ninamalizia kwa kusema kuna siku hawa viongozi wetu watakaa na kusema ningejua kuwa ingekuwa hivi nisingefanya wakati ndo umeshaharibu.
ReplyDeleteNdugu Salum Abdullah Ahmeid, umejikanyaga kanyaga sana kwenye habari yako hii, ndiyo maana ni vyema kuandika machache na yakaeleweka kuliko hadithi ndefuu isiyokuwa na kichwa wala mbele,of course ,hujakosa washabiki hapo juu,maana binadamu kwa kawaida yetu tunapenda dezo. (1) Ingekuwa rahisi Salum ukatoka kidogo ukaishi angalau mwaka mmoja nchi nyingine,ili ukajifunze taratibu zao za ulipaji kodi na namna serikali zingine zinavyowalea raia wake. Kuna nchi hapa duniani, ukishaamuka asubuhi unaanza kulipa kodi mpaka unaporudi nyumbani kulala,hiyo ni kodi ya kila siku, baadaye mwisho wa mwaka ukifanya incometax yako unatozwa tena ushuru, kama unakajishamba kako ,lazima ukalipia ushuru kila mwaka ,kama unakajumba kako ,lazima ukalipie ushuru kila mwaka, ukikaa kwa mama ntilie kula wali maharage ,lazima mama ntilie akutoze zaidi na hela ya ushuru ambayo yeye ataiwakilisha serikalini,hivyo hivyo ukienda sinema ,ukikaa bar kila chupa moja unayokunywa unalipa ushuru. Sasa unapolialia na kuloloma kwamba unakandamizwa,huo siyo uzalendo hata kidogo. Wewe na familia yako mnatakiwa muwe wazalendo wa kuijenga hii nchi. Kwa ufupi Taifa letu bado hatujalipa kodi inavyositahili,tuko million 40 na upuuzi lakini huenda ni million 10 tu ndiyo wanaolipa kodi. Na siyo kweli kwamba uneleta gari bandarini kisha unailipia zaidi ya thamani ya hiyo gari, common now !! tuweni wakweli tunapochangia hoja za kuleta maendeleo au kusahihisha jambo ili jambo hilo lilete mafanikio kwa jamii,badala ya kupotosha jamii. Zebedayo msema kweli
ReplyDeleteHapa hatumuachi mtu APUMUE tunakaba hadi penalty, unyama unyama tu. Komaeni ndugu zangu Bongo tambarare mlio ughaibuni rudini nyumbani naona sasa mnajikanyanga wenyewe
ReplyDeleteTupo sana huku Zabedayo msema kweli upo hapo?
Mdau UK.
mimi naomba kuuliza mtu wa TRA,mimi nina gari yangu hapa uk nimeitumia nadhani badala ya kuiuza karibu na bure ningependa kuipeleka bora TZ.Bei yake kwa hapa naijua mwenyewe ni gari ya mwaka 2006 mwishoni aina ya Peugeot partner,quick silver multipurpose 2000CC a family car.sasa naomba TRA waniambie thamani ya gari hii kama kweli wanajua bei zake angalau ili wanapochaji ile thamani iwe inaendana na gari yenyewe.Vile vile TRA ningeomba waweke sehemu katika web yao ili wateja waweze kutambua thamani ya vitu vyao kabla ya kuleta nyumbani ili kurahisisha maelewano.
ReplyDeleteUkandamizaji wa bongo mlikuwa hamuuoni miaka yote hiyo? Na bado. Si mnajifanya kukumbatia hilo lichama lao. Mtu akijitokeza kuwapa mwanga mnamuita mdini, mkabila, katoka kaskazini na majina meeeengi yasiyo na tija kwenye maendeleo. Spika kila kukicha anapindisha kanuni ili akandamize wanaotetea wananchi, ninyi hamnyanyui hata mdomo kukemea. Na mimi ningekuwa huko serikalini ningekula kama kawa maana unaowatetea wenyewe hawajaona kama wana tatizo.
ReplyDeleteZebedayo unasema nini unafanya nini? mimi nimemuelewa salum na sijakuelewa wewe. unalalamika story ya salum ndefu wewe ndio umeuwa kabisa.mpaka nimeishia njiani simalizi.au unafanya kazi tra unatetea?zulma? Wewe sio zebedayo wewe zebe!!!!!!
ReplyDeleteDuuuu bongo noma sirudi. ushuru mara nne nne
ReplyDeleteZebedayo umechemsha nchi unalipishwa kodi zaidi ya mara moja.ni bongo tu.wacha kodi rushwa je?.
ReplyDeleteAgain Zebedayo mchukia wanaoishi ughaibuni katoa hoja zake zile zile za kichuki na zisizokuwa OBJECTIVE.ingawa kama kawaida yake kajifanya anatoa hoja za jinsi nchi nyingine zinavyokusanya sana kodi!!!!
ReplyDeleteNikirudi kwa mwanzilishi wa mada, hoja zake ni za kimsingi ingawa natofautiana na kichwa cha mada yake ambacho kingependeza kama kingekuwa "Kwa nini VIONGOZI WA TANZANIA"wanakandamiza wananchi wake.
Namalizia na hoja ya mdau wa mwisho ni kweli ingependeza kama mtu angekuwa anajua in advance kiwango gani cha ushuru atatakiwa alipe kwa aina fulani ya gari LAKINI kama watu wakijua WEZI WA BANDARINI WATAKULA WAPI?
Wadau hebu toeni maoni mafupi. Mnatuchosha kusoma mnaporudiarudia. Kama mnazo mada ndefu, ni vizuri mkaziweka front page ili zitolewe maoni.
ReplyDeletePAMOJA NA KUJIKANGANGANYA MTOA MADA UNATAKIWA KUJUA WATU WA KAWAIDA BARA HAWANA HABARI KABISA NA HUO MUUNGANO,NA NINA UHAKIKA KURA ZIKIPIGWA WENGI WATASEMA UFE,WATU WALIOENDA SHULE WA BARA WATASEMA HAUNA MAANA UNAINGIZA BARA GHARAMA TU,ZANZIBAR HATA WILAYA YA BAGAMOYO NI KUBWA LAKINI INA WABUNGE KAMA SIKOSEI 29 WAKATI BAGAMOYO NI WAWILI TU,DAR ES SALAAM INA WABUNGE 7 WATU MILION 5 ZANZIBAR WATU 997,000 WABUNGE WOTE HAO 29 WA NINI?? NA UFE HATUUTAKI BARA TUBAKI NA JINA HILO HILO WENYEWE SI WANAITWA ZANZIBAR???? SASA TATIZO NI NINI???
ReplyDeleteWatanzania wanajitahidi kweli kweli kujiletea maendeleo.
ReplyDeleteMapambano dhidi ya umaskini yanafanywa na wananchi wenyewe lakini watawala wanakatisha tamaa na kuwavunja moyo watu.
Matokeo yake nchi imejaa vilio.
Sasa mnachukua hatua gani baada ya kugundua mnakandamizwa? Kulalamika tu huku kwenye vyombo vya habari haitoshi. Mnatakiwa mfanye maamuzi magumu yatakayoleta maendeleo na si kulalamika.
ReplyDeleteMsipobanwa ninyi mkalipa kodi mnafikiri serikali itajiendeshaje? Chapeni kazi acheni kulalamika bana. Nafikiri ni wakati muafaka sasa na mimi kuingia kwenye siasa niondokane na umasikini. Ukiwa huko maslahi yote mazuri yanaelekezwa kwako. Ingieni kwenye siasa muache kulalamika. Njooni mjiunge na chama chenye muelekeo (CCM). Hapo mtapata kila kitu. Hao wengine wanatapatapa tu na hakuna kitachofurukuta. Bado nguvu tunayo. Tunajiamini.
ReplyDeletewewe Zebedayo huyajui maisha ya Ulaya,huku tunalipa kodi nyingi na matumizi yake tunayaona, huduma za Afya ,elemu,maendeleo chakula , makazi n.k ,
ReplyDeletekwa nchi yenye kila kitu kukaa kuwakumbatia wageni ni upungufu wa Fikra ,Tuwapeni uhuru Zanzibari na tutaona watavyo tuacha mbali maana wao wana maadili ya kiubinadamu, VIONGOZI WANA KASHFA NZITO ILA BADO WANANG´ANG´ANIA MADARAKA ; NCHI IMEJAA dhuruma ,rushwa ,uongo, utapeli na maneno maneno tu yamekithiri, nasasa tunabadilishwa na tunalazimishwa tuone kama hii ni hali ya kawaida.Nasasa tunapelekwa kidikta kama dokta Ulimboka ameteswa na kunyanyaswa vile kwa kuwasilisha maslahi ya madaktari je niaje hawa viongozi wezi na bado wanadunda tu mitaani.
WOTE SI WAFAHAMIKA????:
mdau. Raia.
Zubedayo mimi naona wewe ndio hujasoma na kufahamu tatizo sio kodi elewa tatizo lipo katika ulipaji leo unaambiwa unalipa hivi kesho unakutana na mwengine anakwambia lipa hivi nafikiri nimekuwekea kwamba hakiangaliwi kitabu cha ushuru kilichoandikwa wala computer juma wa TRA ndio anakuamulia!Na mimi niko nje kwa Taarifa yako ninatetea wanyonge wauza maandazi wanalipishwa kodi halafu kodi hazijulikani wapi zinakwenda!mimi nahisi wewe ndio si mtanzania sbb hukufahamu kiswahili nilichoandika nyinyi ndio waganda wahamiaji mnaotaka watanzania wakimbie muchukue nchi!
ReplyDeleteNapenda niamini kuwa kama mtu anatozwa kodi asilimia 1,400 basi labda wale wanaodanganya bei na mwaka wa gari. Kama bei na mwaka havina dosari sidhani kama utatozwa fedha nyingi kiasi hicho. Hata hivyo naungana na waliotangulia kuwa TRA waweke wazi mahesabu ya kodi ya vitu.Siyo kusubiri mtu kaleta mzigo halafu wanaanza kubambika kodi nyingi nyingi tu. Kupandisha kodi bila mpangilio kunatengeneza mianya ya rushwa na inawezekana watu wa TRA wanafanya hivyo ili mhusika azungumze lugha inayoeleweka kwao (atoe rushwa). Utamaduni huu umekomaa si bandarini tu. Hii ni hatari tunatengeneza bomu.
ReplyDeleteNaona hoja ipo kweli,lakini mtoa mada na wachangiaji wengi hawajajiandaa.Wanatokatoka nje ya hoja au hawaeleweki wataka kusema nini.Ndo maana mwambiwa hamjasoma nyie.
ReplyDeleteKwenye mada jazba ya nini?Na mnachanganya mambo hadi kinachotakiwa kuzungumzwa kabisa haikieleweki.
Mnaongelea rushwa,au badhirifu,au ufisadi,au kodi kubwa katika kutoa mizigo,au muungano?
Mwisho mwaonekana mmetumwa tu,na mawazo ni ya kifisadi zaidi ovyoooooo!
Pangeni mawazo na sema kimoja unachotaka kutuambia tuwaeleweni.
Unajua sheria, taratibu na kanuni za karibu kila sector hapa Tanzania zimefichwa kwa makusudi Ili kila unapotaka iwe kuingiza gari inchini, kununua kiwanja, kujenga nyumba au kuanzisha biashara uwe ni Mtu wa kuomba kudra za watawala. Yaani unafanywa kila utakacho uonekane umesaidiwa tu na watawala.
ReplyDeleteHuu ni utumwa.
Ndio maana wakenya huwa wanashangaa ukienda dukani "unaomba" unachokitaka kununua halafu unalipa.
"usipoomba" unaonekana wewe ni jeuri na unakomeshwa kwa dhulma fulani au kunyimwa tu haki yako.
UZURI WA MAJUU KILA KITU KIPO WAZI. UNATIA GARI MAFUTA, RISITI INAONYESHA MAFUTA £ NGAPI NA KODI £ NGAPI.
ReplyDeleteUNANUNUA VITU DUKANI, RISITI INAONYESHA MUUZAJI ANAKULA NGAPI NA VAT WANALAMBA NGAPI.
UNALETA MZIGO TOKA NJE YA UK HASA EUROPE HM REVENUE WAMEFAFANUA KABISA KWENYE MTANDAO KODI YA GHARAMA YA MZIGO/BIDHAA YAKO UTALIPIA KODI KIASI GANI.
HAKUNA LONGOLONGO LA KUMSUBIRI SHAMTE, JONGO, KIMWERI, AJE ND'O AKUPANGIE KODI.
HUYO ZEBE WALA MI SIMWELEWI. KAMA UPO UK UNAUNGAJE MKONO KITU USICHOJUA?
TATIZO NCHI IMEJAA WIZI SIYO RUSHWA TENA. NI WIZIIIIIII MPAKA KWENYE MATE. WATU THA NA TRA, MSUKUMA KOKOTENI, BODABODA, DALADALA, MUUZA MANDAZI YAANI USIPOANGALIWA UTAIBIWA NA HATA MWANAO WA KUMZAA MWENYEWE.
MI MWANANGU YUPO TRA ALITAKA KUNITIA NDANI KARIBU MILIONI 3 NZIMA ETI AKIDAI NDIYO KODI HALISI. WIZIIIIIII WAKUBWA NYIEEEEEEEEE NDO MAANA KILA MTU SIKU HIZI ANAJIFANYA MSANII. MMESOMEA WAPI FANI HII JAMANI?
hii nchi imefikia patamu kuna siku kile kitu kinacholia mbaaaa!! mtu chini watakiona cha kawaida(survival of the fittest na ngoja tusubiri bila shaka siyo mbali na ikiwa mbali sana haitazidi 2015 natanguliza salaam((:
ReplyDeleteMdau mwenye Peugeot 2006....
ReplyDeleteNa kwa ufahamu wa wengine.
Sheria ipo kukuruhusu kuleta gari 1 kwa matumizi binafsi bila kulipa ushuru kabisa.
Labda kama Bunge la juzi limebadilidha sheria katika malipo.
Vigezo ni hivi.....
1. Uwe raia wa Tanzania aliyeishi kihalali nje zaidi ya mwaka mmoja.
2. Gari liwe lilisajiliwa huko ughaibuni kwa zaidi ya mwaka mmoja kwa jina lako na matumizi yako binafsi.
3. Gari isiwe zaidi ya miaka kumi.
Ukitimiza hayo yote. Unaruhusiwa kuleta gari moja kwa kila familia (pamoja na vifaa vyote vya nyumbani, bila ushuru)
Gharama ya kulipia TRA ni Tsh 350,000 tu! kwa gari ya aina yeyote ile.
Utakutana na gharama za huduma za bandarini tu.
Nimeshatumia huduma hii, nimeleta 40ft container ilyokuwa na gari pamoja na full furniture pamoja na vifaa vyote vya kisasa vya nyumbani mpaka split system airconditoners...... Bila kuhonga wala kujuwana wala kubembelezana..... duty free kabisa. Kama nilivyosema gharama za TRA zilikuwa laki tatu na nusu tu!!!! 300,000 ya kusajili, 45,000 za number plate halafu kulikuwa na shs 10,000 za TBS.
Tatizo wadau wengi mlozamia ughaibuni elimu ndogo na ufahamu wa vitu vina endeshwaje hamna. Kilichowapeleka na sasa kinachowarudisha ni ki jazba jazba tu... Malalamiko meeeengi na kujuwa kudogo!!!
Jielemisheni kwanza jamani.
Kuna wanao ongelea muungano, sijui upuuzi gani ..... jamani jielemisheni kwanza kabla hamja kurupuka na kuropoka bure!
Hivi wewe unayejiita Zebedayo msema kweli ulishawahi kuishi ulaya hata kwa mwenzi mmoja tu ukaona huduma za jamii zinavyopewa kipaumbele? Unalipa kodi kibwa ulaya lakini haikuumi maana ukiumwa tu ukipiga 999 dakika mbili ambulance imefika. Njoo kwenye barabara lami mpaka vijijini, umeme 24/7, maji, huduma za usafiri, barua unadondoshewa mlangoni, takataka unaweka nje zinachukuliwa, na bado unapewa uhuru wa kutoa maoni yako kama huridhiki na huduma inayotolewa na serikali yako ya mtaa. Unaona why you paying tax, sio kuwafaidisha wajanja walioko serikalini.
ReplyDeleteTatizo watanzania mnapenda sana kujifanya mnajua kuwaponda wenzenu wanaotoa maoni, swala sio kulipa kodi tu, tatizo hatuoni huduma zikitolewa kulingana na kodi zinazolipwa na wananchi. Nikufahamishe wewe mjinga Zebedayo msema kweli, nchi za ulaya raia wake wakikosa kazi wanapata jobseeker allowance ya kuwasaidia kuishi hadi watakapopata kazi, hii ndo maana ya kulipa kodi, nahisi wewe ni ndugu wa hao mafisadi walioko serikali ndo maana unaongea pumba, you don't know anything.
aha !! kumbe Salumu uko nje , wewe baki huko huko,tutakapomaliza kuijenga nchi yetu na wewe wakati huo ushafikisha miaka 67,basi njoo,tutakupokea tu hatuna noma,utakula na utalala bureee. Sisi kodi zote tutazilipa zikiwemo na za kwako. Kama ni rushwa , duniani kote zimejaa-acha kutupotosha hapa.Zebedayo msema kweli
ReplyDeleteNamuonga mkono haya maneno kweli tanzania hakuna upendo kwa wananchi wao mimi ninauchungu na hao watu wanaitwa viongozi hawana imani na wananchi wao, wao roho binafsi roho zao walizo nazo wana wivu wa maisha kwa wananchi ukinuna chochote huku nje kosa bora ndugu zako wafe kuliko kuwasaidia chochote cha maendeleo tanzania ni nchi viongozi wanawivu sana wa wananchi wao. Leo tuma trekta hilo halina ushuru lakini ukifikisha wataka pesa ya ushuru wanakupa hesabu yao TRA,mimi ninauliza hiyo TRA nini aina maana gani kuweka viwango vingi vya pesa kwa manufaa yao sio ya wananchi?nimechoka na utanzania hiyo tanzania sio ya viongozi ndio wasema na kuamua vyao bila mwananchi kumfikiria, kujaza matumbo kwa pesa za wananchi nchi imeoza.Sasa hivi viongozi wote wa nchi hiyo Tanzania wanaimaliza tanzania wao wanafikiri wanchi hawajui? wanachi wanashindwa waende wapi kuripoti. imezidi kodi kwa mtanzania ni mkibizi ndani ya nchi yake hana la kufanya sasa nina ni kabaila katika nchi hiyo uhuru 50 watoto washule wanakalia makaratasi na hamna vyoo pesa hizo tunazota za ushuru wapi zinaenda? Faida ya nchi inategemea tu kwa wawekezaji sio kwa mtanzania? Nchi bongo ni bomu hata miaka1000 haitopata maendeleo kabisa kwa kuwabana wananchi, mfano China India ni wananchi walikuwa nje ya nchi zao ndio wanaoleta maendeleo sio serkali> Tanzania inwapa wananchi wako nje woga wasirudi na wasiendeleze nchi yao hiyo ni Radhi ya mungu. Watu wafaidi ni wahindi na waarabu wanaleta vitu vyao kwa mali kauli na kupitisha.Bora mungu arudi kusaidia wananchi wa Tanzania. Roho inaniuma sana. The time of primitive Tanzania citizens is finished. The tanzania leader their not educate if their educate they can't do for their peoples.
ReplyDeleteAcheni kelele zenu , njooni CCM kila kitu mtakipata.
ReplyDeleteWeee zebe sio salumu / salum
ReplyDeleteHeeer juma swedi umeandika gazeti!!!!
ReplyDeleteSasa
ReplyDeletewahindi na waarabu unawaingizia nini
sisi tunasema watanzania wacha wivu wewe
we mwenyewe labda unafanya kazi kwa muhindi opsss samahani mtanzania mwenye asili ya kihindi
.ushaelewa eeeeeee
Weee zebe nchi kashindwa mnaemuita baba wa taifa utaweza wewe?. list yangu 1 umeme 2 maji 3 rushwa 4 ajali barabarani 5 ajali baharini 6 ujambazi na wizi 7 ajira 8 elimu na mashule pamoja na vifaa 9 huduma za raia kama vile ambulance,fire,nk. na 10 wajinga kama wewe. kama kuna msamaria mwingine aongeze tu list maana mengi sikumbuki yote
ReplyDeleteZebedayo wewe nimganda kama hujui kutamka salum basi wewe si mtanzania jikate kabla hatujashuka!
ReplyDeletewadau,
ReplyDeletenadhani tuache jaziba, na huyo aliyeitetea TRA nadhani amepatia kabisa, sheria zipo kuleta gari kwa matumizi ya familia. Mimi niko nje na niliagiza mawili na yakatolewa bila kuonga tukalipa (kupita ajenti) kodi kama tovuti ya www.gariyangu.com walivyotoa mwongozo.
sasa wapo wadau hap juu mnaosema TRA iweke kdi zake bayana, nilitoa mada majuzi nikielza jinsi kodi hizo ziko bayana na wameweka pia claculatoa ya import costs kwa gari na size ya injini na mwaka.
temebela tovuit hii:
www.tra.go.tz. Hapa sio tu utakua vielelezo, lakinipia utakua sheri za kodi zilizopo kwa sasa, simu za kupiga kulalamika, simu za mameneja wa TRA wa miko nk..sasa sio kweli kwamba jamaa wanakubandikia kama unajua haki zako.
wameweka pia kodi ya mtu binafsi mapata..hadi 750,000 na kipata zaidi ya hapo.
wamekweka pia kodi za wafanya biashara kulingana na mapata.
Tatzio kubwa ninalo liona na TRA ambalo nadhani ni uonevu lakini pia linatokana ana tabia ya uongo kwetu sisi tunaoagiza vitu toka nje au kufanya biashara, ni TRA kukata bei mtu aliyonunulia bidhaa ( iwe gari, mafuta, trekata) na wao kuweka bei yao, baada wakaitumia hiyo kukuhesabia kodi.
kuna mdau aliyesema kuwa aliwaonyesha hata tovuti ya wale alikonunua bidhaa ili TRA wadhibiti bei zilizowekwa pale lakini bado waoa wakagangna.
sasa sheri ya kuwalazimisha TAR kukubali bei iliyothibitika ya manunuzi itakuwa nzuir. na sheria hiyo kumpa haki mlalalmikaji kudai pesa yake kama TRA wamelazimisha, kwani kama mnunuzi wa hicho kitu, utataka ukitoe isiwepo storage charges.
sasa sheria(vile sasa tunatengenza katiba mpya) imuwezeshae mwanachi kwamba kam akuna utata(disputes) basi gharama za storage ziwe waved mpaka pale hiyo itakapokuwa imekubalika. TRA wasiburuze watu kwa uplift bei za bidhaa bila ushahidi wa kudanganya kwa mlengwa. na zaidi kama mlengwa anaonyesha ushahid bei aliyonunua ni ile, basi mama TAR itoka counter evidence au wakubali..hiyo sheria iwabane TAR na walipa kodi..basi tuwaslishe maoni yetu kwa hiyo tume ya katiba..huu ni uzurumaji mkubwa, naamini hivyo, labda Zebedayo ana la kuongeza!!