Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akijumuika kuomba dua iliyoombwa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba (katikati) baada ya kuwasili kwa ajili ya kufungua rasmi semina elekezi ya Masheikh wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Veta mjini Dodoma leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya kufungua rasmi semina elekezi ya Masheikh wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Veta mjini Dodoma leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba, baada ya kufungua rasmi semina elekezi ya Masheikh wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Veta mjini Dodoma leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini na viongozi wa Jumuiya za Kiislamu wakati akiondoka, baada ya kufungua rasmi semina elekezi ya Masheikh wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Veta mjini Dodoma leo
Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya za Kiislamu na waumini wa Dini hiyo, waliohudhuria semina elekezi ya Masheikh wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) iliyofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Veta mjini Dodoma leo, Julai 15, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal amefungua semina elekezi kwa Masheikh wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA inayofanyika katika ukumbi wa VETA mjini Dodoma.

Akizungumza katika hafla hiyo Makamu wa Rais aliwataka viongozi wa dini kuhakikisha wanawahimiza waumini wao kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti 26 mwaka huu na kusisitiza kuwa msingi wa zoezi hilo ni Utanzania na kamwe halisimami katika misingi ya rangi, dini, kabila ama eneo analotoka mtu.
Alisema sensa ya watu makazi inatoa fursa kwa serikali kujua idadi kamili ya wananchi wake na pia kupata takwimu zingine muhimu zitakazosaidia kuratibu mipango ya maendeleo katika nchi.
“Hili ni zoezi linalomhusu kila Mtanzania kwa kuwa linalenga kurahisisha mipango ya maendeleo kwa Watanzania,” alisema Makamu wa Rais na kusisitiza “Msingi wa zoezi hili ni UTANZANIA na kamwe halisimami katika misingi ya rangi, dini, kabila ama eneo analotoka mtu,”.
Dkt. Bilal aliwaambia Masheikh hao kuwa serikali imejipanga vizuri kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kama ilivyopangwa. Alibainisha kuwa hivi sasa maandalizi yote yamekamilika, kinachosubiriwa ni siku hiyo ya Watanzania kuhesabiwa.
“Katika dini yetu tunazo hadithi mbalimbali zinazohusu zoezi hili la sensa.
Naamini ninyi Masheikh mnazo hadithi nyingi za mifano kuhusu suala hili nyakati za Mtume (S.A.W). Ni vema sasa mkafunua vitabu vyenu na kuwapa waumini wenu nukuu mbalimbali zinazowiana ili waelewe vema umuhimu wa sensa kwa maendeleo ya Taifa na kwa maendeleo ya jamii yetu,” alisisitiza.
Makamu wa Rais alitumia fursa hiyo kuwakumbusha Waislamu umuhimu wa kujifunza namna bora ya kutumia benki zisizotoza riba za Kiislamu na kutumia benki hizo vizuri kwa kujipatia mikopo itakayowasaidia kuanzisha ya miradi ya kuwaondolea umaskini.
Aliwasisitiza wanazuoni watakaotoa mada hiyo kwenye semina hiyo kuhakikisha wanawaelimisha vyema washiriki hao kuhusu matumizi bora ya mikopo ya benki zisizo na riba katika kujikomboa na umasikini.
Alisitiza pia suala la utii wa sheria za nchi bila shuruti na uboreshaji elimu kwa kuanzisha shule ili kuwawezesha vijana kupata elimu na hatimaye waweze kumudu kuishi vema katika dunia ya sasa.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dodoma
Julai 15, 2012
Tafadhari ninaomba kuelimishwa hawa Ndugu zetu waislam, je hizi kofia wanazovaa zina wadhifa tofauti au ni fashion tutu, meet wangu ameshindwa kunipa jibe.
ReplyDeleteAnon. wa mwanzo kabisa uliyetaka kuelimishwa. Hizo kofia wavaazo WAISLAM. La hasha, hazina wadhifa tofauti na wala siyo fashion, bali ni jumla ya kulikamilisha vazi zima la KIISLAM kwa upande wa wanaume. Ispokuwa tu, bei zake ndio zinaweza kutofautiana kutegemea na aina ya maua, uzi uliyotumika (rangi au quality ya uzi huo) ushonwaji wake, uzuri pamoja na mpangilio mzima wa maua yake kwa jumla.
ReplyDeleteIla niliwahi kuskia kwa wenzetu Wasomali huwa zinatofauti, ilai sina hakika kama ni kweli au laa! Lakini kwa upande wetu sidhanii hilo, ni upendo wa mtu tu binafsi na uwezo wake.
mdau wa pili usingemjibu jamaa huyu wa mwanzo yeye hataki kuelimishwa ila anataka kukebei/kusanif dini yetu nakuambia waALLAHI Si muulizaji huyu
ReplyDelete