Baadhi ya Wananchi waliozitambua maiti zao katika Viwanja vya Maisara wakisaidiwa na Askari kutokana na Huzuni kubwa waliokuwanazo.kwa kuzama kwa Meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.Hadi mchana huu Maiti zilizopatikana ni 39 kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Zanzibar na bado waokoaji wanaendelea na zoezi hilo katika eneo la Tukio.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika Foleni ili kwenda kuzitambua Maiti zao katika Viwanja vya Maisara kutokana na kuzama kwa Meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.Hadi mchana huu Maiti zilizopatikana ni 39 kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Zanzibar na bado waokoaji wanaendelea na zoezi hilo katika eneo la Tukio.
Baadhi ya Wageni kutoka Nchi mbalimbali wakiwa katika Viwanja vya Maisara ili kujuwa Ndugu zao na kuangalia taratibu zinazofanyika viwanjani hapo kutokana na Kuzama kwa meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.Hadi mchana huu Maiti zilizopatikana ni 39 kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Zanzibar na bado waokoaji wanaendelea na zoezi hilo katika eneo la Tukio.
Wananchi mbalimbali wakizitambua Maiti zao zilizopatikana katika Ajali ya Meli ya skagit iliozama hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.Hadi mchana huu Maiti zilizopatikana ni 39 kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Zanzibar na bado waokoaji wanaendelea na zoezi hilo katika eneo la Tukio.
Baadhi ya Maiti zilizopatikana katika Ajali ya Meli ya Skagit ilizama zikiteremshwa katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar ili kutambuliwa na Jamaa zao.Hadi mchana huu Maiti zilizopatikana ni 39 kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Zanzibar na bado waokoaji wanaendelea na zoezi hilo katika eneo la Tukio.
Madaktari wakiandika Orodha ya Maiti zinazoletwa hapo katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar Baada ya kupatikana kutoka katika Meli ya Skagit iliozama hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.Hadi mchana huu Maiti zilizopatikana ni 39 kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Zanzibar na bado waokoaji wanaendelea na zoezi hilo katika eneo la Tukio.
Wahusika wa Matayarisho ya Mazishi ya watu waliokuwa bado hawajatambuliwa na Jamaa zao ili kuzikwa kiserikali wakiwa katika kazi ya kutayarisha Sanda hapo katika Viwanja vya Maisara Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi wakiwa wamekusanyika katika Viwanja vya Maisara ili kuweza kupata taarifa ya Ndugu zao waliokuwa katika Meli ya Skagit ambayo imepata Ajali ya Kuzama katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali wakiwa katika Viwanja vya Maisara ili kuweza kupata Taarifa mbalimbali za kuletwa kwa Maiti ambazo zimepatikana katika ajali ya Meli ya skagit iliozama hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2012

    inna lillahi wainna ilayhi raajiuun. Hawa ndio hatma yao. Ajali ni sababu tu. Mungu kawaandikia wazanzibari tangu mwaka wataondoka katika vyombo vyao wanavyosafiria.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2012

    Poleni wafiwa, tupo pamoja nanyi.

    (1) Hivi serikali yetu kwa nini babo ina mambo ya kizamani namna hii. Yaani kuliko watu kukaa kwenye misululu mirefu hivyo, NI BORA WANGEZIPIGA PICHA MAITI HIZO NA KURUSHA KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA MITANDAO ILI KURAHISISHA ZOEZI LA KUWATAMBUA.

    (2) Kwa nini wanaharakisha KUZIKA MIILI HIYO YA WAPENDWA WETU HALI BADO WENGINE TUPO NJIANI TUKIJA HUKO KUWATAMBUA. KWA MAITI ZENYEWE MBONI CHACHE KWANI HAKUNA VYUMBA YA KUHIFADHI?

    (3) TUNAOMBA VYOMBO HUSIKA KUFANYA HIVYO HARAKA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 19, 2012

    Kila nikizipitia hiz picha, hususan picha za hao watoto wanne kwa kweli machozi yananibubujika, utafikiri wamelala vile, how terrified they must have been,yote kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa, wapumzike kwa Amani, milele.
    Dr Gangwe Bitozi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 19, 2012

    Rekebisha kidogo maelezo ndugu mtoa taarifa siyo "waliozitambua maiti zao bali ni walizitambua maiti za ndugu/jamaa/rafiki ama watoto wao".
    INASIKITISHA NA KUHUDHUNISHA SANA. mUNGU AWAREHEMU WALIOTUTOKA NA ATUJAZA MOYO WA UVUMILIVU KTK KIPINDI HIKI KIGUMU.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 19, 2012

    Ndiyo maana ikaitwa blog ya jamii na iko juu.Mnatusikiliza sana sisi washika dau.Asante sana kwa kuziondoa hizo picha za watoto,zilikuwa zinatuliza sana.Mungu awarehemu wote hususan hao watoto..

    David V.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 19, 2012

    Sheria zinatakiwa ziwe kali kuhusu usalama wa watu wanotumia vyombo vya usafiri. Meli tatu zimezama bado hakuna somo Wazanzibari tulilojifunza. Zaidi ya UAMSHO hakuna kinachofanywa.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 20, 2012

    SAWA NI AJALI AMBAYO HUPANGWA NA MUNGU:

    PIA NI SOMO TOSHA ILI TUJIREKEBISHE KWA MAMBO MAWILI HAYA,

    1.TUACHE KUENDESHA MAMBO BILA KUJALI TARATIBU,KANUNI,VIGEZO NA MASHARITI,,,MFANO USAJILI WA CHOMBO HICHO INASEMEKANA DALILI ZA RUSHWA NI VILE CHOMBO HAKIKUWA KINAFAA KWA MATUMIZI YA SAFARI NDEFU.

    2.MAMLAKA YA HALI YA HEWA NA MWENENDO WA MABADILIKO YA BAHARI INATAKIWA IWE INAZUIA VYOMBO KUSAFIRI AU KUHAKIKISHA HATUA ZA KUSITISHA USAFIRI ZINAFIKIWA ENDAPO TAHADHARI ITATOLEWA KUHUSU HALI YA HEWA ISIYO ELEWEKA AU KUFAA KWA USAFIRI,,,INASEMEKENA MAMLAKA ILITOA TAARIFA ZIKAPUUZWA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...