Habari. Naitwa Elvan Limwagu wa www.limwagu.blogspot.com
Kutokana na tukio la vifo vya watu waliokunywa Pombe kali ya Gongo hivi karibuni, mimi binafsi napenda kuwaletea picha chache tu kuonyesha namna pombe hiyo inavyoandaliwa.
Kule kwetu Pombe hii huitwa kwa jina la NIPA wengine kwa kuipendezesha wakalirefusha jina hilo kuwa "New Internationa Pure Alcohol" na kwa hakika viongozi wengi waliotokana na makabila ya Wayao na Wamakuwa walisoma kutokana na ADA ya mapato ya pombe hiyo kali. Itakumbukwa kuwa kwa mara ya kwanza katika kampeni za uchaguzi za mwaka 1995 Mgombea moja alidiriki kuwaahidi wananchi wa makabila hayo kuwa wakimchagua ataruhusu pombe hiyo na kuiwezesha iwe inaandaliwa kitaalamu, ingawa kura hazikutosha.
Pombe ya Gongo au Nipa kule kwetu hutokana na Mabibo (tunda la mkorosho) ambalo hukaushwa juani na hatimaye kuweza kuhifadhiwa hata kwa zaidi ya miezi sita. Mabibo unayoyasikia yakishakauka hubadilika jina na kuitwa KOCHOKO ambazo inapofika wakati wake (ni baada ya msimu wa mauzo ya korosho kupita) hupatikana kwa adimu sana na waandaaji wake huitafuta hata kwa maili zaidi ya 60.
Kochoko hizo baada ya kuchambuliwa na kuondoa takataka hulowekwa kwa wiki nzima ndani ya pipa au mtungi (chungu kikubwa) na maji yake yakipata ladha ya juisi inayoweza kulevya (staili ya mnazi au ulanzi), ndipo huwa tayari kwa kupikwa kama unavyoona hizo picha.
Vifaa vilivyosababisha jungu hilo ni: Mtungi, mtutu uliounganishwa na ngalawa, chungu kidogo cha kufunika mtungi kwa ajili ya kuzua mvuke usitoke nje, udongo wa mfinyanzi kwa ajili ya kusiliba maunganisho ya mtungi na chungu na tundu la mtutu kutolea mvuke hadi kwenye chupa.
Mvuke unaotoka hupozwa ndani ya mtutu kwa maji baridi na kuwa maji yanayoitwa NIPA (Gongo). Ile Pure huitwa IPACHO ambayo ni Spiriti kabisa kwa kuwa inawaka wanapoijaribia wenyewe, ile ya mwisho inaitwa ALEKA ambayo kwa wanaojifunza huweza kuitumia. Ili kupunguza makali ya IPACHO huwa inachanganywa na ALEKA, hata hapo Konyagi ni cha mtoto.
KWA TAARIFA YAKO NI KOCHOKO NI MALI GHAFI ADIMU MASASI.
IPACHO kwa kihaya inaitwa mbandule. Na wahaya wanatumia Pipa kubwa kutenegenza sio kibuyu. Sasa hiyo IPACHO imeshaua watu wengi, an kweli inawaka.
ReplyDeleteInafurahisha kuona ujuzi ni ule ule, japo wahaya wanatumia juisi ya ndizi kali, laki kusiliba, mrija, kupoza nk, ni teknolojia mambayoinatumia.
halafu kuhus kipato, kweli Gongo linaleta kipato kusaidia jamii nyingi, na wanaotumikia taifa leo wamesoma kwa mapata ya Gongo..sasa kualarishwa sijui, maana hata huku Ulaya, bado kuna watu wanatengeneza Gongo na ni kinyeme cha sheria. Nadhani mwaka jana Uingereza watu sita walikufa baada ya pipa kulipuka. huko Bukoba hilo Pipa likilipuka huwa linapaa hewa mithili ya misile..ni hatari..na athari zaidi ni kiafya..nasiki inaunguza matumbo..sasa huyo mgomeb aliyeahidi kuipa nafasi kisheria naweza kukubaliana naye, kwani maana yake ni kuwa watu watumia vyumba vya kisasa, usalama uwekwe, usafi nk na gongo itoke, maana kama ulivyosema, Tecla, Konyagi, Vodka, John walkers zote ni Gongo za kileo, kizungu..kwani nini za kiafrika iwe kero?
Oluburi
Kumbe hii "distillation" tunayofundishwa ktk somo la Kemia mashuleni asili yake kwa Wayao na Wamakuwa?
ReplyDeleteAA wapi. Unadhani kwa nini ikaitwa pombe ya Moshi. Tumenyamaza tuu bwashe hatutaki kesi.
ReplyDelete