Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa-Itikadi na Uenezi, Mh. Nape Nnauye akisalimiana na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya ya Mpanda, mkoa wa Katavi
 Maandamano kuelekea kwenye uwanja wa Kashaulili wilaya ya Mpanda.
 Mh.Nape akihutubia wananchi wa Mpanda waliofurika kwenye  uwanja wa Kashaulili,ambapo alikemea vikali vitendo vya vyama vingine kuendekeza vurugu badala ya siasa.
 Mh.Mwigulu Mchemba akieleza wananchi masuala muhimu ya kiuchumi na kwa nini kunakuwa na mfumuko wa bei,pia alitumia fursa hiyo kukemea mauaji yalotokea kwenye jimbo lake ambapo kijana mmoja kiongozi wa chama aliuawa na wanachama wa chama cha upinzani

 Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi,Mh. Charles Tizeba akizungumzia masuala ya kuimarisha reli na pia  utunzaji wa treni zetu ikiwa suala zima la usafi, pia aliwaambia wananchi serikali imeagiza mabehewa ya abiria na ya mizigo.
 Naibu Waziri Kilimo na chakula,Mh. Adam  Malima akihutubia wananchi wa mkoa wa Katavi, juu ya masuala mabali mbali ambayo yametekelezeka likiwemo suala la umeme na pia aliwaambia wakulima kwamba serikali imeandaa utaratibu mzuri wa vocha za kilimo ambazo utatangazwa hivi karibuni.
Naibu Waziri TAMISEMI,Mh.Aggrey Mwanri akihutubia wananchi wa Mpanda mkoani Katavi,ambapo aliwasihi kutokubali kudanganywa danganywa na pia aliwaambia wananchi serikali hii isingependa kuona wananchi wa chini akionewa, hivyo alitoa tamko la kutowalipisha ushuru wakina mama wafanya biashara ndogo ndogo mfano vitumbua na chapati.
Picha zote na mdau Adam Mzee

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2012

    mawazari rudini bungeni, sasa sio kutangaza sera za chama fanyenyi kwa vitendo ili wenyewe waamue na sio kuwaaminisha maneno matupu, mtu wa vitendo anajitangaza kwa vitendo vyake na sio simple politics.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...