Uncle Issa Nahitaji Msaada kutoka kwa wadau..
nilipokua nikisafiri wakati niko kwenye transit hotel Cairo.. niipata nafasi ya kuogelea sasa maji yakaingia masikioni nikajaribu kurukaruka hayakutoka nikapanda ndege kuendelea na safari yangu mpaka nikafika leo ninasiku ya tano nahangaika sana kutoa yale maji lakini bado hayataki kutoka masikioni yananifanya nishindwe kusikia vizuri alafu sina balance ya kichwa naomba kama kuna doctor anaeweza ku recommend nifanyaje please anisaidie niko nchini kwa watu hata english hawajui nimejaribu kwenda clinic nikakuta hatuelewani....
Rogers Akatoeli
Ndugu wewe kwani umekulia wapi ? maana hilo siyo tatizo hata kidogo kwa sisi watu wa ziwa victoria. cha kufanya weka maji mengine ndani ya hilo sikio ,halafu inamisha kichwa chako mara moja upande upande sehemu ya sikio lenye maji,BASI !!! hayo maji mapya utakayoweka ,yata kilieti vaqumu na yatayavuta yale mengine ndani ya sikio na yatatoka-watoto tulikuwa tunafanya hivyo. Nijulishe kama nimekusaidia, mimi siyo daktari wala nini,machinga tu. Zebedayo.
ReplyDeletejaribu kulalia upande wa hilo sikio lililoingia maji usiku huu, make sure unalalia upande huo huo usiku mzima bila kugeuka...utashangaa tu maji ya moto yametiririka ghafla kutoka sikioni, huwa nafanya hivyo maji yakiingia sikioni kwangu na mara zote huwa inasaidia kuyatoa nikifanya hivyo. yasipotoka huna jinsi ndungu yangu, itabidi utafute mkalimani ikiwezekana, ila nenda hospitali.
ReplyDeleteElekeza sikio lenye maji chini kisha gonga gonga kichwa opposite na ule wenye sikio lenye maji utaona matone yanatoka pole pole
ReplyDeletePole sana ndugu yangu kwa hali iliyokukuta.cha msingi fanya hivii..weka maji kwenye kiganja chako kisha yamimine kwenye lile sikio lililoingia maji hakikisha maji yameingia kwenye tundu ya sikio vizuri kisha kwa haraka inamisha sikio lako ili maji yatoke,hapo utaona na yale maji yaliyokuingia sikioni yanatoka pamoja na yale uliyoyaingiza.Ikishindikana kwa mara ya kwanza fanya tena.kama hukuelewa jinsi ya kufanya tafadhali wasiliana na mimi ili nikujulishe kwa njia ya simu.namba yangu ni +32 49 222 33 25 hata kama huna pesa kwenye simu yako fanya kunibeep then mimi nitakupigia.pole sana ndugu yangu kwa hali hiyo,najua jinsi unavyoangaika ila ni kitendo cha dakika tu kuyaondoa hayo maji.Hiyo njia ni rahisi na salama kabisa.natumaini kwamba utanielewa kama hukunielewa fanya mawasiliano nami.Maganga One.
ReplyDeletePole kwa tatizo hilo .Jaribu kulala upande wa sikio lenye maji na yatatoka .Jaribu kulalia huo upande kama dk. 10-15 hivi.Ikishindikana jaribu kumuona Dr. wa Masikio ,Koo na pua,huwa kuna mtaalamu wa kitengo hicho na ni tatizo dogo sana endapo utawahi.Kila la heri ,mdau na mtaalamu ktk medicine .Big Joe
ReplyDeleteHaihitaji doctor kaka yangu...kwa sisi wa pwani tulozoena kuogelea baharini tunalitambua hili. Hayo majo yaliyomo ndani ya msikio yameweka kama ngome na ndio maana hayatoki...sasa cha kufanya achukue maji kidogo kama matone mawili matatu aweke kwenye sikio hilo lenye maji na haya maji utakayoyaweka yatavunja hiyo kitu kama ngome na yote yatatoka....na kama haitasaidia muone doc...
ReplyDeleteHuko uliko,
ReplyDeleteSisitiza huko uonane na Wataalam wa (Head, Nose and Throat) 'HNT' ndio utapata msaada sahihi.
Kama ungekuwa hapa Dar ningekushauri uende Magomeni mwembe chai kwa Dr.Ole ,Dakitari mmoja Mmasai Bingwa wa masuala hayo ana hiyo Hospitali anaendesha.
wewe mdau wacha uzushi wako na ulimbukeni wa safari eti natafuta doctor wa kunisaidia kwani hii ni site ya madokta?
ReplyDeleteeti nimeenda kliniki hawajui english hahahaha kuna sehemu ikakosa hata mtu wa kukusaidia kuongea hicho kilugha cha hapo?
wacha kutujazia ukurasa wa ankali kwa vitu vya kijinga wewe mchimba chumvi rudi kwenu ukapigwe na vumbi
Unapenda starehe Unaogelea hadi ukiwa safarini. Huko unakoishi hakuna madaktari. Au unataka madaktari wa mtandaoni tu?
ReplyDeleteUshauri wangu ukome kufanya starehe za kuogelea ukiwa safarini.
Wacha fiksi ww labda umeenda viclinic cya vichochoroni. Misri imetawaliwa na waingereza na majority wanao gea kiingereza. Itakuwaje ukose wa kukuelewa?
ReplyDeleteNdugu yetu,
ReplyDeleteWewe hujui kuogelea halafu unazama bila utaratibu.
Kuogelea kuna basics zake za kufuata isipokuwa kwa chura na samaki wao kimaumbile wameumbwa tayari kwa maisha ya maji na hawahitaji maelekezo kama sisi viuombe wengine ambao maji sio makazi yetu!
wewe usiwe mjinga kiasi hicho chukua maji kwenye kiganja chako fanya laza sikio kiubapa kamavile unataka kuyaingiza sikioni tena kabla hayajaingia vizuri inamisha sikio chini yatatoka yote na yaliyokuwa ndani,jaribu nipe jibu au nipigie kwenye +255713450966 nikuelekeze vizuri
ReplyDeleteunatakiwa uzibe pua yako alafu usukume pumzi nje na hayo masikio yatafunguka
ReplyDeleteNdugu Rogers,
ReplyDeleteNaomba uwe mkweli omba usaidiwe lakini sidhani kama katika mahospitali ya Cairo hakutakua na daktari anaelewa kizungu au ni wewe umeshindwa kujieleza kizungu.
hivi mwenzetu darasani ulikuwaga unakuwa wangapi? umesoma vizuri lakini alichoandika au jazba tu na kusikia mbongo kaogelea nje ya bongo haaa haaaa
DeleteZiba pua na mdomo halafu fanya kama unameza mate mara kadhaa then nipe majibu
ReplyDeleteRogers Akatoeli tafadhali nitafute kwa namba 0654037007 nikusaidie
ReplyDeletekwa umbile la sikio jinsi lilivyo hayo maji hayaendi kokote zaidi, nadhani kinachokusumbua ni hali ya kutojisikia vizuri na kutosikia ktk kipindi hiki kuanzia sasa jaribu kulalia upande huo huo wa sikio lililokua na maji kutokana na mgandamizo mkubwa wa joto maji yatatafuta njia na yatatoka yakiwa ya ujoto, ni vizuri ukawa mtulivu yaache yaishe taratibu hakuna kubwa zaidi la kutisha zaidi ya kutojisikia vizuri tu.
ReplyDeleteDuuh wengine wanapaka na wengine wanatoa ushauri haya kazi kwenu..
ReplyDeletefuata ushauri wa juu wa kutia maji kwenye kiganja kwa sababu ni bubbles zimefanya kwenye ear canal mara tu ukitia maji zile bubble zitapasuka na maji yatatoka yote.
ReplyDeleteduh...pole sana...zeee zeee doktaaaz wamegomaaaaz
ReplyDeleteMtu kaomba msaada kidogo kelele nyingi msaada hakuna, kweli utu umekwisha. Na wewe ndugu yangu hata mkalimani hakuna?
ReplyDeleteKwani ulivyokua unaondoka uliaga vizuri kwa Mzee nanii?
ReplyDeleteRogers, umefurahisha sana jamvi leo hata mimi nimepatamo na mambo mapya, hizi ndizo mada nzuri za kuchekesha na kupeana maarifa,angalia mimi ,nilikuwa naijua njia moja tu ,kumbe ziko nyingi !!! Hongera sana Michuzi kwa kutoibania hii mada ya jamaa Roger, sipendi zile mada za kubishania dini, au Muungano-hizo mada zinaleta chuki na wala hazichekeshi,halafu watu wa UK wanakuwa wakali ukiwakosoa. Zebedayo
ReplyDeletePole sana ndugu yangu
ReplyDeletefugua bomba la kuogea la maji ya mvua (shower) inamisha kiwa upande wa sikio lenye maji fungua bomba maji yatoke kwa nguvu kidogo yawe yana ingia kwenye sikio lenye maji kama dakika 2 hivi nafikiri maji yote yatatoka unaweza kurudia mara 2-3 hivi mpaka maji ya ndani yatoke yote kama hujaelewa nibip nikupigie nikuelekeze zaidi 8190 4422 8555
Jamani Asante hiyo njia ya kuongeza maji imenisaidia maji yametoka..... God Bless you all.. Alafu sorry to say this mtu unapokua na shida lazima uwe desprate sana, ni mara yangu ya kwanza kufika kwenye hii nchi ya Souther Mongolia hakuna watu wanajua english zaidi ya hotelini ambako wameita tax tax ikanipeleka clinic kufika hapo ndo hatuelewani kabisaa.. hivyo sio uzushi
ReplyDeleteJamani mtu ameomba msaada wa tatizo lake, kwa nini kumsimanga?eti hakuna mkalimani, alikuwa wangapi darasani, aliaga kwao.... yote haya ya nini?? Angewaomba hela je?
ReplyDeleteRogers,
ReplyDeleteMshukuru Zebedayo na Mama K,sio tu wamekuelewa ila wamekupa ushauri mzuri. Umeona lakini wale waliodhani bado uko Misri? Umeona wale waliokupa ushauri wa dkt bila kukwambia useme kwa kiingereza kwa hao madkt? Maana hoja ilikuwa hiyo. zebedayo alianza vizuri baadae akapagawa na Sangara!
Zebedayo, umeona daraja la mbagala leo? Mti tu na mfereji umejaa taka halafu useme Bongo kumekucha!
Pole ndugu, pamoja na kashfa kibao lakini angalau umefanikiwa. Ila hapo juu kuna jamaa nae kachakachua! Eti kasema ukawaone madaktari mabingwa wa HNT (Head, Nose and Throat) ...... Aise? Ndugu yangu ni ENT (Ear, Nose and Throat).... Darasa la bure hilo mdau. Shukran Ankal, kweli blogu yako ni Shule ya aina yake. Twajifunza mengi humu ati......
ReplyDelete