Wanajumuia TANA Edmonton na Watanzania Canada na Popote Mlipo.
Nasikitika kuwafahamisha kuwa Mtanzania mwenzetu, Abraham Khamis (pichani), amekutwa amefariki dunia chumbani kwake hapa Edmonton. Baada ya kuwasiliana na ndugu wa marehemu huko nyumbani, Tanzanian Community Association of Northern Alberta (TANA) kwa kushirikiana na marafiki wa karibu wa marehemu tumeanza kufuatilia maswala ya kumzika mwenzetu huyu hapa Edmonton na makadirio ya gharama zilizopatikana kutoka funeral homes ni kiasi cha Can$ 7,000. Ili kuwezesha shughuli hii kufanyika, michango yenu ya hali na mali inahitajiwa. Tafadhali tuma mchango wako kwenye akaunti ya umoja wa WaTanzania, Edmonton (TANA) kama ifuatavyo:

Akaunti namba/Account No:  04089 003 1018118
Jina la Akaunti/Account Name: TANA

Au tuma kwa interac e-mail kwa: 
TANA President, H. Katalambula, hhhk2@yahoo.com,  
TANA Treasurer, H. Kuffar, henru98@yahoo.ca au 
TANA Secretary, G. Mollel,  gmollel@gmail.com.

Kwa maelezo zaidi au kutoa mchango wako kwa njia nyingine tofauti, wasiliana na:

Harrison Phudjo,   780 708 1996
Karama Arewi,  780 690 9674
Ally Salum (Babu),  780 680 5590
Ashraf Safi,  416 577 9375

Swala hili ni zito kwa hiyo ninaomba tusaidiane ili tuweze kumpumzisha mwenzetu.
Tafadhali sambazeni taarifa hizi kwa wote ambao mnadhani hawanazo.

Natanguliza shukrani.

H. Katalambula,
President, TANA. 
 1 780 218 4770 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2012

    INNALILAH WAINA ILAYHI RAJIUN...POLENI SANA WAFIWA

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2012

    jamani hebu nisaidieni hakuna vyma vya kufa na kuzikana kwa Watanzania wenzetu walioko nje?Au hakuna hata mfuko wa kusaidiana kwa nyie mnaoishi nje?Kwa kweli napata simanzi sana nionapo tangazo la tanzia la Mtanzania mwenzetu aliyefia huko,halafu kutwa kucha kuomba michango.Hebu jamani kuwe na chama kwa ajili ya haya mambo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...