Kiungo hodari wa timu ya Yanga,Haroun Niyonzima akiwachachafya mabeki wa timu ya Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo unaopigwa hivi sasa uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam,ikiwa ni hatua ya Robo Fainali ya Masindano ya Kombe la Cecafa Kagame.Kipindi cha Kwanza kilimalizika kwa Yanga kufungwa Bao 1 na sasa ni kipindi cha pili dakika ya pili ya Mchezo,Yanga wanasawazisha bao kupitia mshambuliaji wake Machachari,Said Bahanuz.hivyo mpaka sasa Matokeo ni Yanga 1-1 Mafunzo.mpira unaendelea.
Beki wa kati wa Yanga,Athuman Iddy akijiandaa kumtoka Kiungo wa Timu ya Mafunzo,Walid Ibrahim katika mchezo unaoendelea hivi sasa Uwanja wa Taifa.
Kelvin Yongani wa Yanga akichanja mbuga.
Hamis Kiiza yeye na kipa.
Wachezaji wa timu ya Mafunzo wakiomba dua.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...