“Enyi Mlioamini! Mmefaradhishiwa Kufunga (Ramadhani) kama Walivyofaradhishiwa
Waliokuja kabla yenu ili mpate Kuwa wacha Mungu.”
Madrassatul Noor Leicester ikishirikiana na An Noor Community Leicester za Uingereza kwa heshima kubwa zinapenda kuwaalika Waislamu wote waishio katika mji wa Leicester na miji ya karibu katika Darsa za mwezi wa Ramadhan za kila mwisho wa Wiki
-Jumamosi na Jumapili-
Na baadae kufuatiwa na Futari ya pamoja.
Kama ulivyo utaratibu wa miaka yote, familia na kila ataeshiriki anakumbushwa kuleta chakula kwa ajili ya Futari
Kumbuka, unapomfunguza mwenye kufunga, ujira wako ni sawa na wa mwenye kufunga!
Darsa na Futari Inshaallah zitaanza Jumapili 22-07-2012 na kuendelea kila Jumamosi na Jumapili za Mwezi wa Ramadhani
PAHALA: Madrassatul Noor Leicester, First Floor, Kocha House,
Malabar Road, Leicester, LE1 2PD
MUDA: Kuanzia Saa moja Kamili jioni (7.00pm) mpaka Magharibi
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana nasi:
Simu: 07792174408 / 07982124581 / 07903978481
E mail: madrasatulnoor.01@gmail.com
Wabillahi tawfeeq
RAMADHAAN MUBAARAK


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...