Wakimbizaji wa Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wakiwasili kwenye Viwanja vya Tangamano,Jijini Tanga Mchana wa leo.Wa tatu kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Mh. Halima Dendegu.
 Mwenge wa Uhuru Ukiwekwa katika sehemu yake Katika viwanja vya Tangamano Jijini Tanga ambako pia kunafanyika Tamasha la Wazi la Filamu nchini.Mwenge huo umefika uwanjani hapo kwa Kulipa Baraka Tamasha hilo ambalo linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake kisicho na Kilevi cha Grand Malt.
 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Cpt. Honest Mwanossa (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Tanga ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mh. Halima Dendegu wakisikiliza kwa makini salamu na utambulisho uliokuwa ukitolewa na Mratibu wa Mbio za Mwenge Mkoa wa Tanga.
Kiongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Cpt. Honest Mwanossa akimwagia mafuta kwa lengo la kuchoma moto nyavu za uvuvi haramu alizozikuta kwenye moja ya mabanda ya wajasilia mali.
  Nyavu za uvuvi haramu zikiwaka moto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...