Huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimerejea katika hali ya kawaida baada ya Madaktari kurejea kazini Jumatatu ya leo Julai 2, 2012.

Tathimini iliyofanyika kuanzia asubuhi saa mbili hadi saa 11 jioni inaonyesha kuwa katika Idara ya Tiba, Madaktari Bingwa 19 kati ya 21 wamefika kazini ambapo watatu wako likizo. Aidha Registrars wote 12 walikuja kazini. Kliniki zote za tiba zimefanyika kama kawaida.

Katika Idara ya watoto, yenye Madakatari Bingwa  16, kati yao 14 walikuja kazini wengine wawili wako likizo na Registrar watatu kati ya sita walikuja kazini ambapo watatu wako likizo

Upande wa OPD yenye Registrars saba, sita kati yao walikuja kazini na mmoja yuko likizo. Aidha Madaktari Bingwa wote walikuja kazini.

Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili  yenye Madakatri Bingwa 10, tisa walikuja kazini na mmoja wao yuko masomoni.

Upande wa Emergency Medicine, Registrars wote 10 walikuja kazini.

Kuhusu huduma za upasuaji, wagonjwa wote waliolazwa wodini wameonwa, na baadhi ya kliniki za huduma ya upasuaji zilifanyika. Hata hivyo, upasuaji haukufanyika kwani hakukuwa na orodha ya wagonjwa waliopangwa kufanyiwa upasuaji..

KWA UJUMLA, MADAKTARI WAMEREJEA KAZINI.

Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Julai 2, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2012

    Bila shaka kuna watu wengi kama mimi watakaofurahi kusikia habari hizo hapo juu.Jambo kubwa ni hakuna aliyeshinda na hakuna aliyeshindwa katika mgogoro huu.Nawaomba wale walio na madaraka wayaangalie matatizo ya mishahara ya madaktari. Mara nyingi wao huwa wanasahauliwa wakati wajanja wengine mishahara yako kila mara yapandishwa.Cost of living is going up and up, salaries need to be adjusted accordingly.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2012

    Kaazi kweli kweli. Hii ni hosipitali ipi ya Muhimbili?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2012

    Leo mchana nimeona kwenye ITV wakitangaza kuwa madaktari bingwa wa Muhimbili nao wameamua kugoma kuanzia leo na baadae kusoma press release ya hao madaktari wakidhibitisha kuwa wameungana na wenzao rasmi leo kugoma. Sasa hii taarifa ya kuwa madaktari wote wamerudi kazini leo inatoka wapi? Vipi kama wagonjwa wakeinda Muhimbili kesho na kukuta hakuna madaktari wa kuwatibu?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2012

    nadhani wengi hawajui hata wanachokigomea wanafuata mkumbo tu wasionekane wasaliti,rudini kazini bwana ningekua serekali ningepiga crush program yakupata madaktari kama 3000 kwa muda wa miaka minne kama mtaringa tena

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2012

    Kweli upeo wetu ni mdogo sana kwa mtaji huu! Crush program ya madaktari? Usiniambie unataka uue watu kwa kuleta madaktari wa "UPE".
    Danganyweni tu na wanasiasa na siku mtakapoambiwa nchi imepewa muwekezaji kama tunavyoona wanavijiji wakifukuzwa ndo mtatambua kwamba inabidi kuwapa support wasomi wenu.

    Mnaokumbuka kwamba mwaka 2001 tukiwa chuo kikuu tuligomea uanzishwaji wa tume ya mikopo na tukaitwa wahuni na wanasiasana baada ya hapo hata watu wa mtaani wakaandamana kutuita wahuni tusio na adabu na wengine walikuwa wanafunzi wa shule waliotumiwa na wanasiasa. Angalia leo madhara ya hiyo tume ambapo sisi tuliona mbali watoto wa waliotuita wahuni wangsoma bila matatizo lakini nashangaa kila siku wanagoma.....Jifunzeni kutafakari wanayoyadai wasomi na muache kurukia ya wanasiasa ambao wanapenda kuwadanganya kila siku.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 02, 2012

    Natetea fedha yetu ya kodi, tafadhali siku ambazo madaktari waligoma na kutofanyakazi wakatwe kwenye mishahara yao. HARAMU NA DHAMBI kuchukua kisicho haki yako

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 02, 2012

    Propaganda haitakuja saidia hii nchi.Mgomo uko palepale na madaktari mabingwa leo wamegoma..sasa aliepost hii press release arudi kuitoa polepole tu kwa aibu..!
    POLE SANA BWANA ELIGAESHI!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 03, 2012

    Tatizo kubwa ni ule utaratibu wa zidumu fikra. Hii taarifa ina lengo la kumfariji mwajiri ili aone kwamba wapo watendaji wanaotekeleza maagizo. Ukweli ni kwamba huwezi kumlazimisha mtu kama Dr kufanya kazi,ataripoti kazini nakusoma michuzi siku nzima. Tanzania tunasema tuna wasomi lakini walioko madarakani wamehudhuria tu madarasa maana mwenye elimu yake hawezi kufanya kazi kwa vitisho vya mwajiri kama huyu afisa uhusiano. bado tuna kazi kubwa mbele yetu lakini bila hawa wazee wetu waliong'ang'ania ofisi kuondoka, bado vijasa wasomi tutabaki kubeba mikoba yao na kuwafungulia milango. Umwinyi na ubwanyenye havitaisha hadi hawa waliochiwa nchi na mkoloni wapite, fikra mpya zitakuja kutoka kwa vijana wasomi na wenye uzalendo wa kweli kama J Makamba (anajitahidi), Zitto, Mnyika, na wengineo. Miaka kumi ijayo hatutakuwa na hawa babu zetu madarakani hivyo vijana tupendane, tuungane tuwe tayari kupokea nchi tusikubali kugombanishwa kwani wote tumekula mihogo na juisi za limao shuleni.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 03, 2012

    Mdau wa nne hapo juu, yako mambo ya kufanya crash program siyo hili, fanya crash program walimu na kungineko ambako madhara yake siyo ya mara moja au moja kwa moja, ufanye crash program Udacktari unataka waue watu badala ya kutibu, au wewe unadhani lele mama, ndo maana wenzako wanadai waongezewe mshahara mambo siyo mchezo, kama unavyofikiria.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 03, 2012

    Mara nyimgi migomo ikitokea ni wachache tu wanaunga mkono wengine huwa wanalazishwa na wakrofi tena wanafuatwa mpaka katika maofisi au vyumba vyao na kupigwa sisi tunawaona wanafunzi pale chuo kikuu tena doria inawekwa kila mahali hata vituo vya basi mabwenini wanatolewa. WASICHANA WANAPIGWA WENZAO WANATEMBEA NA BAKORA. Ili mradi kuna wakorofi wa migomo, Kuna watu ajira yao migomo kama akina bi BISIMBA NA USSU MALLYA.
    MIGOMO HAIKUANZA WAO WAMESHAFIKA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 03, 2012

    Natumaini kurudi kwenu kazini hakutatafsiriwa kuwa ni kushindwa bali ni moja ya changamoto katika kudai haki.

    Na kwa upande wa serikali sitarajii serikali ijigambe kuwa imeshinda kwa sababu ya vitisho. Ila walichukulie hili kama changamoto kwa upendeleo wanaojifanyia kwenye maslahi huku wengine wanaofanya kazi kama wao au pengine nzito kuliko wao wakiambulia makombo.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 03, 2012

    Hali hiyo hawajafanyiwa crash course, kutwa kukosea kuwatibu watu, mara mgonjwa wa kichwa anapasuliwa mguu. wa mguu kichwa, sindano za kulemaza watu na madhara kadhaa.
    Kwa nini mnaita madai ya muajiri vitisho? Nyie mnaojidai mmesoma, hamjui kama kuna kitu kinaitwa terms of employment? Serikali inajukumu la kukusomesha lakini halina lazima ya kukuajir, na kama itakuajiri basi kwa masharti yaliopo, hakuna nchi hata moja duniani masharti yakaandikwa na muajiriwa na kulazimishwa na muajiriwa.
    Huyo anayesema tujifunze wanaosema wasomi, wasomi gani hao wano-behave very unprofessional, unethical, inhumane and very very selfish indeed. Na propaganda naipiga nyinyi kuwaaminisha watu kuwa madaktari hawajarudi bado, wako waliorudi kwa taarifa yenu na wanakuwa intimidated na hao wenye ajenda zao za kisiasa, huyo mama bisimba anamwanae daktari kwa hiyo anahoja binafsi ikichangiwa na ya kisiasa. Yule mwingine Annanilea muda wake Tamwa umekwisha anang'ang'ania tu kiubabe sasa huyu anaweza kuwa advocate wa good governance, hana analolijua bumbuu anajua kuapayuka tu.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 03, 2012

    Madakitari:

    Kuna umuhimu tukatazama upende wa pili wa Shilingi ama kuwa na 'jicho la tatu' kuhusu madai yao.

    Pamoja na kuwa wote wamerejea kazini isiwe kuwa ndio suluhisho limepatikana kwa kuwa wasiwe wanafanya kazi nyeti kama hii lakini wakiwa na kinyongo, hii ni hatari sana kwetu!

    Kwa nini tusiangalie sula la kuwapa Mitaji ili waendeshe miradi nje ya kazi ili kujiongezea kipato cha ziada?

    Ili waweze kuziba pengo la upungufu wa kipato walichoomba?

    Ni jambo la tahadhari kuhudumiwa ktk suala nyeti kama afya na mtu ambaye moyo wake haujakunjuka!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 03, 2012

    Ni wauaji watajibu kwa muumba. WANGEKUWA HAWANA PESA WANGEENDA LEADRS CLUB. Madaktari wasomi wanatumiwa na baadhi ya taasisi kunyanyasa wanyonge.Endeleeni na mgomo na mungu halali anawaona na uroho wenu badala ya wito.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 03, 2012

    Unaweza mlazimisha punda kwenda mtoni lakini huwezi mlazimisha kunywa maji. Je mtatuhakikishiaje kuwa ni safe kutibiwa na hawa most demoralized and demotivated doctors??? Isije yakawa ya wa mguu kafanyiwa operation ya kichwa wa kichwa mguu

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 03, 2012

    NAIOMBA SERIKALI ISIWABEMBELEZE HAWA WATU WANAOJIITA MADAKTARI WA KUPASUA MTU KICHWA BADALA YA MGUUU, HAWANA UBINADAMU HATA KIDOGO WANAINGIZA SIASA KWENYE UHAI WA MTU KAMA MTU ANATAKA SIASA AACHE KAZI YA UDAKTARI AKAJIUNGE NA SIASA NA SIO KUCHEZA NA MAISHA YA WATU KWA UBINAFSI WAO NA KUTUMIWA NA WATU KWA FAIDA ZAO,KAMA KWELI WENYEWE WALIAMUA KUGOMA WANGEGOMA KUMTIBU NA HUYO MWENZAO INAMAANA YEYE MTU MMOJA WALIOONA MAISHA YAKE NDIO YANA THAMANI SANA KULIKO HAO WAGONJWA WOTE WALIOWATELEKEZA MAODINI BILA HUDUMA, KESHO KWA MUNGU MTAENDA KUJIBU VIFO MLIVYO SABABISHA NYINYI NA HAO WANAOWATUMA. WATANZANIA WANAAKILI TIMAMU NA WANAJUA KILA KINACHOENDELEA, NA HAWA KINA BISIMBA NA ANANIELY NKYA WAANGALIWE SANA HAWA WATATULETEA MATATIZO NCHINI SIONI KAMA WANA DHAMIRA NJEMA ZAIDI YA UCHOCHEZI.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 03, 2012

    CHADEMA OYEE KWA KUPIGANIA HAKI ZA MADAKTARI. WAO WANASUBIRI MIGOMO, WATU KUGOMBEA ARDHI ILI WAJIINGIZE, HIZO NDIZO SERA ZA KUICHUKUA HII NCHI. KWELI KAZI IPO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...