Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihudhuria kikao cha Ulinzi na Usalama cha Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa Ethiopia. Kulia ni Rais Robert Mugabe wa Zimbabbwe
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na kiongozi wa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini China Bwana Quan Zhezhu wakati walipokutana jijini Addis Ababa Ethiopia.

Rais Dkr.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na ujumbe wa wafanyabiashara wakubwa kutoka China Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2012

    Tafadhali Jk usiwe unawakubalia kila mwekezaji kuja kuwekeza nchini kwetu kwani inabidi kuwachuja kwa undani na kujua biashara zao kwanza.Tujifunze kutoka Botswana kwani hawa wawekezaji hawaoni umuhimu wa kuwekeza huko? kinachowashinda ni masharti yaliyowekwa na serikali ya Botswana kwa kulinda maslahi ya wananchi wake na taifa lake.Kuna siku hawa viongozi wetu watakuja sema sikujua kama hawa wawekezaji wangefanya hivi laini wakati huo ni mambo ya ninge, wange, haisaidii kitu.Mwekezaji yoyote lazima amwingize mtanzania awe na share na huyu mtanzania awe ndie anayehusika na kulipa kodi.Hii itasaidia serikali kupata mapato na hawa waekezaji kuacha mtindo wa kupata free tax exemption for 5Years na baada ya 5yrs wanabadilisha jina la kampuni na kupwea tena 5yrs free?Pia tuache kuuza Ardhi zetu kwa watu wa nje tutakuja nunu awkao miaka 15 ijao kwa bei ya juu kabisa.Pia wachina hawana vibali wanatengeneza saa,kubeba mizigo je watanzania wasiokuwa na elimu wafanye nini? Uhamiaji uko wapi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2012

    mkuu wa mwanzo nakuunga mkono na miguu yangu yote miwili kwa mawazo yako lakini kwenye blog hii wako wachache tu wenye kufikiri kama wewe na watendaji wapo wapi unamwambia mkuu wetu yanaingia sikiyo mmoja yanatoke sikio la pili

    mungu anaita

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...