- Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mgeni wake Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam kwa maongezi rasmi pamoja na dhifa ya kitaifa.
- Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiwa na mgeni wao Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam leo kwa maongezi rasmi pamoja na dhifa ya kitaifa.Hapa akisalimiana na Baadhi ya wanachunzi waliofika Ikulu kumlaki mgeni huyo. PICHA NA IKULU
Home
Unlabelled
RAIS KIKWETE AMKARIBISHA RAIS WA LIBERIA IKULU JIJINI DAR
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mapokezi mazuri sana, hakika ni heshima kwa nchi yetu
ReplyDeleteKAKA MICHUZI HIVI KUMBE BENDERA YA LIBERIA INAFANANA NA YA MAREKANI??NAOMBA KUJULISHWA TAFADHALI
ReplyDeleteLiberia ilikuwa moja ya state za marekani inasemekani hao wa Liberia ni baadhi wa watumwa waliorudishwa kutoka marekani na kupewa makazi hapo sina uhakika sana. anayejua atujuze pls
ReplyDeleteHawakurudishwa, bali kuna baadhi wa watumwa wenye asili ya Africa walikimbia utumwa huko marekani na walipotua na meli zao, wakafikia pwani ya Africa mashariki ndio ambayo ikaja kuwa nchi ya libelia, wakanzisha na serikali na utawala wao na bendela kila kitu, na jamii nyingine ya kiafrica kwa wakati huo walikuwepo eneo hilo , wengi wao walikua wanaishi mapolini mbali na pwani, na hao waliotoka marekani wakajita Americo, na kama unavyona bendela kama sehemu mmoja ya wamarekani
ReplyDeleteHongera! Hongera! Rais Kikwete pamoja na First Lady kum karibisha Rais wa Liberia. Wakati wa Kinamama sasa! Kwa Rais Kikwete pamoja na First Lady ni mafunzo makubwa kwa waTanzania kutoka kwa Rais wa Liberia. Kila kheri! Songa mbele Tanzania! Dr. Migiro 2015 iko karibu vipi wakinamama Tanzania? wakati ndiyo huu waku jitarisha! Je Tanzania iko tayari kuongoza na wakinamama!
ReplyDeleteTafadhali annanymous hapo juu fanya mapitio ya yale unayoandika kabla ya kutuma. Watumwa hao walifikia pwani ya Afrika ya Magharibi na siyo pwani ya Afrika ya Mashariki. Kuhusu bendera ya Liberia ina nyota moja tu tofauti na ile ya USA ambayo ina nyota nyingi kila moja ikiwakilisha jimbo (state)
ReplyDeleteUlishaona nchi zilizoendelea kuwa na mapokezi ya watu kibao wamejipanga barabarani? Tena wanafunzi. Shule kwishne kwa siku hiyo na kama kazi hakuna/hakuna uzalishaji. Tutazidi kuwa maskini milele.
ReplyDeleteHe siku hizi Liberia iko pwani ya Afrika Mashariki? Mkiambiwa msikimbie somo la Jiografia hamsikii!! Haya tena lete story na Tanzania iko pwani ya Afrika Magharibi lol!
ReplyDeleteAnonymous wa 12:46:00 masahihisho kidogo
ReplyDeleteHawakukimbia utumwa bali walikuwa ni watu weusi ambao waliweza kununua uhuru wao au walioweza kutunukiwa uhuru wao kutokana na vigezo fulani enzi hizo(wengi wao walikuwa mchanganyiko na wazungu-"half caste" au wasomi, au watumwa ambao walifanya kazi kwa wadhifu na kusababisha wamiliki wao wawaachie). Kutokana na kunyanyasika japokuwa walikuwa huru yaani wazungu bado waliwatenda kama vile watumwa kwa sababu ya rangi yao nyeusi ingawa walihesabika kuwa huru. Hawakuweza kumiliki ardhi, kupata kazi kama watu weupe na walithibitiwa katika mambo mengi. Kwa msaada wa Serikali ya Marekani, watu weusi hao wakashauriwa kurudi barani Afrika na kuanza maisha kama wakoloni katika nchi ya Liberia. Wakakabidhiwa silaha na fedha na kukwea kwenye meli mpaka Liberia. Kufika Liberia sasa, wao ndio wakawa kama watawala. Na wao wakaanza kuwanyanyasa waafrika ambao waliowakuta huko. Wakaipindua serikali na kuwa wamiliki wapya waliberia. Tokea hapo siasa ya Liberia ikawa ndio ya kupinduana tu na mavita kila siku kwa sababu waafrika asilia na watu weusi wahamiaji kutoka marekani walikuwa hawaelewani (na sababu zingine). Kwa hiyo Liberia ina bendera kama Marekani kwasababu ilikuwa koloni la Wamarekani (weusi na huru enzi za utumwa)barani Afrika.
Wanahistoria mbalimbali wanadhani kwamba hio ilikuwa ni njia tu ya kuwafukuza watu weusi hao kwa sababu uhuru wao ungesababisha watumwa wengine wagome au kwa kuwa hawakuwahitaji tena.
Dada J.
Halloo!!! Nasahisha hapo juu, sio Pwani ya Africa mashariki, ni magharibi, nilipitiwa wadau
ReplyDeleteMhe. Raisi JK nimegee kidogo na mimi !
ReplyDelete...umbea unanisumbua...
Je, kicheko chako picha ya chini kimeletwa na nini?
Nahisi Madame Ellen Johnson Sirleaf Raisi wa Liberia amevutiwa na Wanafunzi wa kike akakwambia ni wakati wao sasa wewe JK ukitoka Ofisini uwape na wao!