john_atta_mills_072412
Hayati John Atta Mills

Taarifa kutoka afisi ya rais zinasema kuwa alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali siku ya Jumatatu usiku.
Kifo cha rais wa taifa la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kupogania tena urais.Msaidizi wake pia amethibitisha kufariki kwa kiongozi huyo.
Rais Attah Mills ambaye husafiri mara kwa mara kwenda ng'ambo kwa matibabu alifariki muda mfupi baada y kupelekwa katika hospitali moja mjini Accra , Ghana.
Ni hivi majuzi tu rais huyo alisafiri hadi Marekani kwa kile kilichosemekana kwa ni uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Kwa muujibu wa katiba ya Ghana, Makamu wa Rais John Dramani Mahama anatarajiwa kushikilia hatamu za uongozi hadi uchaguzi wa urais utakapofanywa.
Ghana ilikuwa inatarajiwa kwenda katika uchaguzi mkuu mwezi Disemba mwaka huu ambapo John Attah Mills alikuwa ametangaza nia yake ya kutetea uadhifa wake.
Wakati wa uongozi wake, uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.
" Ni kwa masikitiko makuu na kwa moyo mzito... Tunatangaza kifo cha ghafla cha rais wa jamhuri ya Ghana " taarifa iliyotumiwa shirika la Reuters kutoka ofisi ya rais ilisema.
Tarifa hiyo ilisema kuwa Rais Mills mwenye umri wa miaka 68 alifariki saa chache tu baada ya kupelekwa hospitali.
Hata hivyo hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.
Lakini msaidizi wake mmoja ambaye hakutaka kutajwa, alisema kuwa Rais John Attah Millis alisikika siku ya Jumatatu akilalamika kwa anaumwa.
Hali yake ilizorota na hatimae kufariki mapema siku ya Jumanne.
Mills , anajulikana kwa kuanzisha uchimbaji wa mafuta nchi Ghana.
Chanzo: BBC SWAHILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 24, 2012

    Our prayers and thoughts are with your family and the entire nation of Ghana. RIP President Mills.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 24, 2012

    Huyu rahisi nilidhani ni Professor? Na kama ni kweli kwa nini msimpe heshima yake kwa kumwita prof maana amesotea hiyo title.

    Kwa ufupi Ghana kwa sasa iko kwenye middle class countries kama Malaysia. Jamaa amepiga kazi ...tuwaombee Wa Ghana wapate mrithi ambaye hatawarudisha nyuma kimaendeleo

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 25, 2012

    Unaeuliza kuhusu uprofesa upo sahihi,alikuwa profesa. Ila si lazima uitwe profesa hata kama umesotea kiasi gani. Huo ni ulimbukeni tu wa kibongo. Unajua kwamba Obama ni Profesa?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 25, 2012

    RambiRambi kwa familia ya Rais Mills pamoja na wananchi wa Ghana. Mungu amlaze pema. Amen.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...