Rais wa Liberia, Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 17 Julai, 2012 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. Ziara hiyo ya Mhe. Sirleaf inafuatia mwaliko wa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Sirleaf ambaye atawasili siku hiyo saa 8.00 mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, atapokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Akiwa hapa nchini, Mhe. Sirleaf anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo rasmi na Mhe. Rais Kikwete tarehe 17 Julai 2012, ikifuatiwa na Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake na Mhe. Rais Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Sirleaf pia anatarajiwa kuzindua Ofisi za Mradi wa Viongozi wa Afrika wa Kudhibiti Malaria (ALMA) tarehe 18 Julai, 2012 na siku hiyo hiyo Mhe. Sirleaf atatoa Mhadhara katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhusu “The Role of Women in African Development”.

Vile vile, tarehe 19 Julai, 2012 Mhe. Sirleaf atatembelea Kiwanda cha Kutengeneza Vyandarua cha A to Z kilichopo Arusha kabla ya kuondoka siku hiyo hiyo kurejea nchini kwake.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.

17 JULAI, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 16, 2012

    I wish ningeweza kuhudhuria huo mhadhara jamani!

    Mimi ni mwanaume, tena mchapakazi haswaa kwa mafanikio makubwa tu. Ila naamini kwa dhati kabisa kuwa mwanamke ni chachu kubwa sana ya maendeleo, zaidi mnooo kuliko mwanaume.

    Wanaume wenzangu, jinyime mwaka mmoja tu wa ubinafsi (ubabe) na uzingatie mkeo au mama yako anavyokushauri, nakuhakikishia utaendelea fasta fasta na utamuheshimu sana. Wana akili sana watu hawa, safi sana!

    Big up to my mother!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 17, 2012

    Karibu sanaa mama. ulimwengu utakombolewa na akina mama wenye uwezo kama wewe. Kina baba kazi yetu ni ketengeneza silaha na kuua. tutaachana lini na haya mauaji?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 17, 2012

    Haya akina mama mwenzenu huyo namefanikiwa muungeni mkono isiwe kama hspa spika analaumiwa zaidi na wanawake wenzie hata kuliko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...