RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein (pichani), ameiagiza Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo kuandaa utaratibu wa kupata fedha ndani ya wiki moja kwa ajili ya kununua meli kubwa mpya ya abiria wapatao 1000 na yenye uwezo wa kuchukua mizigo ya tani 100.
Dk. Shein ametoa agizo hilo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na uongozi wa Shirika la Meli pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Shirika hilo ambapo pia kikao hicho kilihudhuriwa na uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo.
Katika kikao hicho maalum Dk. Shein ameiagiza Wizara hiyo kutafuta fedha hizo kutokana na vianzio vya ndani au nje ya nchi ama kutokana na taasisi zinazohusiana na mambo ya fedha.
Alieleza kuwa katika kipindi kisichozidi miezi miwili ujumbe maalum uende kwa Kampuni zinazotengeneza meli nchini Korea Kusini, China au Japan kwa ajili ya kuwasilisha fedha za utangulizi kwa ajili ya ujenzi wa meli hiyo.
Mapema uongozi wa Shirika la Meli, ulimueleza Dk. Shein kuwa kwa kawaida ujenzi wa meli yenye ukubwa huo, huchukua mwaka mmoja kukamilika.
Kikao hicho ambacho kilikuwa na lengo la kuangalia mwelekeo na Mipango ya Shirika la Meli pia, kilijadili hali halisi ya meli za Shirika la Meli na baadae kujadili masuala ya ununuzi wa meli mpya itokayowaondoshea usumbufu wa usafiri wa baharini wananchi wanaosafiri kati ya Unguja, Pemba na Tanzania Bara.
Hili agizo ni zuri ila kama tulivyojijengea ufisadi kuwa ni mila yetu, utasikia meli itakayoletwa ilishatumika miaka mingi (used) au bei yake imezidishwa mara 1000... sijui tuna laana gani sie?
ReplyDeleteTulikua wapi siku zote kupanga huu ununuzi? Haya mambo ya zima moto yanasababisha baadhi ya mambo muhimu kutotiliwa maanani. Mf tunaweza kulazimika kuingia bank na kuchukua mkopo wa riba kubwa. Naombea tufanye vizuri katika hili.
Ignorant,
EU
Hiyo meli nadhani ni ndogo, ile Spice Islander iliua watu zaidi ya 2000, sasa wakiagiza meli ya watu 1000 huoni kama ni Risk nyingine hiyo? nadhani serikali ingekaa na kutafuta njia nzuri, nawashauri wanunue meli itakayoweza kuchukuwa abiria angalau 2500 na mizigo tani 500 ili kuondoa doubts, kila la kheri, Shain kazi yake tunaiona na InshaALLAh Mola atawasiaida.
ReplyDeleteWazo lako Mheshimiwa ni zuri na ni la kutia moyo ila je tofauti za kisiasa tayari zimeshaondolewa kabisa kabisa? Ikumbukwe kwamba serikali huko nyuma ilijali sana maslahi ya wananchi kwa mambo mengi likiwemo hili la usafiri kiasi cha kusimamia upatikanaji wa meli meli mpya iliyoitwa MV Mapinduzi. Meli hii ilikuwa ni kubwa na imara sana na ililetwa ikiwa ni 'brandy new' baada ya kutengenezwa na Niigata Engineering Company ya Tokyo, Japan. Ilikuwa ikifanya safari zake baina ya Zanzibar, Pemba, Dar es Salaam, Mtwara, Mombasa, Msumbiji na Komoro na haikuwahi kuwa na matatizo hata siku moja.
ReplyDeleteTatizo lililokuja kujitokeza ni tofauti za kisiasa ambazo zilisababisha wananchi wengi wa Pemba (ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliokuwa watumiaji wakubwa wa usafiri huu) kususia matumizi ya meli hii na nyinginezo za Shirika la Meli la Zanzibar. Hali hii kwa kiasi kikubwa ilisababisha Shrika kushindwa kujiendesha kibiashara na hatimaye kudhoofika sana. Zaidi ya hayo kuna watu walitumia tofauti hizo za kisiasa kuzifanyia hujuma meli za shirika ikiwemo hii ya MV Mapinduzi ili zife, kwa kiasi kikubwa walifanikiwa. Sasa je, changamoto hizo zinaweza kurekebishwa au ni kuzidi kuitia hasara serikali wakati tunakabiliwa na mambo mengine mengi tu ya kufanya zikiwemo huduma za kijamii kama za afya na elimu? Tafadhali tuwe wawazi na wakweli.
na meli itanunuliwaje ndani ya wiki moja? tutapata bomu bure! msichezee maisha ya sie wazenj
ReplyDeleteAhsante Mhe.Raisi Shein!,
ReplyDeleteUtaratibu utumike wa ICB (International Competitive Bidding) ili kumpata atakae fanya utaratibu wa manunuzi hayo ya meli ili tusije kuuvaa mkenge tena kwa meli mbovu.
"Ukubwa wa pua sio wingi wa kamasi"
ReplyDeleteDo not have a knee jerk reaction in solving this mess, ukubwa wa meli siyo tija, meli yaweza kuwa kubwa na ikazama vilevile, angalia Titanic, SS Morro Castle, Royal Pacific Cruise, hvi karibuni Costa concordia, Norwegian Dawn,Star Princess, Pacific Sun NK, zote zilikuwa ni meli kubwa tu.
Cha maana ni kufuata utaratibu wa safari, hali ya hewa ilikuwa mabaya sana, skagit haikutakiwa kuruhusiwa siku ile ya ajali.
We can`t panick in sorting this out, it we panick,the front part of the brain which deals with cognitive functions shuts down, the midbrain takes over (this part is useless at executing higher level cognitive functions!
We may still have Skagit size boats which are well serviced, not overloaded and don`t travell in extreme weather!
Dr Gangwe Bitozi.
Watu wakawaida wengi wana tegemea kusafiri kwa meli. Pongezi kwa Dr.Shein na serikali!
ReplyDeleteAnon no. 3 nakubalina na maoni yako. Mapinduzi ilikuwa 'Brand New' kutoka JAPAN. Nakumbuka na kanga zake zilitoka zilikuwa zimebaba maandishi yasemayo "MV MAPINDUZI FURAHA YA WAZAZI" kama kumbu kumbu zangu zipo sahihi na huku zikiwa na picha kubwa ya meli, leo hata kivuli chake hakipo waliokuwa wakinufaika na kuiangamiza ni hao hao 'Mtajiju'
ReplyDeleteNadhani kwa matukio haya mawili mfululizo ya ajali za Meli zilizopelekea kuwapoteza mamia ya wananchi wetu, wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki zetu, basi ingefaa liwe somo tosha lisilohitaji 'kudurusiwa' tena. Tatizo la viongozi wetu na khasa kwenye wizara/idara husika, huwa hawaangalii wala kujali au kufanya 'Risk assessment' katika baadhi ya mambo yanayoweza kuleta athari kwa binaadamu.jamii kwa jumla, mfano kama hivyo vyombo vya usarfiri ( wa bahari, nchi kavu na hata angani), madawa ya wagonja mahospitalini, vyakula vya makopo madukani n.k. Wao husubiria mpaka maafa au athari mbali mbali zinapotokea au kusikika, ndio wanaanza kukurupuka wakati maangamizo yameshatokea 'beyond repair'. Nadhani imefikia wakti sasa mikakati maalumu iwekwe na kufatiliwa ipasavyo ili tatizo linapojitokeza, iwe rakhsisi kujulikana chanzo chake ni nini au wapi na nani wa kulaumiwa na hatuwa gani za kisheria zichukuliwe.