Kutokana na maombi ya wengi, Ankal ameridhia kuanzisha  safu ya kila Jumapili inayohusu kubadilishana mawazo na utundu katika upigaji picha. Michango, maswali na mawazo chanya vinakaribishwa katika kuendeleza Libeneke hili ambalo Globu ya Jamii ina imani kuwa wengi wataliunga mkono - KARIBUNI.

Aghalabu huwa naulizwa na wadau hivi ni kamera gani bomba kuliko zingine? Mie huwa nna jibu rahisi sana kwa mdau wa aina hiyo;  Kwanza kabisa ni je, mfuko wako una kiasi gani kabla ya kwenda dukani kununua hiyo kamera? Nikishapata jibu, huwa najitahidi kutoa mawazo ya kamera gani itamfaa (kulingana na uwezo wake) na wengi wamefurahia matokea ya kufuata ushauri wangu.

Ushauri wangu wa pili ni kumuomba mdau anieleze anataka kuwa na kamera kwa matumizi gani? Nikipata jibu na kwa kuangalia uwezo wake, natoa ushauri husika na, hapa napo, wengi wamenufaika.

Hadi hapa najua wadau wengi watakuwa wanajiuliza Ankal anatumiaga kamera gani?  Well, mie ni mtu wa Canon. Hivi sasa natumia Canon EOS 5D Mark III (BOFYA HAPA) ambayo imetoka mwezi wa March, mwaka huu. Hiyo ni baada ya kutumia Canon EOS 5D Mark II  (BOFYA HAPA) kwa muda mrefu, na hiyo mpya ilipotoka nikaona si vibaya ku-upgrade. Na hadi sasa sijajutia uamuzi wa kutumia Canon, kwani kutokana na kazi zangu, kamera hii imekuwa na manufaa makubwa kwa kila hali.

Halahala wadau, sijasema kuwa Canon ndiyo kamera bora kuliko zote. Naomba nisisitize hapa kwamba hilo ni chaguo langu, kwani hakuna siku ambapo Canon imeniangusha katika kariban miaka 25 ya kupiga picha.

Na hili linanisogeza karibu katika mada yetu ya leo ya kuanzia safu hii, ambayo ni kusaka kamera iliyo bora. Jibu, kwa mujibu wangu, hii inategemea (i) Uwezo wako (ii) nini matumizi yako. Katika safu zijazo nitajaribu kuchambua kamera aina mbalimbali (pamoja na bei zake) ili mdau ujue ipi inayokufaa kutokana na matumizi yako.

Kwa wenzangu na mie ambao hadi leo wanaotumia kamera zenye kutumia filamu (sio digital), kwa maoni yangu, naomba wajitahidi waondoke huko. Sio kwamba kamera za filamu zimefutwa. La, hasha. Hii ni kwa sababu kamera za aina hiyo (filamu) zimekuwa adimu katika kuundwa na kusambazwa kwake, kutokana na maendeleo ya teknolojia.  Itafikia siku hata Studio za kusafisha picha za filamu zitatoweka, nasi tutajikuta matatani. Hivyo basi, kwa ushauri wangu, mdau unayetumia kamera ya filamu, jipeleleze na jiulize upya kama bado unapenda libeneke la picha.

Kwa leo naomba niishie hapa huku nikiomba maoni, ushauri, mawazo na hata changamoto ili kuifanya safu hii inoge.

-Michuzi






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. habari hii itatufaa sana hususan kwa sisi ambao hatukosomea mambo ya uandishi wa habari thanx sana michuz!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2012

    Bora umesikia Kilio chetu maana nilikuomba ushauri ukaniweka kapuni. Hayo Ndio mambo bwana "Lighting another candle does not dim your own"

    Mdau wako

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 15, 2012

    mimi sina matumizi makubwa ya camera ila sijawahi kununuwa kabila nyengine ila hii canon tu nakubaliana na wengine kuwa hili kabila nikiboko

    picha zinatoka safi sana nasubutu kusema kuwa canon is the best

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 15, 2012

    ANCLE KULIKONI KUTUMIA WINO MWEKUNDU?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 15, 2012

    Anko umefanya jambo la maana kweli Bei yake mbona Bomba 3,199$ Dahhhh

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 16, 2012

    Bei ya kamera kuli gharama za kijigari changu. Itabidi sasa Ankal tukufuate ukisinzia tunaondoka na kamera yako!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 16, 2012

    habari nimeipenda safu hii mimi natumia sony digital kwa matumizi ya nyumbani na vijimatukio ya kijamii sasa nikipiga sijajua setting hupiga picha huwa ndogo au mbali naomba ushauri

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 16, 2012

    Nami ni mpenzi wa canon kwa miaka mingi tu. Kwa sasa natumia Canon EOS 7D.
    Kama alivyoeleza Ankal matumizi na mfuko wako ni mambo muhimu.Mimi nafikiri kabla ya kukimbilia dukani kwanza jiulize unataka kufanya nini? Unataka kupiga picha za nini na za namna gani? Ni wapi utapiga picha na nyakati gani? baada ya kupiga picha zako utazifanyia nini(processing).
    Mashine hizi sio za 'hobby' je una ujuzi gani?
    Lazma ujue kuwa kulenga na kupata picha haiimanishi kuwa umemamliza kazi ya picha yako

    Mambo ni mengi naachia wenzangu wajimwage uwanjani pia.
    Pongezi kwa Ankal

    mdau BG

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 16, 2012

    Kwa kweli nami ni mtumiaji wa kamera kwenye vishughuli vya hapa na pale (visivyo vya kibiashara)kwa sasa natumia olympus inafanya sio vizuri saaana kihivyo lakini mbona nasikia eti Nikoni D3s ni the best?!!duniani lakini hata hivyo hizo unazotumia ni kali!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 16, 2012

    Ahsante anko kwa mipango mizuri.

    Tafadhali tueleze lensi unayotumia mara kwa mara, lensi ambayo kama ungeambiwa uwe na hiyo tu, ungeichagua hiyo.

    Natambua kua matumizi ya DSLR yanatoa fursa kubadilisha lensi kulingana na mahitaji ya mpiga picha. Hata hivyo kwa watu wanaopiga picha kwa upenzi tu na si biashara (si rahisi kupanga kutumia mamilioni yanayohitajika katika kukusanya lensi mbalimbali) watakua na swali moja tu, lensi gani ya kuanzia au inayoweza kufaa katika mazingira tofauti.

    ReplyDelete
  11. Ankal, mie nimenunua Canon 600D hivi karibuni.. Ni mgeni kidogo katika kutumia jamii hizi za camera. Napata shida na baadhi ya functions zake.. Unaonaje ukianzisha na darasa hata mara moja kwa mwezi hata kwa fee flani ili watu wajifunze kuzitumia vizuri? Mie ntakuwa mmojawapo wa wanafunzi wako kaka..

    Ditto

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...