Spika wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Magreti Nzziwa Nantongo (kulia), akibadilishana mawazo na Mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Shy Rose Bhanji.
Wabunge wa Afrika Mashariki Shy Rose Bhanji na mwenzake kutoka burundi wakibadilishana mawazo na spika wa bunge la Afrika ya Mashariki, Magreth Nzziwa (katikati), kutoka Uganda ambaye ni spika wa kwanza mwanamke toka kuanzishwa tena EAC.hapa wakiwa kwenye kikao cha kupanga kazi za mwaka za bunge hilo katika Hotel ya East Afrikan jijini Arusha.
Mheshimiwa Shyrose,
ReplyDeletekwanza hongera sana kwa kuchaguliwa kutuwakilisha katika Bunge la Afrika Mashariki.
Mbali ya Kushinda Uchaguzi, Jamani Mtuwakilishe vizuri, someni sana current International Affairs, muelewe Dunia inakwenda wapi?
Mjuwe National Interests zetu Kama Tanzania ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ni zipi, na mzisimamie na kuzipigania kwa nguvu zote.
Msione aibu kuomba ushauri, Tanzania ina Hazina kubwa wa watu wenye Uzoefu wa mambo mbali mbali lakini wanaweza wasiwe wabunge kama nyinyi.
Kikubwa Zaidi, Jaribuni kila wakati kuongea kwa Sauti Moja kama Taifa *Tanzania* kwa kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo na sera za Serikali yetu zinazohusiana na Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki.
Kila la Kheri