NILITOA TANGAZO KUWA NAMTAFUTA MZEE WANGU VICENT SASAGU KULIGI JUZI SIKU YA JUMATANO NIPELEKEWA HEWANI TANGAZO LANGU NASHUKURU SANA SINA CHA KUWALIPA ILA MWENYEZI MUNGU ATAWALIPA MICHUZI BLOG NA TIMU YAKO NZIMA NI MIAKA 36 SASA! MICHUZI INANIKUTANISHA NA MZAZI WANGU ASANTE ASANTE SANA

MDAU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2012

    Hata hii shukurani si ndogo, umeonesha kujali. Tunakutakia mafanikio mema.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 13, 2012

    Libeneke Oyeeee Ankal

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 13, 2012

    MBONA HUELEWEKI MDAU?INAMAANA UMESHAMPATA MZAZI WAKO?TOA BASI MAELEZO ILIKUWAJE?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 13, 2012

    Waahuu!Miaka 36!!!!
    Jamani,,Kweli ni michuzi Blog ya Jamii!
    Maana ukiangalia siku zote hizi kuna TV magazeti na vitu vingi tu ambavyo ungeweza kutangaza ukampata mzazi wako!lakini wapi!Hizi Thawabu zote zilikuwa zinamsubiria tu Bw.Issah Michuzi!
    Na sisi Mola atuwezeshe tuweze kufanya jambo kubwa kama hilo,hata kama kwa njia zingine,kama kuweza kumpa maji mwenye kiu kali,,au kumpa chakula mwenye njaa kali,,haijalishi unamfaham au laa!Hayo ndo malipo mazuri tuyonasubiria kutoka kwa Mungu,,,
    Michuzi umefanya jambo la maana,,duu! kumkutanisha mtu na mzazi wake waliochana kwa miaka 36!!,,Allah akuzidishie
    AHLAM,,UK

    ReplyDelete
  5. Nimefurahi pamoja na wewe kwa kumpata baba yako. Michuzi oyeeeeee

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 14, 2012

    wewe mzembe wa UK, lini sasa utaanza kutoa hayo maji kwa mtu mwenye kiu au chakula, mwenziyo michuzi kafanya kitu hiki kizuri kwa umma ,sisi sote tunakitumia tena bureee, sasa leo unaona ajabu Michu kumuunganisha jamaa na baba yake,eti unamwambia angalitumia magazeti au TV-siku hizi bongo chati ni computer tu ,watu wanalaptop mpaka Nzega. Michu, nimeleta masipika makubwa sana ya muziki mengi tu naomba anayehitaji,anitafute kupitia blog yako angalau nikiuza ,niweze kukushukuru. Zebedayo.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 14, 2012

    Mdau Mungu atakujalia tunasubiri siku kusikia umekutana naye InshaAllah.

    Zebedayo zarau wacha kuwa na roho hiyo unauhakika gani hatoi hayo maji au kusaidia? unaye mkashifu?? haifai ndugu yangu kuwa hivyo usipende kukashifu watu kwa kumuita mzembe hata humjui umerukia mzembe.

    Ahlam endelea kuwa na moyo wako mzuri hivyo hivyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...