Mjane wa Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere Mama Maria Nyerere akipeana mkono na Muigizaji wa filamu nchini kutoka Kundi la Bongo Movie,Steven Mangele "Stive Nyerere" pamoja na Wasanii wenzake alioongozana nao kwenda kumtembelea Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar.

Mwigizaji wa filamu nchini kutoka Kundi la Bongo Movie,Steven Mangele "Stive Nyerere" jana alikabidhi filamu yake aliyoiigiza kama Mwalimu Nyerere kwa Mama Maria Nyerere ikiwa ni kama shukrani zake, baada ya mama huyo kumsaidia katika kukamilisha filamu hiyo ambayo aliifanyia Butiama.

 Stive alisema kwamba kumpa filamu hiyo Mama Maria Nyerere ni kuweka kumbukumbu kwamba,anathamini msaada na mchango wake katika filamu hiyo na hana kikubwa cha kumpa wala cha kumfanyia zaidi. 

Amesema Mama Maria Nyerere alimsaidia sana katika kumuonyesha vitu gani mwalimu alikuwa akifanya, na vitu gani  mwalimu alikuwa akivipenda, na sehemu ambazo mwalimu alipenda kukaa baada ya kazi zake.

Pia ametoa shukrani kwa wasanii wenzake ambapo waliojitahidi katika hali moja au nyingine kuhakikisha filamu hiyo inakamilika.
Mama Maria Nyerere akisalimiana na Mwenyekiti wa Bongo Movie,Jacob Steven "JB".
Mama Maria Nyerere akiwa na Filamu alizokabidhiwa na Muigizaji,Steven Mangele "Stive Nyerere".
Mama Maria akitoa somo kwa Wasanii wa Bongo Movie waliomtembelea nyumbani kwake.
Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 06, 2012

    steve nyerere kila anapokaa ni maigizo tuu,sasa ona hapo utafikiri anasubiri mpira wa faulo hahahah

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 06, 2012

    Ama kweli Duniani wawili wawili, Julius Kambarage Nyerere ametutoka kimwili hayupo nasi lakini kifikra anaendeleza Steve Nyerere!

    Dogo anaweza!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 06, 2012

    Hongereni sana Wasanii wa Tanzania kwa kumuenzi Mama Maria Nyerere, Mama wa Taifa letu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...