Wapendwa wakereketwa wanachama wa CCM hapa DMV, tawi linaendelea na shughuli zake katika misingi ya uadilifu,uwajibikaji, heshima na ustamilivu na umoja kati ya viongozi na wanachama.

Kama tuluvyoweza kutoa taarifa hapo mwanzoni, azimio la kuanzisha tawi hili lilifikiwa mwezi November 5, 2011 hapa Maryland na wanachama wa ccm waishio maeneo ya DMV. Katika kikao hicho wajumbe waliweza kuchagua viongozi wa Tawi. Miongoni mwa mikakati ya chama katika kikao hicho ni kupata idadi mpya ya wanachama wakereketwa wa ccm waishio maeneo ya DMV.

Tunapenda kuwatangazia wakereketwa wa chama, tawi hili la ccm hapa DMV toka kuzinduliwa kwake rasmi November, 2011 limepata mafanikio yafuatayo:

1. Tawi limeweza kutambuliwa rasmi na makao makuu ya chama, kama moja ya matawi ya ccm nje ya nchi. Vile vile tawi limefanikiwa kuongeza idadi kubwa ya wanachama katika tawi katika kipindi hiki kifupi.

2. Mwenyekiti ameweza kufanikiwa kupata vifaa vya chama kama vile kadi za uanachama wa ccm na kopi za katiba ya chama.Tunapenda kutangaza rasmi kadi za CCM zimeanza kutolewa kwa wale wote ambao wanahitaji. Tafadhali wasiliana na viongozi wa Tawi ( Mwenyekiti na Katibu ili taratibu za upatikanaji zikamilike mara moja. Loveness Mamuya-240-423-0437 na Yacob Kinyemi 202-629-7841.

3.Chama kimeweza kuboresha hatua za mawasiliano kati ya viongozi na wanachama kwa kufungua posta na email address za chama hapo juu.

Viongozi walikubaliana hatua za kuwa karibu na wanachama wake ndani ya tawi ni kuwa na kurasa hizi za mawasiliano ili viongozi waweze kupokea maoni kutoka kwa wanachama ya kuboresha na kuimarisha sera za chama cha mapinduzi nje ya nchi.

Wapendwa wanachama wa ccm hapa DMV tunapenda kutangaza kutakuwa na sherehe za ufunguzi wa tawi letu hapa DMV zitafanyika rasmi August 25,2012 na kuudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama kutoka Makao makuu taifa na wabunge machachari ndani ya CCM.

Taratibu za vikao vya wanachama na viongozi kuandaa sherehe hizo zitatangazwa rasmi hivi karibuni. Tafadhali, tunomba wananchama wa ccm wajitokeze kwenye mikutano hii ya uandaaji wa sherehe za ufunguzi wa tawi. Kama tunavyojua sherehe hizi zitakuwa ni za kwanza kutokea katika kufungua tawi la CCM hapa Marekani.

Mwisho kabisa, uongozi unatoa shukurani kwa wanachama wote wa ccm hapa DMV walioweza kuchangia maoni mbali mbali na kufanikisha shughuli hizi za utendaji mpaka leo hii. Bado mikakati mbali mbali itahitajika katika kukiimarisha chama cha mapinduzi nje ya nchi.

Asanteni, Naamini tuko pamoja kuimarisha chama cha mapinduzi hapa Marekani.

Asante na Kidumu chama cha mapinduzi,

Yacob Kinyemi
Katibu wa ccm Tawi, DMV (Washington,DC Maryland na Virginia)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 13, 2012

    Tunawaunga mkono ndugu zetu wa CCM waishio Washington DC, Virginia na Maryland. Sababu ni moja tu: Chama cha Mapinduzi ndicho chama pekee Tanzania kinachoweza kuwaunganisha Watanzania wa makabila, rangi na dini zote na kudumisha amani tuliyoirithi kwa waanzilishi wa Taifa hili (our founding fathers) na iliyotufanya tuwe kisiwa cha amani katika bahari ya tufani na msukosuko. CCM ni kama ANC Afrika Kusini, SWAPO Namibia na FRELIMO Msumbiji.Mungu ibariki Afrika. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki CCM. Amen. Ngulumbalyo Mandai Mmatumbi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...