SERIKALI kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi leo, Ijumaa, Julai 27, 2012 majira ya saa tisa alasiri, imepokea notisi ya saa arobaini na nane (48) ya kusudio la walimu wanachama wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kugoma kuanzia Jumatatu tarehe 30 Julai 2012 saa moja na nusu asubuhi.
Kabla ya notisi hii kutolewa, Serikali imekuwa ikifanya jitihada nyingi za kujadiliana na viongozi wa CWT kuhusu jinsi ya kuboresha maslahi ya walimu kwa nia ya kumaliza suala hili kwa maelewano kwa kutumia vyombo na ngazi mbali mbali za kisheria.
Kwa sasa, shauri hili liko Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na leo hii siku ya Ijumaa tarehe 27 Julai, 2012 majira ya saa sita mchana pande zote mbili zilifika Mahakamani, na Mahakama ikaamuru kwamba pande zote zikamilishe maelezo yao ifikapo siku ya Jumanne tarehe 31 Julai, 2012 saa sita mchana, ili kuiwezesha Mahakama kuendelea kusikiliza shauri hilo na hatimaye kutoa uamuzi.
Kwa hiyo, Mgomo huu siyo halali kwa sababu shauri hili bado liko Mahakamani.
Kwa msingi huo hatua ya CWT kutoa notisi ya kuanza kwa mgomo kabla ya kukamilika kwa shauri hili ni kukiuka taratibu halali za Kimahakama ambazo kila mmoja anawajibika kuziheshimu.
Serikali inapenda kuwafahamisha walimu wote kuwa kujihusisha na mgomo huu ni kwenda kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu za kazi. Hivyo, walimu wanapaswa kupima madhara ya mgomo huu usiokuwa halali na Serikali inawataka walimu kupuuza mgomo huo na kutokujihusisha nao. Walimu wote wanatakiwa waendelee na kazi kama kawaida.
Peniel M. Lyimo
KAIMU KATIBU MKUU KIONGOZI
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
27 Julai, 2012
Kwangu mimi tangu niifahamu historir ya nchi yetu, sijawahi kusikia kuwa serikali imebariki mgomo wa jumuia au kundi lolote linalodai haki dhidi yake. Yote huwa ni batili ni lini ubatili huu utakuwa na ukomo!??
ReplyDeleteMimi ningekuwa ndo kiongozi wa Nchi hiyo, ningesha anua ngoma juani wakati ule Madaktari wanagoma, unajua ningefanyeje, ningefungua Flood gate kwa style, yaani, madaktari tufanye walikuwa wananidai mfano, nyongeza ya Tsh
ReplyDelete50,000/=waongezewe kwenye mishahara yao, Basi ningefanya hivi; ningekusanya makundi yote ambayo nahisi yangenidai baadae kama ningewapa Madaktari pekeyao,
na kuzigawa hizo Tsh.50,000/= kwa makundi yote kwa ratio maalumu nikianzia na madaktari wenyewe na hivyo wangeona aibu kunidai zaidi
Kwa namna hiyo ninge pre-empty madai mengi kama siyo yote.
Mfano kwa kutumia hiyo Tsh50,000/= wanayonidai Madaktari, ningetoa Tsh15,000/= kwa Madaktari, tsh 10,000/=kwa Walimu, labda Tsh 5,000/=kwa kundi jingine, Tsh5,000/=kwa wengine na kuendelea mpaka hiyo elfu hamsini iishe, halafu ningewaangalia kwa zamu nani mkorofi anadai zaidi, nadhani hakuna ambaye angenidai zaidi kwasababu wengine wangepata bila hata kutegemea hiyo ni neema kwao ni neema hiyo na madakta wangejisemea moyoni sasa tudai nini zaidi mbona amewapa na wenzetu.
Huko ndo nilikoita "to open a flood gate in style.
Ni mimi,
Mwana-Saikolojia ya watu.
Sasa wewe mdau wa pili unadai wanaogoma wapewe wanachodai. Fedha itakayotosha kuwapa itatoka wapi? Watu wachape kazi uchumi ukue waache kudai fedha ambazo taifa halina. Siku serikali itakapopata fedha za kutosha tutagawana mishahara minono kama tunavyogawana vyeo.
ReplyDeleteWaalimu msigome tulieni. Mtu anaponyolewa anatakiwa atulie vinginevyo atanyolewa vibaya.
Serikali imekula kwenu!!!!
ReplyDeleteMWALIMU mwenye akili timamu na aliyekabidhiwa jukumu la kuandaa vijana wanaojiamini, LAZIMA ASIKILIZE KAULI YA CWT,cwt ni chama ambacho kipo kwa mujibu wa sheria za jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
WALIMU tusisikilize neno lolote toka kwa wanyonyaji (serikali).
MGOMO UNAANZA JUMATATU SAA1:30asubuhi
Frankly speaking Tz inaonea sana imagine waalimu waliowafundisha Rais,mawaziri, wabunge na madaktari then tufikirie madaktari wanaoshika damu, usaha, mavi, mkojo n.k. Then think about mbunge anaekwenda bungeni kulala tangu achaguliwe hajawahi hata kusalimia wananchi wake hao ndo serikali inawajali mare than yule ambaye akikosekana inahatarisha maisha ya wananchi. Waalimu msikubali hadi kieleweke acheni kubembelezwa kwa pipi takeni mkate, maziwa, sukari na majani. Good luck
ReplyDeleteMdau UK
walimu wa msingi mbona wanapata mshahara mkubwa?wanapata laki nane wakati kuna secta nyingine wanapata kidogo.sasa hizo nyongeza zitatoka wapi jamani?
ReplyDeleteHaina haja ya kubishana sana. Katika pita pita yangu, nimekutana na sheria hii hapa. Anayesema wamekosea, atufafanulie wamekosea wapi.
ReplyDelete80.-(1) Subject to the provisions of this section, employees may engage in a lawful strike if -
(a) the dispute is a dispute of interest; strike
(b) the dispute has been referred in the prescribed form to the Commission for mediation;
(c) the dispute remains unresolved at the end of period of mediation provided under section 86(4) read with subsections (1) and (2) of section 87.
(d) the strike is called by a trade union, a ballot has been conducted under the union's constitution and a majority of those who voted were in favour of the strike; and
(e) after the applicable period referred to in paragraph (c), they or their trade union have given fourty eight hours notice to their employer of their intention to strike.
87.-(1) Where the employees or a trade union refer a dispute of interest to the Commission under section 86, the mediator may:-
(a) extend the period stipulated under section 86(4) by a further thirty days if the employees or union fail to attend the hearing arranged by the Commission;
(b) shorten the period stipulated in section 86(4) if the employer or employers' association party to the dispute fail to attend the hearing.
(2) Where an employer or an employers' association refers a dispute of interest to the Commission under section 86, the mediator may-
(a) extend the period stipulated under section 86(4) by a further thirty days if the employer's or employer association fails to attend the hearing arranged by the Commission;
(b) shorten the period stipulated in section 86(4) if the employees or trade union party to the dispute fail to attend the hearing.
wewe mdau hapa juu unakopi sheria za kazi unatuandikia iliiweje?soma vitabu mwenyewe huko yaaa.
ReplyDeleteJamani jamani waalimu msigome chondechone msiwasikilize hao chadema. Nchi haina fedha. Mshahara sh laki nane ni nyingi mno kwa taifa letu. Tuvumiliane kwani kazi ya ualimu na udaktari ni wito. Poleni lakini. Kama mdau hapo juu alivyosema "jitahidini mtulie wakati mnanyolewa vinginevyo mtanyolewa vibaya".
ReplyDelete